Kuhusu Bangi..

Boflo

JF-Expert Member
Jan 20, 2010
4,390
1,225
marijuana.jpg

Nimewahi vuta Bangi mara moja....Kumbe haina madhara???
Tuvuteni bangi wana Jf

Kwako MziziMkavu umeona sasa hapo vifo vya sigara na alcohol.

========================
Bangi (pia: bhang, bhangi; kutoka Kihindi भांग, bhāṅg) ni maandalizi kutoka majani na maua (matumba) ya mmea wa kike wa Cannabis.

Ndani yake kuna dawa linalosababisha namna ya ulevi unaotegemea kiasi cha dawa linaloingia mwilini. Hutumiwa aidha kama kinywaji, kama kiungo ndani ya vyakula au huvutwa. Katika desturi asilia za Uhindi mavuno na maandalizi huja wakati wa maadhimisho ya Holi mwezini Machi na Vaisakhi mwezini Aprili, hivyo kuhusishwa na Bwana Shiva. Imekuwa sawa na Holi, mpaka kuvuta bangi wakati huo ni kitu cha kawaida.

Nta (wakati mwingine fuwele) hutenganishwa na majani na matumba ya Cannabis. Bangi inayochangamsha akili husaidia kueneza roho ya Holi, tamasha ambayo hailazimisha vikwazo vyovyote. Thandai,Pakoras na vadas,yote mapochopocho ya kitamaduni yenye bangi kama kiungo cha muhimu, huonjwa na kila mtu siku hiyo.

Bhang Ki Thandai(Kihindi) ni kinywaji maarufu katika maeneo mengi ya India ambacho hutengenezwa kwa kuchanganya bangi na Thandai, kinywaji baridi kitayarishwacho kwa karange,masala, maziwa na sukari. Matumizi ya bangi na vitu vya kuchangamsha akili kumekatazwa na baadhi ya madhehebu ya dini la kihindi kama vile Shikshapatri, na pia ni haramu katika Uislamu, ingawa si katika madhehebu yote.

Historia, Bangi mwanzoni ilitumika kama sehemu ya ibada ya Hindu nchini India kuzunguka mwaka wa 1000 KK na baadaye ikawa sehemu muhimu ya utamaduni wa Kihindi. Katika nakala ya zamani ya Atharvaveda, bangi inaelezewa kama mitishamba ya manufaa ambayo "humaliza wasiwasi". Maandalizi ya bangi yalikuwa takatifu kwa miungu, hasa Shiva. Moja wa sitiari za Shiva ni "Bwana wa Bangi" na inasemekana ni yeye aliyegundua tabia aali ya mchanganyiko.


Maandalizi
Katika kumuiga Shiva, wengi wa Wasadhu hutumia bangi kuongeza kutafakari na kufikia hali ya transcendental. Bangi au boza inajulikana pia ni maarufu miongoni mwa Wasufi kama msaada ecstasy kiroho.

Mila ya kutumia bangi wakati wa Holi ni wamba hasa Kaskazini mwa India ambapo Holi yenyewe huadhimishwa kwa pupa huku haijulikani mahali kwengine. Walakini bangi hutumiwa sana kule Varanasi au Chembada, nchi ya Shiva, ambapo bangi hutayarishiwa kwenye ngazi zake maarufu Popote kwenye ngazi, mtu anaweza kupata idadi kubwa ya wanaume wanaohusika katika mchakato wa kuandaa bangi.

Kutumia kinu na mchi, matumba na majani ya Cannabis husagwa na kuwa uji mzito wa kijani. Kwa mchanganyiko huu maziwa, siagi, na masala huongezwa. Wigo la bangi sasa ni tayari kufanywa kinywaji kinacho lewesha, Thandai, mbadala kwa pombe. Bangi pia huchanganywa na siagi na sukari kufanya uji wa kijani, na pia vipira vidogo vya kutafuna vinavyo washa, viitavyo 'golees' (ambayo kwa mantiki hii inamaanisha peremende au kidonge katika Kihindi).

