Kuhudumia Mwanaume Kabla ya Kuoana.

Ni kama vile wanatufanyia Interview! hapo hujanipata. Hayo nitafanya ukinivisha pete wangu. kama inakushindaa
kwaheri
Pete mbona zimejaa kwa masonara, kama huo ndio msimamo wako jifikirie mara mbili, ni afadhali mtu asiepropose ndoa kuliko msanii anaekuingilia kwa gia ya kukuoa.
Utavimba bichwa kwa kuvalishwa pete kumbe kuna wenzako 6 nao wameshavalishwa pete, jamaa atajilia mzigo kwa ulaini akitosheka anakuachia manyoya. wake up usiwe mjinga.
 
sio kwamba wamama wana matatizo sema la life cycle inachangia mama kushindwa kumudu majukumu ya nyumbani mfano mama unatakiwa kazini saa moja na nusu na upo dar inamaana unatakiwa uondoke home saa kumi na moja na kurudi umewai sana saa 2 sasa hapo majukumu yanaenda kwa housgirl ndo maana mimi sidhani kama mwanaume ananioa ili nimfanyie kazi za nyumbani na siwezi kuishi na mwanaume eti nimsaidie kazi za home atafute mtumishi.mimi nikiishi nae ni mambo mengine maana automatically kama lengo lake ni kumfanyia kazi za nyumbani,naeza kushindwa kuzifanya sio kwamba sipendi ila ni kutokana na situation tu ya maisha

Ni kweli hakuoi ili umfanyie kazi, lakini katika ndoa kuna "obligations and responsibilities" kwa kila mwanandoa (wote mume na mke). Kimsingi bila kujali umechoka au haujachoka unapaswa umwandalie (au umpikie) mumeo chakula, na sio kipikwe na house girl. Tatizo jingine kwa visingizio hivyo, majukumu yote ya familia anaachiwa h/g (Atafua nguo zoote za mumeo, za kwako, mpaka na chupi za mumeo, atakutandikieni kitanda) n.k. Matokeo yake anamalizia kabisaa na "shughuli ile yenyewe yenye utamu", alafu utamlalamikia nani.

Ladies, you ought not to avoid your responsibilities and obligations, employment should not be an excuse. Afadhali kwa wamama wenye watoto wachanga, tutasema wanahitaji usaidizi, lakini wengine wako wawili tu, na bado h/g ndo kila kitu. Mnaziangamiza ndoa zenu kwa kutokujua.
 
Halafu kama wewe kwa kuangallia tu picha yako tayari nimesha-kudisqualify hata nafasi ya interview ya kuwa hose wife sikupi... Labda Ceremonial wife pia kwenye 6*6 nakupa 100% .... Jikoni najua 0%, Jeans najua hufui 0% .....kunyoosha najua ni dobi ... mh! labda niwe fisadi ....

Ha ha haaa haaa haaa!!! yaani ungejua tu. usingesema yote hayo. Muulize dadaangu Ashdii. ananijua Vizuri.
 
Pete mbona zimejaa kwa masonara, kama huo ndio msimamo wako jifikirie mara mbili, ni afadhali mtu asiepropose ndoa kuliko msanii anaekuingilia kwa gia ya kukuoa.
Utavimba bichwa kwa kuvalishwa pete kumbe kuna wenzako 6 nao wameshavalishwa pete, jamaa atajilia mzigo kwa ulaini akitosheka anakuachia manyoya. wake up usiwe mjinga.

Naamanisha ile pete kubwa Dadiito.
 
Nilidhani tunazungumzia mahusiano ya kabla ya ndoa....ambayo kimsingi yanakuwa na imbalances (mpini/makali) za kila namna. Pale mwanzo ndio maana nikasema kuna 'nipe, nikupe' (compromises) nyingi tu katika kujaribu kutengeneza mahusiano ambayo baadae yanaweza kwenda kwenye hatua ya ndoa.

