Kuhesabu muda

Hahha kwa mujibu wa swali lako umekusudia muda ni nini ?

Ukitoka nje ya dunia(bila kifaa chakuhesabu muda) ukaingia universe huko ambako hakuna day and nights je kuna Muda ?
 
Kama walitumia kigezo cha jua kupanga saa unadhani ingeshindikana ile saa 7 mchana kuiita saaa moja mchana?

Kwa nini ingeshindikana?
Kwa miaka ya zamani mwenendo ya jua na mabadiliko ya mchana na usiku vilitumika kuhesabu muda. Na ndio wataalamu baada ya kusayansi kujua wakatumia hilihilo jua kupangilia saa, sekand n.k

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yaani mkuu penye utata ni kwamba jee muda hauwezi kupimwa kama kuna tukio moja tu limefanyika na sio mawili kama anavyosema bwana mkubwa Albert?


Mkuu Safuher, hebu toa mfano mmoja unaokiuka hiyo concept ya Einstein.
 
Kwa hiyo yupi anamtegemea mwenzake kati ya muda au matendo?

Matendo ana muhitaji muda ili atokee au muda ndo unahitaji matendo ili uitwe muda?

Na muda unaokusudiwa ni upi?
Dakika na sekunde na lisaa ?,au mchana,asubuhi jioni,usiku?


Muda hauwezi kuwepo bila kuwepo kwa matukio, muda ni zao la matukio (function of events).

Mfano unapotaka kujua umri wa mtu utaanza kuuliza kazaliwa lini na leo ni mwaka gani kutokana na hayo matukio mawili yaani mwaka wa kuzaliwa na mwaka huu wa sasa, ndipo utakapoweza kujua muda (umri wake). Hapo ndipo Einstein aliposema muda unazuia matukio mawili yasitokee kwa pamoja, kama yangetokea kwa pamoja usingeweza kupata muda (umri wa huyo mtu).

Au turahisishe hivi; mtu kazaliwa 1940 na kafariki 1960, muda wake alioishi duniani ni miaka (1960-1940=20) miaka 20, hapo utaona kuna matukio mawili kuzaliwa na kufariki ambayo hayakutokea kwa pamoja na ndiyo maana umepata muda wa miaka 20, sasa kama ungeambiwa mtu kazaliwa mwaka1960 na kafariki mwaka huohuo 1960 tafuta muda (miaka) alioishi hapo utapata hukuna muda yaani miaka 0, kwasababu hapo matukio yote ya kuzaliwa na kufa yametokea kwa pamoja (katika mwaka mmoja).

Hiyo ndiyo concept ya Einstein kuhusu "muda"--- huyu jamaa alikuwa very genius, kwa sababu hiyo concept kwa hakika mimi binafsi naikubali sana.
 
BA's tuchukue iyo ya mwanzo wa kitu na mwisho ndio huunda muda, kwaiyo hata nikifanya vitu nane kwa wakat mmoja bado ntatengeneza muda maana nilianza nkamaliza

But iyo theory haijakaa vzur au bado hatujaielewa


Hauelewi nini, kupima muda lazima kuwe na matukio mawili, mfano ukisema" leo nimewahi kula chakula"-- swali linakuja umejuaje kwamba umewahi kula chakula??, jibu litakuwa umepima muda na ukaona jana ulianza kula saa 6 na leo umeanza kula saa5, hivyo kutokana na hayo matukio mawili ya jana kula saa 6 na leo kula saa 5, ndipo umeweza kupima muda na kujua leo umekula mapema.

Hivyo ni kutokana na matukio ndipo unaweza kuhesabu au kupata muda. Hiyo ni dhana (concept) aliyoitengeneza Einstein ili kujua "muda" ni nini, kwa sababu hakuna definition ya muda ila kuna concepts tu.
 
Mfano wa mwanzo ambao naona kama una utata ni hivi

"nimeanza kutembea huku naimba kwa pamoja na nikastop kufanya vitu vyote ndani ya dakika 10"

Mfano huu hauonyeshi kwamba vitu viwili nimevifanya kwa nyakati moja na havina tofauti ya muda baina ya kitendo kimoja na kingine?