Utamaduni.
Kwa vile ni ya kale, bangi imekuwa ni sehemu muhimu ya utamaduni wa India hata imekuwa kiashirio cha mambo mengi. Bangi huhusishwa na Bwana Shiva, kwani mmea wa Hampa hujulikana kama mtakatifu kwa Wahindu wa Kaskazini mwa India. Kuna hata imani kwamba kukutana na mtu liyebeba bangi ni ishara mbaya ya kufanikiwa. Na, kama hamu ya mmea wa hampa kunaashiria furaha, kuuona katika ndoto kunahakikisha mafanikio kwa mtu katika siku zijazo. Pia, kutembea juu ya jani takatifu la bangi hua minika kuashiria mabaya.

Watu wanaamini katika mali ya dawa ya mmea wa Hampa. Ikitumiwa kwa kiwango sahihi, inaaminika bangi kutibu homa, kuhara na sunstroke, kutoa kikohozi, kuharakisha kusagwa kwa chakula tumboni, hamu ya chakula, kutibu kasoro za kuongea na utata, kufanya mwili kuelewa yanayoendelea. [3] Wenyeji pia hudai kwamba bangi hutoa Kuwakwa Mchomo kwenye shingo ya nyuma.

Baadhi michoro ya mapenzi kutoka era ya Mughal ya India huonyesha wanandoa wakifanya ngono huku wakivuta bangi kuongeza mapenzi. Nchini Nepal, siku ya tamasha ya Wahindu ya Matta Shivaratri, bangi hutumiwa katika aina mbalimbali kama moshi, kuchanganywwa na pipi au kinywaji. Kutoa sadaka ya bangi kwa Bwana Shiva ni kawaida wakati wa tamasha hii.

Kalasinga Wanihang kutoka jadi wanapenda bangi sana, ambayo wanaiita Sukkha Prasad yaani "Apatianaye amani ". Katika Kisanskriti neno "Sukhi" humaanisha furaha na, "Prasad" ni sadaka kwa mungu ambayo ameionja na kuamua kugawana na kerende. Ilikuwa ikitumiwa kutuliza maumivu kabla na baada ya vita kwa vile wengi wa WaNihang wakirudi wangekuwa na majeraha makubwa. Kalasinga hufunzwa kuitumia kama dawa badala ya burudani.
 

Father of All

JF-Expert Member
Feb 26, 2012
3,089
1,225
Mwanangu Boflo inaonekana wewe na bangi bangi na wewe ni kitu moja! Hebu muangalie kaka yako Mutabaruka kwenye link hii .
 
Last edited by a moderator:

Blaine

JF-Expert Member
Jan 11, 2012
2,280
0
Boflo, that's why some states zimelegalize, watu wamefanya homework na kuthibitisha it's benign.
 
Last edited by a moderator:

MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
40,480
2,000
Mkuu Boflo Boflo boflo Boflo Boflo boflo Unaniharibia jukwaa langu ninalolipenda JF Doctor Rudi kwenye jukwaa lako la Jamii Photos Unakipaka una haribu jukwaa langu nitakulamba BAN unahalalisha vilivyo haramishwa ahhhBoflo boflo hufai hata kidogo.

Msitu wa Mlima Kenya una ufahari wa kuwa chanzo muhimu cha maji humu nchini, vilevile una sifa ya aibu ya utoaji wa bidhaa iliyopigwa marufuku ...ukuzaji wa bangi. Msitu huu unafaa sana kwa kila hali kuhusiana na ukuzaji wa bangi. Na ingawa polisi wanadai kwamba wamedhibiti upandaji wa bangi katika msitu huu bado wanakabiliwa na changamoto ya kuizuia biashara hiyo haramu.
 
