kidadari
JF-Expert Member
- Jul 26, 2012
- 8,647
- 9,574
Imekuwa ni kawaida kwa jamii siku hizi hasa vijana walio wengi ambao hawana ajira kuomba kazi hata kama hazijatangazwa. mimi ni mhitimu wa chuo kikuu nikiwa kama husika wa hili (mimi) na rafiki zangu tumekuwa tunazunguka ofisi zaidi ya 50 ndani ya miezi miwili hapa mjini kupeleka barua za maombi pasi kazi kutangazwa.....swali je? hizo barua huwa wanazifanyia kazi ua wanaturidhisha tu na kutupa matumaini tusikate tamaa kakutafuta kazi? kwa sababu sehemu zote tulizopeleka hazijakataliwa, zilipokelewa kwa ukarimu sana, na hakuna kati yetu aliyeitwa kwenye enterview hata mara moja.