Binafsi kabla sijaoa, nimepita kwenye similar situation lakini ilikuwa ni kwa ridhaa ya binti mwenyewe bila kumshurutisha na hata mimi kuna mambo nilikuwa namfanyia bila kushurutishwa ambayo hayakuwa majukumu yangu from a strict point of view.
Yaani mkuu unakwenda na mstari na hata sina haja ya kukuuliza umri maana najuwa wewe ni wamakamo yangu, sio wa level ya usharobaro, maana kuna wakati demu anaweza akakugeuza wewe ndio dingi mapenzi kidogo mizinga mingi.
 
  • Thanks
Reactions: SMU
<span style="font-family: comic sans ms">Ndio maana ndoa nyingi zitaendelea kuvunjika... Haya ni majukumu ya msingi kwa mwanamke yeyote na hata kama wote tumeajiriwa Houseboy/girl anasuppliment tu na iko siku nitataka wewe unipikie na pia sio busara hao wengine wakanifulia nguo zangu katika mazingira ya kawaida. Hapa ndipo maendeleo na uzungu unapotumislead!! I stand to be criticised!</span>
<br />
<br />
Wala hujakosea. Wengi wanafikiri houseboy au house gal ni kila kitu. Ila ukweli ni kuwa tunataka tujue huyu mke atakuwaje nikiwa nae baada ya ndoa nionje mapishi yake, nijue kama hata anajua kupika maana wengi siku hizi hata kukatakata kitunguu hajui, nimuone fua yake au ni wale wanaoloweka nguo wiki, nijue reaction yake siku nimerudi namwambia wazi ile hela ya salon uliyoomba sijapata nione anakuwaje. Nione maisha yakibadilika anareact vipi kutokana na mabadiliko
 
ndo nyingi siku hizi hazina tofauti na sela za ccm, nzuri mwanzoni tu lakini mbeleni wote ni wapita njia
 
Mi napita tu hapa wajameni, ila kama kuna mdada atataka kuhamia kwangu akaribie tu niko free, aje tutambuane
 
Ni tatizo sana nowdayz, hasa kwenye issue ya zaa kwanza ndo tuoane?! sasa huwezi pata mtt ww si mke? ndoa nyingi wanawake vitumbo mbele, kama hawajishikishi ili waolewe basi ni condition aliyopewa na mkaka, kufua poa tu as huwezi kwenda kwa mshikaji mkalalia mashuka machafu, or mkapitia chipsi unapika kidogo. Ila kuhamia kwa mkaka bila ndoa wont advice.
 
Mi napita tu hapa wajameni, ila kama kuna mdada atataka kuhamia kwangu akaribie tu niko free, aje tutambuane

Karibu kwangu si unajua working class women we have every thing except husband material
 
Ni tatizo sana nowdayz, hasa kwenye issue ya zaa kwanza ndo tuoane?! sasa huwezi pata mtt ww si mke? ndoa nyingi wanawake vitumbo mbele, kama hawajishikishi ili waolewe basi ni condition aliyopewa na mkaka, kufua poa tu as huwezi kwenda kwa mshikaji mkalalia mashuka machafu, or mkapitia chipsi unapika kidogo. Ila kuhamia kwa mkaka bila ndoa wont advice.

Swala la kuzaa kwanza eti ndio ujue kuwa mwanamke ana uwezo wa kuzaa nafikiri si la kisayansi kwani yawezekana pia mwanaume akawa ndo chanzo.... na wala silifagilii kwani haileti picha nzuri kwenye jamii.
 
Yaani mkuu unakwenda na mstari na hata sina haja ya kukuuliza umri maana najuwa wewe ni wamakamo yangu, sio wa level ya usharobaro, maana kuna wakati demu anaweza akakugeuza wewe ndio dingi mapenzi kidogo mizinga mingi.

Nachoshindwa kushangaa ni kwamba wanawake wengi wanaojaribu kukwepa huu ukweli wa majukumu ya mwanamke anapokuwa kwa mume wake hawajaolewa, na sitoshangaa kama hawataolewa kwa kutafuta usawa.

Utashangaa huu usawa unakujaje wakati tangu uumbaji Mungu alishamkabidhi kila mmoja majukumu yake??
 
