Kuhusu Kura Ya Wazi au Kura Ya Siri!

Profesy

JF-Expert Member
Jun 24, 2009
385
13
Baada ya msuguano wa #Posho, Bunge letu maalum la Katiba limepoteza karibu wiki nyingine nzima kubishana kuhusu uamuzi wa kuwa na Kura ya Wazi au Kura ya Siri. Tayari wiki mbili zimepita la Bunge la siku 70 (wiki 7) lakini yaliofanyika ni majadiliano ya Posho na hili la kura.Hili linatuonyesha kabisa wengi wa wakilishi wetu katika hili Bunge wameenda zaidi kimaslahi yao binafsi au ya kichama. Tunachosahau ni kwamba hili ni Bunge maalum la Katiba na walionda huko ni wawakilishi wa wananchi na maslahi yanatakiwa yawe ya wananchi na nchi yetu kwa ujumla (national interests).Ingawa nimejitahidi sana kunyamaza huku nikifatilia mitandaoni na kwenye magazeti, nimeona nisiendelee kunyamaza. Wiki hii nilichambua kitabu cha Chinua Achebe ‘There Was A Country: A Personal History of Biafra’ na kati ya mambo ambayo Achebe alihimiza ni kuwa waandishi lazima washiriki katika harakati za kisiasa. Kwa maneno mengine lazima waandike la sivyo watakuwa tu kama “footnotes”. Hilo ndo nililojifunza sana na ukisoma uchambuzi wangu utaona ata nimenukuu aya nzima kutoka kwa Achebe kuonyesha umuhimu wa kuandika. Hivyo nami nimeona nisikae kimya tena kuhusu hili swala la Kura ya Siri au Kura ya Wazi.Kidemokrasia kabisa na kwa mantiki ya Bunge Maalum kama hili la Katiba hoja yenye nguvu ni ya Kura Ya Wazi. Kwa nini? Kwa sababu zifuatazo:
  • Bunge hili linawakilisha wananchi katika makundi mbali mbali. Waliotumwa ni wawakilishi wa hayo makundi hivyo wanatakiwa maamuzi yao yawe wazi ili wanaowakilishwa wajue wawakilishi wao walisimamia lipi.
  • Kusema kuwa wawakilishi wataogopa vyama vyao na hawatakuwa na uhuru wa kusimamia wanachoamini ni UOGA na pia KUZALALISHA utume ambao wawakilishi hawa wamepewa na makundi yao na pia Rais. Wewe kama umepewa utume na nafasi kama hii ni kwamba umeaminika kuwa una uwezo wa kuchambua na kufanya maamuzi sahihi kwa ajili ya wananchi na Taifa. Kwa nini uogope leo kusema kwa wazi msimamo wako?
  • Kura Ya Wazi itasaidia wajumbe KUWAJIBIKA na maaumuzi waliofanya. Nimekumbuka sana kampeni za 2008 za Marekani ambapo Obama alimshinikiza Mama Clinton kuwajibika na kura yake ya kupitisha vita vya Iraki. Kura za jambo lile muhimu zilikuwa za wazi na ndio maana inajulika ni nani alipigia nini. Uingereza wabunge nao wanapiga kura za wazi kwenye mambo muhimu na wale ambao wanapingana na misimamo ya vyama vyao wanajulikana na huwa wanaitwa “rebels”. Na hii ni ilama ya demokrasia maana mtu ana uhuru wa mawazo na msimamo wake. Kwa mifano zaidi na michanganuo juu ya “rebellions in parliament” angalia Rates of rebellion, 1945-2014 | Revolts . Kwa hiyo hakutakuwa na neno kukiwa kuna “rebels” ambao watapingana na misimamo ya vyama vyao katika vifungu flani flani vya katiba. Huu ndio utashi wa kidemokrasia. Mbona Mbunge Esther ameweza kuwa kinyume na msimamo wa chama chake na kutetea kura ya siri? Hivyo angeweza pia kupiga kura ya wazi kwa jambo ambalo si sawa na msimamo wa chama chake.
Kwa kusema haya si kwamba nafungia macho hoja za wanaotetea Kura ya Siri. Hapana. Hawa wana hoja lakini hoja yao sio ya kidemokrasia, ni ya ki “context”. Kwa maana wanajua kuwa wajumbe wengi ambao ni wa CCM wataogopa kuwa na msimamo tofauti ya chama chao kama watapiga kura ya wazi.Hoja nyingine ya kura ya siri ni “mazoea”. Nimesikia wengi wakitoa mifano ya kura zinapigwa kwa siri, lakini hili ni Bunge la Katiba na kura zitakazopigwa sio za “kumchagua mtu” ni za vifungu vya katiba. Kwa nini iwe siri? Ingekuwa ni kura za kumchagua mgombea wa nafasi flani sawa, lakini ni ya kupitisha kifungu cha katiba kwa niaba ya wananchi. Hivyo hamna haja ya siri. Kura za siri zitafanyika wakati wa referendum ambapo kila mwananchi, binafsi kama mwananchi, ataamua uamuzi wake. Hapo Bungeni mko kama wawakilishi kwa maslahi ya makundi mnayo yawakilisha na wanananchi kwa ujumla na sio kwa maslahi yenu binafsi. Kwa ufupi ninasema, kama wewe ni mjumbe na hauwezi kusimamia unachooamini na kukisema wazi…huna maana maana hutaki kuwajibika. Tanzania tuacheni uoga.