Last edited by a moderator:

MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
40,480
2,000

Polisi walinasa bangi inayokhisiwa kugahrimu shillingi millioni moja katika nyumba moja kwenye mtaa wa Kitengela jana usiku

https://www.jamiiforums.com/jamii-photos/322281-madhara-ya-bangi.html

Madhara ya bangi yanaongezeka


AADA ya kuwepo kwa baadhi ya tafiti zilizokuwa zikiruhusu uvutaji wa bangi kwa madai kwamba ilisaidia wagonjwa waliosumbuliwa na msongo wa mawazo, hali hiyo imesababisha baadhi ya nchi kuruhusu matumizi yake.
Pamoja na mawazo ya wengi kufikiria kuwa kutokana na nchi ya Jamaica ndiyo ilikuwa mstari wa mbele kwa watumiaji wengi

ingekuwa ya kwanza kuruhusu bangi, lakini ukweli ni kwamba nchi ya Canada ndiyo ilikuwa ya kwanza kukubali bangi kutumiwa kama dawa ya maradhi.

Baada ya utafiti huo wa awali hivi karibuni watafiti wengine wamegundua kuwa matumizi ya bangi kwa muda mrefu yanasababisha kujiongezea madhara badala ya kutibu kama ilivyokuwa ikisemekana hapo awali.
Watafiti hao wamekwenda kinyume na wale wa kwanza kwa kusema kuwa matumizi yake yana uwezekano mkubwa wa kumletea mtumiaji magonjwa ya kupungua uzito mara kwa mara, magonjwa ya figo, ini na ugonjwa wa akili.

Watafiti waliogundua athari hizo ni wale wanaotokea nchini Australia ambao katika utafiti wao wamegundua kuwa zaidi ya vijana 3,100 walio katika umri wa miaka 20 ndio wamekuwa watumiaji wakubwa wa bangi.
Utafiti wao umekwenda mbali na kubaini kwamba asilimia 18 ya vijana hao ni wale waliojiingiza katika matumizi ya dawa hizo za kulevya kwa muda wa miaka miwili au mitatu.

Asilimia nyingine 16 ya vijana wa umri huo wamebainika kutumia kwa muda wa kati ya miaka minne hadi mitano.
65 kati ya watumiaji wamegundulika wameshaathirika na maradhi ya ugonjwa wa akili.
Wakati hao wakisumbuliwa na tatizo hilo wengine 233 wamebainika kuathirika kwa figo na ini.

Watafiti wamebaini vijana wengine kati yao wanasumbuliwa na tatizo la kupata uchizi (wehu).

Baada ya kubaini hayo watafiti wametoa ushauri kwa vijana kutotumia dawa hizo za kulevya kwa vijana kwa zaidi ya miaka sita au zaidi tangu pale siku ya kwanza alipoanza kutumia.

Wanasema kuwa kwa wale ambao sasa wamevuta kwa muda mrefu kati ya miaka 15 na zaidi wengi wao wamekumbwa na tatizo la kiakili.

Kwa mujibu wa Dk. John McGrath, wa kituo cha uchunguzi wa afya ya wagonjwa wenye mtindio wa ubongo cha Queensland, nchini Marekani, anasema: “Wengi wa wagonjwa ambao wamekumbwa na matatizo hayo tumegundua ni wale waliowahi kutumia bangi kwa muda mrefu na hatimaye kujikuta wakipata tatizo la akili.”

Daktari huyo anasema kuwa ni nadra sana kukutana na wagonjwa wa akili vijana halafu wakawa hawajawahi kutumia bangi, iwe mwaka mmoja au zaidi.

Anasema kuwa iwapo matumizi ya bangi yatakomeshwa tatizo la vijana kupata matatizo ya utaahira yatapungua kwa kiasi kikubwa duniani.
Bangi ni nini, inatumiwaje?

Kwa hapa nchini na baadhi ya nchi, bangi imetambulika kama dawa ya kulevya ambayo imekuwa na majina mengi kutokana na kutumiwa na kundi la vijana zaidi kuliko watu wazima.

Bangi imekuwa ikijulikana kwa majina mengi ikiwamo, dawa, ganja, hashish, kijiti, marijuana, kaya blunt na mengineyo, ilimradi kutegemeana na sehemu inapotoka.

