Kuhujumiwa kwa ITV katika king'amuzi cha STAR TIMES Dar

Huu n uchonganishi na umbea mambo ya kieletronics unasema kuhujumiwa , kwani wao Itv wametoa taarfa ya kuhujumiwa au ndio unataka kuichonganisha serikali na vyombo vya habari

Maskini ITV!
 
Ipo siku Chama Cha Mashetani kitailipua ITV kama alivyolipuliwa Daudi Mwangosi
 
Mtampigia kelele mengi na mwisho mtaonekana majuha. Kodi kama anakwepa angenaswa tu maana TRA hawachezi mbali na wafanya biashara wakubwa ingawa wanawashupalia waziwazi wauza vitumbua. Naye Mengi hawezi kuwa mjinga akakwepa kodi waziwazi kwa sababu anajua madhara atakayokumbana nayo kwa kufanya hivyo. Ni kweli mimi sasa siangalii tena hata Isidingo kwa sababu kila inapofika jioni EATV na ITV ni mikoromo tu kenda mbele. Sijui kama wanalielewa maana sijawahiwauliza. Startime huenda wana matatizo na vyombo vyao na hawajajua wafanye nini. Tuwashauri tu warekebishe tofauti zao na pesa tunayolipa Startime bila kupata tunachonunua ni WIZI MTUPU NA HUJUMA KWA UCHUMI WETU.
 
kitokana na kutoonekana vizuri kwa ITV katika kingamuzi cha STAR TIMES wakati wa taarifa ya habari katika maeneo mbalimbali nchini hususani mkoa wa DSM inasekana kuna taarifa za kukihujumu kituo hicho kikongwe nchini.Baadhi ya vingamuzi kama vile CONTINENTAL,DSTV,AZAM TV,EASY TV,wakati wa taarifa ya habari ITV inaonekana vizuri sana lakini kwa star times inakatika katika hovyo hadi watazamaji wa ITV wanashindwa kutazama taarifa za habari vizuri.mwandishi alipokwenda katika ofisi za sta times walimpoga chenga kwamba hawako tayari kuzungumzia hilo jambo,kama vile haitoshi mwandishi akamlazim kwenda katika mamlaka ya mawasiliano nchini TCRA prof. Mkoma alijibu ana wageni anawasubili.Hivyo katika kingamzi cha star times ITV inahujumiwa.

Dawa ni kuachana na star time
 
Iko maneno hapo chezea chaga wewe. Hapa kuna kampeni ya kuua Azam Product na star times. Mengi mara nyingi hawezi ushindani wa biashara hutumia mbinu mbalimbali kama vitisho vya kuuliwa,uzalendo nk. Sasa hii Jf haikosekani kuna wachaga humu kwa network yao inafanya kazi. Mimi nilikuwa sipati vizuri chanel 10 na Tbc kama ilivyo sasa kwa Itv mbona hamkulalamika Tbc na Chanel 10 vinahujumiwa? Hameni tu Star times sasa hivi tunaona steshen zaidi ya saba kwa Tsh 4800/=,kwanza hiyo Itv imekuwa na siasa egemezi za upande mmoja na kuwakandamiza wasiokubaliana na boss wao,kwa wale wapenda siasa hameni tunaopenda burdan ya tv kama movie,music,sports na education hatuna lazima ya Itv
Kwajinsi nilivyo pata shida ninarudisha kingamuzi cha star times leo watafute mtu wa kumpa bure!
 
Attachments

  • 1422897100419.jpg
    1422897100419.jpg
    49.3 KB · Views: 113
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA
ISO 9001: 2008 CERTIFIED

TAARIFA KWA UMMA

KUHUSU MUINGILIANO WA MASAFA YA EATV NA ITV KUPITIA KING’AMUZI CHA KAMPUNI YA STAR MEDIA KATIKA KITUO CHA KUSAMBAZA MATANGAZO MAKONGO JUU

