Kuhusu Moyo Wako

Kuhusu Moyo Wako

Joined
May 29, 2020
Posts
30
Reaction score
24
KUHUSU MOYO WAKO

BY: Mfalme Hadithi

Moyo huwa unadunda kwa nyendo tofauti kwa hali tofauti tofauti (different Apparitional)

Hivi ndivyo mapigo ya moyo hupiga kwa vipindi tofauti.

(1) UKIWA NA HASIRA

ukiwa na hasira mapigo ya moyo hupiga taratibu sana kutokana na ghadhabu ulionayo na hasira hukaribisha hali ya kushuka kwa mapigo ya moyo na hapo moyo hupata kazi kubwa ili kuweza kujisukumu yaani kujipump.

(2) UKIWA NA FURAHA

kwanza unapaswa kujua kwamba ukiwa na furaha mwili mzima unakuwa huru hata kama kuna magumu yaliyozunguka kila kona ya maisha yako. Hivyo basi wakati wa furaha moyo hudunda kwa wastani sana yaani sio sana wala sio kidogo namaanisha moyo wako unakuwa katika hali ya kawaida kabisa.

(3) UKIWA NA MAWAZO AU WASIWASI(HOFU)

wakati ambapo unakuwa na mawazo hofu au wasiwasi moyo wako hudunda kwa kasi zaidi na hali hii hupelekea kutokwa na jasho lisilo la kawaida na kama ni mtu mwenye presha au magonjwa hatarishi hali hii husababisha kuweka afya yako hatarini au mapigo ya moyo wako kusimama kabisa kwasababu ya kudunda kwa sasi sana.

(4) WAKATI WA KUKIMBIA
Unapaswa kujua kwamba wakati ukiwa unakimbia moyo wako huwa unadunda kama unasuasua kusimama. Na baada ya kukimbia moyo wako huanza kudunda kwa kasi sana.

(5) WAKATI UMELALA

wakati umelala moyo wako huwa unadunda kawaida lakini wakati wa kuamka kutoka usingizini moyo wako huanza kupunguza kupunguza kasi zaidi kwasababu ya kuanza mlolongo wa mawazo yaani kufikiria ufanyeje ili maisha yaende kwa siku hiyo ikiwemo namna ya kutafuta pesa n.k

Hivi ndivyo mapigo yako ya moyo yalivyo kwa hali tajwa hapo juu.

Imeandikwa na: mfalme

1593850105658~2.jpg
 
Back
Top Bottom