Kwa mujibu wake Bwana mkubwa haimaanishi kwamba hapokatika vitendo hakuna muda?

Mkuu Safuher, hebu toa mfano mmoja unaokiuka hiyo concept ya Einstein.
 


Hapo kweli utakuwa hujaelewa hiyo concept, hapo matukio siyo kutembea na kuimba kwa pamoja, ukichukua matukio ni kuimba na kutembea kwa pamoja basi muda ni sufuri kwa sababu matukio yote yameanza pamoja na kumalizika pamoja na hapo huwezi kuwa unatafuta muda labda unatafuta jambo jingine.

Concept ya Einstein hapo iko


Huo muda wa dakika 10, umeupataje??😁😁, jinsi ulivyopata huo muda ndivyo hivyo hiyo concept inavyosema.

Hapo bila shaka utakuwa umekwisha elewa.😁😁
 
Kwa hiyo kumbe bwana eistein hajakusudia kwamba kama hakuna tofauti ya muda baina ya kitendo na kitendo basi hakuna muda?
Kumbe hakukussudia hivyo?
Kumbe alikusudia kwamba vitendo vinaweza kufanyika kwa pamoja na vikaisha kwa pamoja na ikawa hakuna tofauti ya baina ya kitendo na kitendo na Muda upo tu hata kama vitendo havina tofauti ya uanzaji na uishaji wwake?
Ndo alikusudia hivyo?
 


Naam, na hapo katika huo mfano wako hatuzungumzii vitendo vya kutembea na kuimba ili kuelewa concept ya Einstein bali tutazungumzia juu ya matukio ya kuanza kuimba na kutembea na kumaliza kuimba na kutembea, ni kuanza na kumaliza ndipo utaweza kupata muda wa hivyo vitendo vya kutembea na kuimba.

Hiyo ndiyo concept ya Einstein juu ya "Muda."
 
Ndio sasa nimeanza kuimba na kutembea pamoja na nikamaliza kuimba na kutembea pamoja... Jee muda = zero hapo?

 
Ndio sasa nimeanza kuimba na kutembea pamoja na nikamaliza kuimba na kutembea pamoja... Jee muda = zero hapo?


Uki -note muda ulioanzia kuimba na kutembea (event 1) na uka- note muda uliomalizia hivyo vitendo (event 2), hapo lazima upate muda, na hiyo ndiyo concept ya Einstein.

Lakini ukifanya kutembea na kuimba ni events hapo hupati muda wowote-- na hiyo haitakuwa concept ya Einstein kuhusu "muda".
 
Kwa hyo comcept ya jamaa kwamba muda ni tofauti baina ya kuanza jambo na kumaliza?

Ama kuanza kwa jambo tu hata kamalisiishe lakini kuna wakati maalumu limeanza?

Na ni jambo lolote lile lile?

Kwa sababu hakuna pahala ambapo hakuna vitendo hata kama pametulia tulii?
 
Mmmh hv mnaoandka hv uko mnapo copy mnashindwa ku convert au dah
 
Watu wangekua wanawaza kama wewe leo tusingekua na chochote zaidi ya zana za mawe na mifupa magonjwa kama small pox polio yangeendelea kututesa ila uwepo wa watu wanaotumia akili ipasavyo wamesababisha tupo hapa tulipo.
Wewe endelea kuipumzisha akili yako tu
 
Muda ni kihisishi hakuna muda cjui mnabishani nn hapa tambua ulipo upo hapo hapo izo number majuma visiwachanganye,muda haupo...hivi hamkuwai ckia miaka ilishawai kuhesabiwa ikirudi nyuma na je kabla ya kuanza hesabu miaka ilikuwa na ilichukua makisio gani,endapo mkija katika swala lenu la muda time ni illusions,haipo.
 
Muda ni nini mkuu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…