Kuhusu kukaribisha wageni chakula

Keeping it real wapi, uchoyo tu,tena kabisa anawaambia oh bajet sijui nini,..wapi mtaishi msipate wageni wa ghafla??? Ndo afrika hii hamjazoea tu?
Angalia scenario hiyo utaelewa kwa nini imembidi aanze kuongea mbele ya wageni, wanaishi wawili wenda ni tabia ya wageni wa mwenzake na usikute wamewekeana code of conduct tangu waanze kuishi.
 
wewe ni mpumbvau busara huna...ndio hawajatoa taarifa basi ungekul akimya kimya tu....au munge share hicho....acha roho zakimaskini hizo...hata kiepe mngewanunulia
 
Wewe unafanya kazi gani? daaah ! unahitaji kuombewa pepo likutoke hilooo ungekuwa karibu then unanisimulia hivi ningekuzabaa
 
Kwa sisi waafrika ni bora mwenyeji usile wageni wale hata kama hawajatoa taarifa.
Tulishawahi kuharibikiwa na gari njiani wenyeji wetu walitupa chakula na malazi bure huo ndio uafrika.

Wewe ni mchoyo.
Ni kweli mkuu...siku moja hubby alikaribisha mates wake akiwemo mzungu m1. Mzungu alishangaa kwann sipakui msosi nkamwambia nahakikisha kwamba wagen wote wamepata. Akanambia kwetu (Norway) mwenyeji ndo anakuwa wa kwanza kula. Huyu mleta uzi ajirekebishe. Na achukulie kwa kuleta kwake hoja yake hii hapa jukwaan Mungu anataka kumbadilisha. Maana wachangiaji wengi wamemtupia lawama. Acha uchoyo okoyoko
 
Kwa sisi Waswahili hapo umefanya kosa kubwa sana.

Mimi ndio maana huwa sipendi kula kwa watu hata kama nna njaa ukinikaribisha, ntajifanya nimeshiba.

Masimango, hasa ya chakula huwa siyapendi.

Huwezi kunisimanga kwa ajili ya chakula.

Afadhali wewe umeongea moja kwa moja, kuna wengine hawaongei ukiaga umewapa mgongo, watanung'unika mpaka basi
 
Carl peters wewe!!
Hitler wewe!!
ebo!!
Musolin mkubwa wewe!!
Mkoloni mkubwa sana wewe!!
Au unataka niendelee..,?
 
Mimi nisingefanya kama ulivyofanya wewe, lakini ulichofanya ni sawa tu hawakuwa kwenye ratiba wacha waisome namba!!
 
Tatizo ulilonalo ni kubwa kuliko unavyodhani.
 
aibu sana,mbona tunakufa tunaviacha.daaa,unaroho mbaya balaaa
 
Watanzania hawako hivyo mkuu.

Unawanyima watu M**avi?
 

MKUU,
UNGEWEKA PICHA HATA YA KATUNI INGESAIDIA KIDOGO.
 
mhn,umefanya wewe lakini aibu naona mimi mkuu,chakula! sidhani kama hao wageni walikuja kwa nia ya kula tuu sema ni incidenc wakaja muda wa chakula,mimi siwez kumnyima mtu chakula kama anataka kula,ningekuwa mm msosi tungekula pamoja kama sikushiba ningecheki utaratibu wa kula tena wakishaondoka nijazilize hata na chips kavu ila sio kwa makavu hayo.africa utamaduni wa kunyimana mavyakula kwa staili hyo hakunaga.zpo style nyingine ila sio hyo.
 
Chakula ni mavvi tu....
No uchoyo uliopitiliza kumnyima mtu
 

Yani wewe kama kweli sio unabwatuka tu hapa kuwa unaweza mpa 500k every month mzazi wako na chakula cha mara moja tu cha mgeni kinakutoa roho; then evil is truly devouring the world! And sidhani kama unaweza kuwa mwema hivyo at the same time ukawa mchoyo hivyo, I seriously doubt that!!!
 
Nakumbuka enzi zangu nilikua nikipika naenda kutafuta washkaji zangu oya njoo tule. Kula alone nilikua naona chakula hakipandi.
 
Ndugu Afrika itabaki kuwa Afrika na mambo yake na magharibi na mambo yake. Huwezi kuishi kifikra Ulaya ambako hujawahi fika wakati physically upo Afrika zaidi utaonekana fedhuli fulani. Mgeni haji kula ila kwa desturi zetu za Kibantu ni lazima aguse kidogo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…