A. UTANGULIZI
1. Masafa ni rasilimali muhimu katika shughuli za Mawasiliano (simu, wavuti, redio, na utangazaji). Masafa ya Mawasiliano (Spectrum) hugawanywa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) (ikitambuliwa hapa kama Mamlaka) kwa kutoa leseni kwa watoa huduma za mawasiliano nchini kwa mujibu wa sheria na masharti ya leseni. Moja ya kazi za Mamlaka ni pamoja na kupokea na kusuluhisha matatizo ya muingiliano wa masafa kati ya watoa huduma mbalimbali wa mawasiliano kwa kutumia ujuzi na wataalamu na teknolojia ya mitambo maalumu na mahususi ya kisayansi kufanya kazi hiyo. Kazi hizi zimeainishwa katika Sheria ya Mamlaka ya Mawasiliano ya 2003 (TCRA Act of 2003) na Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (Electronic and Postal Communications Act (EPOCA) ya mwaka 2010.
2. Mnamo tarehe 29 Januari 2015, Mamlaka ilipokea malalamiko kuhusu ubora wa matangazo ya vituo vya ITV na EATV yanayorushwa na Kampuni ya Star Media (T) Limited ambaye ni msambaza matangazo ya dijitali. ITV na EATV wana leseni ya Maudhui (Content Service Lisence) na Star Media wana leseni ya Miundombinu ya Utangazaji (Network Facility License as a signal distributor) kutoka TCRA. Leseni zote za Mamlaka zina masharti ya kuzingatia.
3. Huduma za Mawasiliano hutumia bendi ya masafa tofauti (Spectrum bands). Huduma za mawasiliano ya setilaiti (satellite) hutumia bendi 3.4 mpaka 4.2 GHz, inayofahamika kama C-Band. Ifahamike kuwa masafa ya setilaiti ya kupokea matangazo (satellite downlink frequency) ya 3.644 GHz yanatumika kupokea matangazo kutoka satelaiti ya Intelsat 906 (TP 10) kwa matangazo ya vituo vya utangazaji nchini kupitia mfumo wa dijitali ambao mitambo yake iko katika kilima cha Makongo Juu area. Hata hivyo, sehemu nyingi duniani, ikiwemo Tanzania, hutumia teknolojia ya WiMAX katika bendi 3.5 GHz. Masafa haya yanafahamika duniani kote kwa uwezo wake wa kutumika kiteknolojia kati ya mfumo wa “Fixed Satellite Services (FSS)” na IMT kama vile mwendo kazi wa intaneti bila waya (Broadband Wireless Access (BWA) transmission) ikiwemopia teknolojia ya WiMAX.
4. Kufuatia malalamiko yaliyopokelewa na Mamlaka, TCRA iliteua timu ya wataalamu Wahandisi wa Masafa kufanya uchunguzi ili kubaini tatizo la muingiliano wa masafa yaliyosababisha ITV na EATV kutokuonekana vizuri katika king’amuzi cha Star Media, kwa kutumia utaratibu na jinsi sheria zinavyoelekeza. Timu hiyo ya wataalamu wa masafa iliwasiliana na Star Media na kutembelea eneo la Makongo Juu kwenye mitambo yao ili kubaini aina ya muingiliano, muda wa muingiliano na maeneo husika. Timu hiyo ilifanya uchunguzi kwa kutumia vifaa maalumu kwenye eneo lenye mitambo ya kurusha matangazo ili kubaini muingiliano wa masafa kupitia watoa huduma wa intarneti za mwendo kasi kupitia teknolojia ya WiMAX katika bendi 3.4 – 3.6 GHz. Aidha timu ilifanya tathmini ya vipimo vya matumizi ya masafa na watoa huduma katika bendi nzima ya C- ya kupokelea matangazo (downlink frequency) kutoka 3.4 GHz hadi 4.2 GHz.

B. MATOKEO YA UCHUNGUZI NA YALIYOJITOKEZA

5. Baada ya uchunguzi huo wa kitaalamu kwa kutumia vifaa maalumu vya teknolojia ya sayansi ya masafa, timu ya wataalamu walibaini kuwa muingiliano wa masafa ulikuwa unatokea kati ya saa 12 jioni hadi saa 6 usiku. Uchunguzi katika eneo la urushaji wa matangazo na mitambo ya Star Media ulibaini kuwa muingiliano ulikuwa katika mfumo wake wa kupokea matangazo (satellite receiver station) iliyoko kwenye eneo (S 06◦ 45’ 736 E 39◦ 12’ 632). Mfumo wa kupokea (Low Noise Block down converter - LNB) kutoka bendi 3.4 GHz to 4.2 GHz. Matokeo ya uchunguzi wa masafa ya bendi 3.644 GHz hayakuonesha aina yeyote ya muingiliano. Aidha masafa ya 3.4 GHz hadi 3.6 GHz yalionesha matumizi mbalimbali kutoka masafa ya bendi 3.5 GHz ambayo yanatumika na watoa huduma wanaotumia teknolojia ya WiMAX.

6. Kutokana na matokeo ya uchunguzi kama ilivyoelezwa katika no 5, ilibainika wazi kuwa hakukuwa na muingiliano katika bendi hiyo (In-band interference) kutoka katika mfumo wa matumizi ya inteneti ya mwendo kasi kwani masafa yote katika mifumo yote ya utoaji huduma haikuonesha muingiliano. Vile vile ilithibitika wazi kuwa hakukuwa na muingiliano katika mfumo huo (out-of-band emissions) Mfumo wa huduma wa mwendo kasi wa inteneti unaotumia masafa ya bendi 3.5 GHz huweza kusababisha muingiliano kwa mtoa huduma anayetumia bendi 3.6 – 4.2 GHz (FSS stations).

