Makonyeza
Member
- Feb 2, 2020
- 69
- 252
Nimepitia kurasa kadhaa katika mitandao ya kijamii kama Facebook, magroup ya WhatsApp na Jamii Forums watu wakiijadili kauli ya Rais WA Zanzibar Dr. Hussein Ally Mwinyi alioitoa akikisisitiza kwamba Mtanzania Bara haruhusiwi kumiliki ardhi KISIWANI Zanzibar.
Wengi wa wachangiaji wameonekana kutokubaliana na kauli yake na wengine wakienda mbali zaidi kuulaani Muungano kuonekana hauna maana wakilinganisha na ukweli kwamba Mzanzibar anaruhusiwa kumiliki ardhi Tanganyika kwa Kadri ya uwezo wake.
Suala ka Mungano ni suala mtambuka linalohitaji Mijadala yake binafsi. Na naomba nikiri na mimi kwamba ni kweli Muungano una changamoto zake nyingi tu, inazohitaji hekima za viongozi wetu katika kuzitatua. Leo sitozungumzia sana huko, nitajikita hapa kwenye suala la ardhi tu.
Kwanza ifahamike Ardhi si jambo la Muungano. Naam, si suala ambalo nchi hizi mbili Tanganyika na Zanzibar zimekubaliana kushare kwa mujibu wa ule mkataba wa Muungano uliosainiwa na wazee wetu.
Hii ndio kusema kwamba kila upande wa Muungano una ardhi yake na sheria zake binafsi zinazoongoza na kusimamia matumizi ya ardhi kwao.
Na ni kwa sababu hiyo Zanzibar ina wizara yake ya ardhi kama ilivyo kwa serikali ya Muungano(ilipaswa iwe serikali ya Tanganyika).
Sasa basi, kwa mujibu wa sheria ya ardhi ya Zanzibar, sharti la mtu kumiliki ardhi ni lazima awe Mzanzibar wa kuzaliwa(Zanzibariz by birth), wakati huku kwetu Bara sharti ni kuwa Mtanzania tu inatosha kumilikishwa ardhi,bila kujali huo utanzania wako umeupataje, almuhimu iwe ni uraia halali kwa mujibu wa sheria zetu (wa kuzaliwa au wa kuomba).
Sheria zetu hutungwa kwa malengo, kila sheria ikitungwa hutungwa kwa sababu, ikilenga jambo au dhamira fulani.
Zanzibar ina eneo la Ukubwa wa kilomita za mraba 1650(wengine wanasema 2000),wakati Tanzania Bara Ukubwa wake ni kilomita za mraba 945,000 ikiwa ndio nchi yenye ardhi kubwa zaidi kuliko nchi zote za Afrika ya nashariki.
Sasa kutokana na udogo wa ardhi ya Zanzibar ndipo ilipokubaliwa kwamba isiwe sehemu ya Muungano na sheria rafiki itungwe ili kuilinda ardhi hiyo.
Kumbuka ndani ya kilomita hizo za mraba 2000 (ambazo ndo ndogo hata kwa Jiji la Dodoma kwa zaidi ya kilomita za mraba 600), Wanzanzibar wapatao 1,500,000/-(kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2012)wanahitaji ardhi kwa matumizi ya makazi, maeneo ya wazi, viwanda na Uwekezaji, ardhi ya akiba, ardhi ya mkakati wa kimazingira kuhifadhi uoto wa asili na misitu, huduma za jamii(hospital na mashule/vyuo) na kilimo japo cha kiwango cha kawaida(small scale farming).
Ukigawanya Ukubwa wa ardhi iliyopo na idadi yao unakuta ardhi waliyonayo ni ndogo sana. Na wasiwasi upo kutokana na kasi ya ongezeko la idadi ya watu kutokana na kasi waliyonayo kwenye kuzaliana ambayo inatajwa ni asilimia 4 kwa kila mwaka(wenzetu wanazaliana sana), kuna kila dalili Kuna wakati ardhi ya Zanzibar haitowatosha hata Wazanzibar wenyewe. Kwa kuangalia mbali ililazimu kuweka mazingira ya kuilinda ardhi Yao.
Pengine kama haitodhuru Sasa wangepaswa kuanzia kujipanga kugawa ardhi kwa kwenda juu, yaani hati ya ardhi itolewe juu ya nyumba iliyokwishajengwa.
Sasa nirudi kwa kauli ya Rais Hussein Mwinyi, inawezekana maneno aliyotumia hakueleweka, lakini alichomaanisha ni kwamba kwa ardhi ya Zanzibar kila mtu ataruhusiwa kumiliki lakini kwa utaratibu tofauti na unaotumika huku kwetu Bara.
Kwa maana kwamba, kwa wa Zanzibar kumiliki ardhi watatakiwa kuthibitisha uzanzibar wao kwa kuzaliwa. Na kwa asiye MZanzibar atamiliki ardhi kwa njia ya Uwekezaji pekee. Yaani anaweza kusajili kampuni ndani ya Zanzibar na kampuni hiyo kwa sababu umesajili wa Zanzibar itaruhusiwa kumiliki ardhi (zingatia kwamba Kampuni ni mtu kisheria, yaani legal person).
Na kwa kusajili kampuni bila shaka dhamira ya mwenye kampuni ni kuwekeza sehemu fulani, Ndiyo kauli ya Mheshimiwa Rais Mwinyi ilitokea hapo.
Hivyo ndivyo ilivyo hata huku kwetu Bara, licha ya haki ya kumiliki kuwa wazi kwa Mtanzania yeyote, lakini umiliki huo una Kikomo, unaweza kupewa miaka 33,66 au 99, Yote ndo yale yale tu, ni sawa na Abdallah kumuita Dulla tu. Muda huo ukiisha ardhi si yako inarudi kwa Rais. BADO umekodishwa hujamilikishwa.
Lakini tusijisahau, sababu wanayoitumia Zanzibar kutoruhusu wasio wa Zanzibar kumiliki ardhi, kimsingi Ndiyo tunayo tumia na sisi kukataa kufungua mipaka ya jumuiya ya Afrika ya nashariki kwenye ardhi kwa kuhofia Wakenya kuja kuitwaa ardhi yetu yote(jambo ambalo binafsi silikubali)
Kwako Mtanzania Bara, kama unataka kumiliki ardhi Zanzibar ni rahisi sana, nenda kasajili kampuni, utapata kibali cha kufanya biashara Zanzibar, then tumia kampuni yako kuomba ardhi, utapewa bila kinyongo.
Muungano udumuuuuuuuu