SOURCE: Kuhusu Kura Ya Wazi au Kura Ya Siri #BungeKatiba | Aikande Kwayu
 
Baada ya msuguano wa #Posho, Bunge letu maalum la Katiba limepoteza karibu wiki nyingine nzima kubishana kuhusu uamuzi wa kuwa na Kura ya Wazi au Kura ya Siri. Tayari wiki mbili zimepita la Bunge la siku 70 (wiki 7) lakini yaliofanyika ni majadiliano ya Posho na hili la kura.Hili linatuonyesha kabisa wengi wa wakilishi wetu katika hili Bunge wameenda zaidi kimaslahi yao binafsi au ya kichama. Tunachosahau ni kwamba hili ni Bunge maalum la Katiba na walionda huko ni wawakilishi wa wananchi na maslahi yanatakiwa yawe ya wananchi na nchi yetu kwa ujumla (national interests).Ingawa nimejitahidi sana kunyamaza huku nikifatilia mitandaoni na kwenye magazeti, nimeona nisiendelee kunyamaza. Wiki hii nilichambua kitabu cha Chinua Achebe ‘There Was A Country: A Personal History of Biafra' na kati ya mambo ambayo Achebe alihimiza ni kuwa waandishi lazima washiriki katika harakati za kisiasa. Kwa maneno mengine lazima waandike la sivyo watakuwa tu kama "footnotes". Hilo ndo nililojifunza sana na ukisoma uchambuzi wangu utaona ata nimenukuu aya nzima kutoka kwa Achebe kuonyesha umuhimu wa kuandika. Hivyo nami nimeona nisikae kimya tena kuhusu hili swala la Kura ya Siri au Kura ya Wazi.Kidemokrasia kabisa na kwa mantiki ya Bunge Maalum kama hili la Katiba hoja yenye nguvu ni ya Kura Ya Wazi. Kwa nini? Kwa sababu zifuatazo:
  • Bunge hili linawakilisha wananchi katika makundi mbali mbali. Waliotumwa ni wawakilishi wa hayo makundi hivyo wanatakiwa maamuzi yao yawe wazi ili wanaowakilishwa wajue wawakilishi wao walisimamia lipi.
  • Kusema kuwa wawakilishi wataogopa vyama vyao na hawatakuwa na uhuru wa kusimamia wanachoamini ni UOGA na pia KUZALALISHA utume ambao wawakilishi hawa wamepewa na makundi yao na pia Rais. Wewe kama umepewa utume na nafasi kama hii ni kwamba umeaminika kuwa una uwezo wa kuchambua na kufanya maamuzi sahihi kwa ajili ya wananchi na Taifa. Kwa nini uogope leo kusema kwa wazi msimamo wako?
  • Kura Ya Wazi itasaidia wajumbe KUWAJIBIKA na maaumuzi waliofanya. Nimekumbuka sana kampeni za 2008 za Marekani ambapo Obama alimshinikiza Mama Clinton kuwajibika na kura yake ya kupitisha vita vya Iraki. Kura za jambo lile muhimu zilikuwa za wazi na ndio maana inajulika ni nani alipigia nini. Uingereza wabunge nao wanapiga kura za wazi kwenye mambo muhimu na wale ambao wanapingana na misimamo ya vyama vyao wanajulikana na huwa wanaitwa "rebels". Na hii ni ilama ya demokrasia maana mtu ana uhuru wa mawazo na msimamo wake. Kwa mifano zaidi na michanganuo juu ya "rebellions in parliament" angalia Rates of rebellion, 1945-2014 | Revolts . Kwa hiyo hakutakuwa na neno kukiwa kuna "rebels" ambao watapingana na misimamo ya vyama vyao katika vifungu flani flani vya katiba. Huu ndio utashi wa kidemokrasia. Mbona Mbunge Esther ameweza kuwa kinyume na msimamo wa chama chake na kutetea kura ya siri? Hivyo angeweza pia kupiga kura ya wazi kwa jambo ambalo si sawa na msimamo wa chama chake.
Kwa kusema haya si kwamba nafungia macho hoja za wanaotetea Kura ya Siri. Hapana. Hawa wana hoja lakini hoja yao sio ya kidemokrasia, ni ya ki "context". Kwa maana wanajua kuwa wajumbe wengi ambao ni wa CCM wataogopa kuwa na msimamo tofauti ya chama chao kama watapiga kura ya wazi.Hoja nyingine ya kura ya siri ni "mazoea". Nimesikia wengi wakitoa mifano ya kura zinapigwa kwa siri, lakini hili ni Bunge la Katiba na kura zitakazopigwa sio za "kumchagua mtu" ni za vifungu vya katiba. Kwa nini iwe siri? Ingekuwa ni kura za kumchagua mgombea wa nafasi flani sawa, lakini ni ya kupitisha kifungu cha katiba kwa niaba ya wananchi. Hivyo hamna haja ya siri. Kura za siri zitafanyika wakati wa referendum ambapo kila mwananchi, binafsi kama mwananchi, ataamua uamuzi wake. Hapo Bungeni mko kama wawakilishi kwa maslahi ya makundi mnayo yawakilisha na wanananchi kwa ujumla na sio kwa maslahi yenu binafsi. Kwa ufupi ninasema, kama wewe ni mjumbe na hauwezi kusimamia unachooamini na kukisema wazi…huna maana maana hutaki kuwajibika. Tanzania tuacheni uoga.