7. Matokeo ya vipimo vilionesha kuwa eneo la Makongo Juu hupokea mawimbi ya Mawasiliano kutoka kwa watoa huduma wote wanaotumia masafa ya 3.5 GHz kutoka meneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam kutokana na eneo la Makongo kuwa juu. Hali hii inaweza kusababisha mawimbi ya mwendo kasi wa intaneti katika masafa 3.5 GHz kuibebesha mzigo mkubwa mtambo wa kupokea matangazo ya utangazaji (FSS stations) anayetumia bendi 3.4 – 4.2 GHz kama hakuna wigo wa kuzuia muingiliano kiteknolojia (band pass filter) au mfumo bendi mwembamba (narrow band LNBs).

C. KUTATULIWA KWA MUINGILIANO WA MASAFA

8. Kutokana na vielelezo vya matokeo ya uchunguzi uliofanywa na wataalamu wa masafa kwa kutumia vifaa maalumu, Mamlaka ilitoa maelekezo kwa Star Media ili kutatua tatizo la muingiliano uliokuwepo katika mtambo wake wa urushaji matangazo Makongo Juu. Kwanza, kutumia kifaa kiitwacho IF attenuator/filter katika mitambo yake ya kupokelea mawasiliano ya matangazo ya setilaiti (FSS receiving station); Kutumia LNB converter katika bendi ya masafa 3.7 – 4.2 GHz badala ya kutumia masafa ya (C-band) yote (3.4 – 4.2 GHz); hata hivyo, masafa 3.664 GHz yamehifadhiwa kama wigo unaozuia matumizi kati ya watumiaji wa matangazo ya mitambo iliyosimikwa juu ya ardhi (Terrestrial) - (3.4-3.6 GHz) na yale ya wanaotumia Satelaiti ya kupokelea matangazo (3.7-4.2 GHz). Pili, Mamlaka ingeagiza watoaji wa inteneti ya mwendo kasi katika mitambo yao (BWA) kuwa na nafasi ya kutosha kati ya mitambo ya “FSS” na kufuata utaratibu uliowekwa kulingana na matumizi ya masafa, ikizingatiwa kwamba mawimbi yaliyo mengi katika eneo la Makongo Juu hupokelewa kutoka sehemu mbalimbali kutoka Jiji la Dar es salaam. Tatu, njia mbadala zitumike katika kupokea matangazo ya utangazaji katika kilima cha Makongo Juu kama vile teknolojia ya Mkongo wa Mawasiliano (fiber optic) satelaiti kutumia mfumo wa bendi ya Ku-Satellite band, au “microwave links”.

9. Baada ya Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) kufanya uchunguzi wa kitaalamu kwa kutumia vifaa maalumu vya sayansi na teknolojia mahususi kwa matatizo ya muingiliano wa masafa, imebainika pasina shaka kuwa hakukuwa na hujuma yeyote kutoka kwa Kampuni ya Star Media au kufanya kwa makusudi kwa nia ya kuharibu muonekana wa vituo husika vya ITV na EATV katika ving’amuzi vyake. Tatizo lilikuwa ni la kisayansi na kiteknolojia ambalo hutokea mara nyingi katika huduma za Mawasiliano kote duniani, na tatizo hilo limemalizika kwa kutumia njia za kisayansi na kiteknolojia kwa watoa huduma wote kwa kushirikiana na Mamlaka..

10. Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) inapenda kutumia fursa hii kuwakumbusha watoa huduma wote wenye leseni za Mamlaka kuwa inapotokea matatizo au malalamiko, basi wafuate taratibu zilizowekwa kwa mujibu wa sheria na masharti ya leseni pamoja na kanuni zake ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa kwa TCRA na kutoa ushirikiano katika kutatua tatizo husika kupitia sayansi na teknolojia ambayo hutumika katika kutoa huduma za mawasiliano.

Kwa taarifa zaidi tafadhali wasiliana nasi kupitia dg@tcra.go.tz

Mkurugenzi Mkuu

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)

5th February 2015
4
 
Acheni uongo Sisi sio wajinga mtatataja kika kitu lakini mjue tunaelewa kilichonyuma ya kukatika mawasiliano. Hata ambaye hana elimu ya mawasiliano ataona nyie wahuni tu. Hivi nikuulize swali dogo tu hiyo frequency interference inatokea tu wakati wa taarifa ya habari? Ama kipindi cha Hotmix cha EATV? hebu kuweni watu wazima sio mnakuja na Porojo za kitoto. Mtaumbuka sana mwaka huu si mnatumika kujibu kishamba!
 
Jamani kama ni hujuma basi na continental nao wanatuhujumu
Tena startime yupo juu ila continental ni kama sanamu tu.
Maana sipati matangazo tk nimekinunua ni no signal, TCRA tusaidieni nahisi havina ubora kabisa kama walivinunua kwenye dampo
 
Hakuna uongo wowote hapa. Hakuna siasa katika masuala ya teknolojia. Kama umeisoma report imesema wazi kuwa muingiliano ulikuwa unatokea saa 12 jioni hadi saa sita usiku. Baada ya maagizo ya TCRA kufuatia uchunguzi muingiliano haupo tena.
 
Back
Top Bottom