Mkirua we hujawahi kukutana na kimeo. Bora kutonunua mbuzi kwenye gunia nimuhakikishe kweli ni mbuzi ndo nijitose. Kama mimi ndo nina matatizo hayo mengine. Ila kama najihakikishia niko fit lazima mbuzi nimuone kwa macho
 
Nashindwa hata kuwapa advice gani vijana
wengine tushakua na wajukuu sasa miaka ileeeeeee tushafanya usafi kupika kudeki kufua kuweka mapambo ndani ya nyumba lakini ndani waliingia wengine .,.....kwa hiyo basi (.....)
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Mimi napinga kabisa mwanaume anayetoa masharti kama ya kupikiwa na kufuliwa ndio akuoe. Ila nakubali kabisa wife material lazima atafanya hivyo vitu bila kushurutishwa. Kwa hiyo kwa mtazamo wangu mwanaume anayetoa masharti sijuhi upike, ufue, upate mimba ndio nakuoa si husband material. Na mwanamke asiyefanya hizo kazi pale anapomtembelea mpenzi wake gheto si wife material.

Unajua hata kama sisi wanawake wa kileo tuko busy na kazi na mafoleni bado kuna tofauti kati ya nyumba ya mwanamke asiyejua kazi za ndani na mwanamke anayezijua ila hana nafasi. Kumbuka kuwa mahousegirl wengi si profesional kwa kazi za ndani wanahitaji kufundishwa maana wametoka bush kwa mfano most of them hawajawahi hata kutumia vyoo vya ndani wala kuvisafisha. Sasa kama mama mwenye nyumba hajuhi kupika jua fika hata housegilr hataweza pika chakula kizuri; nani atamfundisha??? Kama mama hajuhi kufua wala usafi wa ndani jua nyumba itakuwa chafu hata kama mna housegirl watatu kwani mkeo hatakuwa anaona kasoro.

Hata makazini supervisor mzuri ni anayejua kazi. Kwa hiyo hata kama hatufanyi kazi za ndani very often we are good supervisors because we know them. Mimi housegirl hakiacha kazi naona mme wangu anavyokuwa na furaha maana ananotice difference ndani katika kila nyanja. Bahati mbaya siwezi hacha kazi.

Nina shemeji yangu alikuwa na girlfriend wake wa muda mrefu saana mdada anakuja gheto kwa shem anampikia afu anaacha vyombo kibao kwenye sink anatimua mpaka nyumba inatoa harufu. Mwisho wa siku jamaa hakuoa japo am sorry kwani alikuja mzalisha dada wa watu. Ila washikaji wote walikuwa wanamwambia jamaa ukioa hapo umevaa mkenge.
 
Habari zenu. Nimekumbwa na utata juu ya suala hili, siku hizi wakaka wengi kabla ya ndoa wanataka wahudumiwe kama kwamba tayari wameoa. Tendo la ndoa, Kufua, Kupika, Usafi wiki end na hata katikati ya wiki na mambo mengine kama hayo. Je hiyo ni sawa kwa mila na desturi zetu?
wengine wanafika mbali zaidi wanataka mtoto kwanza ndipo ndoa ije.
Sasa kweli huo ndio upendo? Naomba Mnieleweshe labda mie wa kizamani mno.

Wivu wenu tu ndo unawaletea shida! unaona ukikaa mwezi bila kumuona mwenzio basi atahamishia majeshi sehemu nyingine.Usipompa huduma atapewa na mwingine! basi ukifikiria hivyo unaamia geto kabisa...Na ukichukulia siku hizi wadada wakimaliza vyuo hawarudi kwenye familia zao,eti nao wanapanga vyumba km akina kaka.Utakuta kwenye chumba chake analala mara 1 kwa wiki.
 
Sina tatizo na kukufulia na kukupikia 365 days a year, tatizo linakuja kuwa sote tumekuwa waajiriwa, katika maisha ya leo. Kwa hiyo wote tunaingia nyumbani kuanzia saa moja na nusu jioni (tulio na bahati mbaya ya kukaa maeneo ya pembezoni mwa mji). Naamini kwa muda huu kuingia jikoni na kuanza kujipikilisha, na uchovu wa kazini (ambao nina hakika na wewe mwenzangu unao) tutalazimika kumuajiri msaidizi. Kwa hiyo sidhani kama ni uzungu ndugu yangu, bali ni suala la sisi wenyewe kuwa considerate kwa wenza wetu. Kama niko tu nyumbani, naamini hayo hayawezi kushindikana.