kaka nimekukubali. Ngoja nitulie kidogo, ntarudi kuchambua kwa hoja
 
.....Na mi binafsi sikubaliani na kupiga kura ya siri kwa hoja ya dhana ya UOGA, kama wao wanakiri kuwa ni WAOGA watatuambukiza sisi tuliowatuma kuwa waoga mara mbili zaidi kwenye nyanja mbalimbali, labda wapewe na semina juu ya dhambi ya uoga nadhani mh. Lema anaweza kuwa muwasilishaji mzuri wa mada....na ili kuondoa UNAFIKI baadae wa kila mtu kudai kwenye hoja fulani alipiga kura ya ndiyo au hapana akiangalia upepo wa kundi alilopo wakat huo bora kura ya wazi itumike hata hao CCM wanaoonekana itawabeba bado sidhani kama ni hivyo nnachokiona ni jinamizi la kura yako kukuandama hadi siku unaingia kaburini ni suala la unachezaje karata yako leo...
 
Baada ya msuguano wa #Posho, Bunge letu maalum la Katiba limepoteza karibu wiki nyingine nzima kubishana kuhusu uamuzi wa kuwa na Kura ya Wazi au Kura ya Siri. Tayari wiki mbili zimepita la Bunge la siku 70 (wiki 7) lakini yaliofanyika ni majadiliano ya Posho na hili la kura.Hili linatuonyesha kabisa wengi wa wakilishi wetu katika hili Bunge wameenda zaidi kimaslahi yao binafsi au ya kichama. Tunachosahau ni kwamba hili ni Bunge maalum la Katiba na walionda huko ni wawakilishi wa wananchi na maslahi yanatakiwa yawe ya wananchi na nchi yetu kwa ujumla (national interests).Ingawa nimejitahidi sana kunyamaza huku nikifatilia mitandaoni na kwenye magazeti, nimeona nisiendelee kunyamaza. Wiki hii nilichambua kitabu cha Chinua Achebe ‘There Was A Country: A Personal History of Biafra' na kati ya mambo ambayo Achebe alihimiza ni kuwa waandishi lazima washiriki katika harakati za kisiasa. Kwa maneno mengine lazima waandike la sivyo watakuwa tu kama "footnotes". Hilo ndo nililojifunza sana na ukisoma uchambuzi wangu utaona ata nimenukuu aya nzima kutoka kwa Achebe kuonyesha umuhimu wa kuandika. Hivyo nami nimeona nisikae kimya tena kuhusu hili swala la Kura ya Siri au Kura ya Wazi.Kidemokrasia kabisa na kwa mantiki ya Bunge Maalum kama hili la Katiba hoja yenye nguvu ni ya Kura Ya Wazi. Kwa nini? Kwa sababu zifuatazo:
  • Bunge hili linawakilisha wananchi katika makundi mbali mbali. Waliotumwa ni wawakilishi wa hayo makundi hivyo wanatakiwa maamuzi yao yawe wazi ili wanaowakilishwa wajue wawakilishi wao walisimamia lipi.
