Kuhusu kufungiwa kwa baadhi ya vyuo na vingine kufutiwa usajili.

AKILI TATU

JF-Expert Member
Feb 10, 2016
2,658
2,804
Hivi ili suala la baadhi ya vyuo kutosajiliwa na bado vinadahili wanafunzi limekaaje?

Na je wanafunzi au mwanafunzi aliyesoma chuo kama hiki anasaidiwaje na serikali hali wakati anajiinga hakuna anajua taarifa za chuo husika kama kimesajiliwa au lah?

Na kuna hivi vyuo ambavyo vilikuwa vimesajiliwa kwa muda au vilipata usajili wa kudumu lakini wakafutiwa usajili ,je wanafunzi waliohitimu katika vyuo hivi vya kati wanajiendeleza vipi ili hali vyuo hivyo vimefutwa kwenye mfumo wa nacte na matokeo yao hayapo kwenye tovuti hiyo?

Naomba Mwenye kujua anijibu kiufasaha.
 
Wazimamizi wa vyuo ongezeeni kasi ya kuvifuatilia vyuo binafisi hasa vya afya vitu vinavyofanyika kwenye vyuo hvyo ni kuizika taaluma ya afya
1 rushwa za ngono
2,rushwa ya pesa
3,wizi wa mitihani
4,usimamizi mbovu wa mitihani
5,wanachuo kujaziwa marks bure bila kufanya hata mtihani ilimradi kampa mwalimu pesa au penzi
Taarifa nawapeni inapofika kipindi cha Mitihani ya wizara kila mwalimu wa somo husika hufanya kila linalowezekana ili aweze kupata majibu ya somo husika ili aweze kuwagawia waliompatia pesa au penzi ,sisi tulioko nje ya mfumo tunayaona haya na so kazi kubwa kuyafahamu ni jambo la kufuatilia tu kidogo mtawakamata tofauti na hapo mtakuja kupata wataalamu wasiofaa wanatoka vyuo binafisi na kuua watu maana huwajui kitu wana vyeti lakini walikuwa wanatoa rushwa tuuuu mwanzo mwisho,
 
Back
Top Bottom