Kuhusu Ajira za ICT (Practicals)

Kuhusu Ajira za ICT (Practicals)

Born_T0WN

Member
Joined
Oct 21, 2016
Posts
15
Reaction score
42
Kuna jambo linanisumbua kichwa siku nyingi naomba niwashirikishe wadau wenzangu.. Mchakato wa Ajira za Utumishi kwa hivi karibuni umerahisishwa upande wa Written interviews kwa maana ya Kwamba wasailiwa hawana ulazima wa kusafiri kwenda Dar es Salaam kufanya mtihani wa mchujo, badala yake mitihani hiyo inafanyika katika mikoa husika wanakoishi wasailiwa.
Shida bado ipo upande wa ICT, practicals zote zinafanyika Dar, chuo cha T.I.A hali inayopelekea baadhi ya wasailiwa kushindwa kufika kwenye usaili huo licha ya kuwa wamefaulu vizuri kwenye mchujo
OMBI LANGU kwa mamlaka zinazohusika.. practicals za ICT ziwekwe angalau kwenye kanda tatu ambazo ni kanda ya KUSINI, KATI na KASKAZINI ili kupunguza gharama wanazoingia wasailiwa wa mikoani kwenda Dar... kwa mfano mtu akitoka Mbeya kwenda Dar anahitaji si chini ya laki mbili na nusu ili aweze kukaa Dar kwa siku mbili.
Naamini mawazo yangu yatafika kwa wahusika na wataliangalia hili.. Asanteni.
 
Back
Top Bottom