  • Kusema kuwa wawakilishi wataogopa vyama vyao na hawatakuwa na uhuru wa kusimamia wanachoamini ni UOGA na pia KUZALALISHA utume ambao wawakilishi hawa wamepewa na makundi yao na pia Rais. Wewe kama umepewa utume na nafasi kama hii ni kwamba umeaminika kuwa una uwezo wa kuchambua na kufanya maamuzi sahihi kwa ajili ya wananchi na Taifa. Kwa nini uogope leo kusema kwa wazi msimamo wako?
  • Kura Ya Wazi itasaidia wajumbe KUWAJIBIKA na maaumuzi waliofanya. Nimekumbuka sana kampeni za 2008 za Marekani ambapo Obama alimshinikiza Mama Clinton kuwajibika na kura yake ya kupitisha vita vya Iraki. Kura za jambo lile muhimu zilikuwa za wazi na ndio maana inajulika ni nani alipigia nini. Uingereza wabunge nao wanapiga kura za wazi kwenye mambo muhimu na wale ambao wanapingana na misimamo ya vyama vyao wanajulikana na huwa wanaitwa "rebels". Na hii ni ilama ya demokrasia maana mtu ana uhuru wa mawazo na msimamo wake. Kwa mifano zaidi na michanganuo juu ya "rebellions in parliament" angalia Rates of rebellion, 1945-2014 | Revolts . Kwa hiyo hakutakuwa na neno kukiwa kuna "rebels" ambao watapingana na misimamo ya vyama vyao katika vifungu flani flani vya katiba. Huu ndio utashi wa kidemokrasia. Mbona Mbunge Esther ameweza kuwa kinyume na msimamo wa chama chake na kutetea kura ya siri? Hivyo angeweza pia kupiga kura ya wazi kwa jambo ambalo si sawa na msimamo wa chama chake.
Kwa kusema haya si kwamba nafungia macho hoja za wanaotetea Kura ya Siri. Hapana. Hawa wana hoja lakini hoja yao sio ya kidemokrasia, ni ya ki "context". Kwa maana wanajua kuwa wajumbe wengi ambao ni wa CCM wataogopa kuwa na msimamo tofauti ya chama chao kama watapiga kura ya wazi.Hoja nyingine ya kura ya siri ni "mazoea". Nimesikia wengi wakitoa mifano ya kura zinapigwa kwa siri, lakini hili ni Bunge la Katiba na kura zitakazopigwa sio za "kumchagua mtu" ni za vifungu vya katiba. Kwa nini iwe siri? Ingekuwa ni kura za kumchagua mgombea wa nafasi flani sawa, lakini ni ya kupitisha kifungu cha katiba kwa niaba ya wananchi. Hivyo hamna haja ya siri. Kura za siri zitafanyika wakati wa referendum ambapo kila mwananchi, binafsi kama mwananchi, ataamua uamuzi wake. Hapo Bungeni mko kama wawakilishi kwa maslahi ya makundi mnayo yawakilisha na wanananchi kwa ujumla na sio kwa maslahi yenu binafsi. Kwa ufupi ninasema, kama wewe ni mjumbe na hauwezi kusimamia unachooamini na kukisema wazi…huna maana maana hutaki kuwajibika. Tanzania tuacheni uoga.

SOURCE: Kuhusu Kura Ya Wazi au Kura Ya Siri #BungeKatiba | Aikande Kwayu

Nimekusoma!.
Pasco
 
Back
Top Bottom