Imagine tumeingia wote nyumbani, unadai chai, maji ya kuoga, chakula to name a few....jamani hata kumfikiria mwenzio kuwa naye alikuwa kazini, au kazi zako tu ndio zinachosha?

Tukirudi kwa wakaka wanaotaka huduma hizi kabla hata ya kuoa, nafikiri mara nyingi akina dada nao wanafanya hivyo kwa kujiona wako insecured na mostly on the loosing side. Kama alivyosema mdau mmoja, wewe ukigoma anakuja mwingine fasta na kufanya huduma zote hizo si ajabu na hela ya matumizi akaacha (haa haa..) Lakini the bottom line ni kuwa unaweza kuvunja mgongo kufua, kupika, usafi mpaka ukalima na bustani ya mboga nje, lakini mwisho wa siku inawezekana kabisa kuna mwingine pembeni ambaye hasumbuliwi kwa namna yoyote ile na anatengeneza kucha mwanzo mpaka mwisho wa wiki (hazigusi maji zaidi ya anayoogea), ambaye ndiyo akaolewa kwa shangwe zote! Na wewe 'employee of the year' ukabaki unasoma namba...tafakari na chukua hatua.

Dinna more than true! Kuna wakati naamini ndoa ni mpango wa Mungu hata uspofua, sijui kupika n.k kama wako will be urs. Wont forget my 4 years doing ever thing for man n we did nt end together. It was well learned lesson, waliofuata karibu kwangu uje na ulizovaa mwilini as ukiondoka utazivaa tena, never sleepover to bf unless hangover! B4 marriage only sex is for offer as U give I give hata vikiend siko we had fun na sikuwa maid wako!
 
Mimi napinga kabisa mwanaume anayetoa masharti kama ya kupikiwa na kufuliwa ndio akuoe. Ila nakubali kabisa wife material lazima atafanya hivyo vitu bila kushurutishwa. Kwa hiyo kwa mtazamo wangu mwanaume anayetoa masharti sijuhi upike, ufue, upate mimba ndio nakuoa si husband material. Na mwanamke anasiyefanya hizo kazi pale anapomtembelea mpenzi wake gheto si wife material.

Unajua hata kama sisi wanawake wa kileo tuko busy na kazi na mafoleni bado kuna tofauti kati ya nyumba ya mwanamke asiyejua kazi za ndani na mwanamke anayezijua ila hana nafasi. Kumbuka kuwa mahousegirl wengi si profesional kwa kazi za ndani wanahitaji kufundishwa maana wametoka bush kwa mfano most of them hawajawahi hata kutumia vyoo vya ndani wala kuvisafisha. Sasa kama mama mwenye nyumba hajuhi kupika jua fika hata housegilr hataweza pika chakula kizuri; nani atamfundisha??? Kama mama hajuhi kufua wala usafi wa ndani jua nyumba itakuwa chafu hata kama mna housegirl watatu kwani mkeo hatakuwa anaona kasoro.

Hata makazini supervisor mzuri ni anayejua kazi. Kwa hiyo hata kama hatufanyi kazi za ndani very often we are good supervisors because we know them. Mimi housegirl hakiacha kazi naona mme wangu anavyokuwa na furaha maana ananotice difference ndani katika kila nyanja. Bahati mbaya siwezi hacha kazi.

Nina shemeji yangu alikuwa na girlfriend wake wa muda mrefu saana mdada anakuja gheto kwa shem anampikia afu anaacha vyombo kibao kwenye sink anatimua mpaka nyumba inatoa harufu. Mwisho wa siku jamaa hakuoa japo am sorry kwani alikuja mzalisha dada wa watu. Ila washikaji wote walikuwa wanamwambia jamaa ukioa hapo umevaa mkenge.

Hivi nyumba kubwa mtu anaweza kukulazimisha uanze majukumu ya ndani ya nyumba kama wife?
mie naona ile huwa tunafanya wenyewe kwa kupenda ..unajefeel kupika pika kama utashinda kwa mwenzio
ukiona nyumba chafu utasafisha na mengineyo kibao.
 
Back
Top Bottom