Watumiaji wengi wamekuwa wakiitumia kwa kuvuta kama sigara au wengine hutumia kwenye kiko kwa kuvuta.
Bangi ni bidhaa iliyochanganyika na kemikali hatari ambazo ni sumu na huathiri afya.

Wapo baadhi ya watumiaji wa bangi ambao wamekuwa wakiitumia kwa kuiweka katika maji wakiifanya kama majani ya chai na wengine huchanganya kwenye chakula.

Bangi inaathiri vipi ubongo?
Wanasayansi wamebaini kuwa matatizo makubwa yanaanza kupatikana kutokana na bangi kuingia kwenye ubongo wa mtumiaji na huathiri mfumo mzima wa akili.

Tatizo kubwa linalomkumba mvuta bangi ni kunyemelewa na magonjwa ya ugonjwa wa shinikizo la damu (BP), kupoteza kumbukumbu, mawazo, anaridhika hata kama ana matatizo.

Pia mtumiaji wa kila siku anakuwa akikumbwa na mabadiliko ya mara kwa mara katika ubongo wake.
Imebainika kuwa bangi inachangia kuongeza mapigo ya moyo kutoka asilimia 20 hadi 100, muda mfupi tu wa saa tatu baada ya kuvuta.

Bangi huaribu mapafu, kwani ina zaidi ya asilimia 50–70 ya kemikali aina ya carcinogenic hydrocarbons kuliko mvutaji wa tumbaku.

Mtumiaji wa bangi hupumua kwa tabu sana kuliko yule anayevuta tumbaku ingawa wote wanaharibu mapafu, pamoja na kuwa na uwezekano mkubwa wa kukaribisha ugonjwa wa kansa.

Imebainika kuwa watu wanaovuta bangi wamekuwa wakisumbuliwa zaidi na matatizo mengi ya kiafya.
Watafiti wamegundua kuwa wavutaji wengi wa bangi wamekuwa hawana mahusiano mema na watu walionao karibu kwani wamekuwa chanzo cha matatizo kutokana na wao kuona kila wanachofanya ndiyo sahihi na cha wenzao si sahihi.

Chanzo:
http://www.freemedia.co.tz/daima/habari.php?id=13857

 
Last edited by a moderator:

MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
40,480
2,000
MARIJUANA SIDE EFFECTS & SAFETY

The cannabinoid, dronabinol, which is found in marijuana, is LIKELY SAFE when taken by mouth appropriately as a prescription medication. Dronabinol (Marinol) is an FDA-approved prescription product.

Marijuana is
POSSIBLY UNSAFE when it is taken by mouth or smoked. It is classified as an illegal substance.

Use of marijuana can cause dry mouth, nausea, vomiting, dry or red eyes, heart and blood pressure problems, lung problems, impaired mental functioning, headache, dizziness, numbness, panic reactions, hallucinations, flashbacks, depression, and sexual problems.
Special Precautions & Warnings:

Pregnancy and breast-feeding: Marijuana is UNSAFE when taken by mouth or smoked during pregnancy. Marijuana passes through the placenta and can slow the growth of the fetus. Marijuana use during pregnancy is also associated with childhood leukemia. Using marijuana, either by mouth or by inhalation is LIKELY UNSAFE during breast-feeding. The dronabinol (THC) in marijuana passes into breast milk.

Heart disease: Marijuana might cause rapid heartbeat and short-term high blood pressure.

A weakened immune system: Cannabinoids in marijuana can weaken the immune system, which might make it more difficult for the body to fight infections.

Lung diseases: Long-term use of marijuana can make lung problems worse. Regular, long-term marijuana use has been associated with several cases of an unusual type of emphysema, a lung disease.

Seizure disorders: Marijuana might make seizure disorders worse in some people; in other people it might help to control seizures.

Surgery:
Marijuana affects the central nervous system. It might slow the central nervous system too much when combined with
anesthesia and other medications during and after surgery. Stop using marijuana at least 2 weeks before a scheduled surgery

Source: .
http://www.webmd.com/vitamins-supplements/ingredientmono-947-MARIJUANA.aspx?activeIngredientId=947&activeIngredientName=MARIJUANA
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom