Kuhusu Mkataba wa kukodisha Bandari: Ni Rais na Mwenyekiti wetu tu ndiye awezaye yote tuyatakayo

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,135
17,802
Kwa mujibu wa Katiba na Sheria zetu zinazoliongoza Bunge, Rais ni sehemu ya Bunge. Kama Rais aliridhia (kwa kuusoma au kusomewa au kutafsiriwa mkataba wa kuikodisha Bandari yetu kwa DP Word) kusainiwa kwa mkataba huo, sehemu moja ya Bunge imeshaupitisha. Mnaelewa?

Kichama, Rais ni Mwenyekiti wa CCM. Bunge 'lote' linatokana na CCM. Kama Mwenyekiti ameuona; ameoneshwa; ameusoma; amesomewa; ametafsiriwa au ameutafsiri mkataba huo kabla ya kusainiwa kwake, kuna Mbunge wa kupimana ubavu na Mwenyekiti? Mnaandika lakini?

Amini nawaambia, mtu pekee wa kufanya vile watanzania wanavyotaka kuhusiana na mkataba huo (kuhusu masuala muhimu kama muda wa mkataba; maslahi tuyapatayo kama taifa; athari za hatari za mkataba huo; umuhimu wa mkataba huo na mambo mengineyo) ni Rais na Mwenyekiti wetu. Tuko pamoja?

Hakuna kama yeye. Ni yeye tu. Mengine yote yatakuwa ni maigizo kulingana na maagizo. Amini nawambieni, kama ilivyo ada, mtengeneza tatizo ndiye 'atakayelitatua'. Na atashangiliwa. Mnabisha? Subirini mjionee.

Caucus ina ukakasi wa kasi!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Dodoma)
 
Ni lazima bunge liunge mkono juhudi za serikali, hilo ni takwa la kikatiba, msisahau kuna mhimili uliojichimbia zaidi kwenda chini🐒
 
Scanned signature au alitumia mkono wake mwenyewe?
Screenshot_20230609-114708.png
 
Duh!.... VUTA-NKUVUTE tangu kipindi cha uchaguzi 2015 leo ndio naona post Yako...Aisee kweli Huwa mko Kwa kazi maalum!!!

Hasa kwa kazi kama hii...ya sakata la Bandari....

Enzi zile JK hakukosea aliposema "Vijana wa mitandaoni wakumbukwe"

Naona mmetumwa tena kubadili upepo mitandaoni kuhusu hili swala la Dp
world....

Nimewapa maua yenu...lumumba
 
Kwenye swala la kusoma na kufatilia mambo Rais wetu ni mvivu wa kusoma na kufatilia mambo kabisa kifupi ni mvivu sana yeye hana muda kila kitu anawaachia watu wahamue
 
Duh!.... VUTA-NKUVUTE tangu kipindi cha uchaguzi 2015 leo ndio naona post Yako...Aisee kweli Huwa mko Kwa kazi maalum!!!

Hasa kwa kazi kama hii...ya sakata la Bandari....

Enzi zile JK hakukosea aliposema "Vijana wa mitandaoni wakumbukwe"

Naona mmetumwa tena kubadili upepo mitandaoni kuhusu hili swala la Dp
world....

Nimewapa maua yenu...lumumba
Una uhakika?
 
Bahati mbaya ndio ameamua kututoa sadaka kwa wajomba zake, lazima watanganyika tujikomboe.
 
Back
Top Bottom