Shukrani kwa hii nyongeza ya nguvu mkuu.Mkuu Safuher, umetoa majibu mazuri sana, majibu hata mimi ningejibu kimsingi ningejibu hivyo hivyo.
Ila cha kuongeza kidogo ni kwamba wahenga wanasema shida ni mgunduzi na kitu chenye manufaa hudumu manaa yake ni kwamba siku zote akili ya mwanadamu inafanya kazi kupambana na mazingira yake, ilipofika wakati ambapo muda ilibidi upimwe ndipo mwanadamu toka awali akabuni mbinu mbalimbali kupima muda kwa siku- hususan walitumia jua kujua wakati wa mawio,mchana na machweo pia walitumia vivuli vya miti na vijiti vinavyobadilika kimo kutokana na mwendo wa jua nk,pia watu hao walitumia matukio makubwa kama vipimo vya wiki,miezi na miaka, kwani utasikia wazee wa zamani wanakuambia kwamba; "mimi nilizaliwa mwaka wa nzige"yaani ni kipindi kile ambacho nzige wengi walitokea katika eneo lao.
Leo binadamu amefikia maendeleo makubwa makubwa mno sio tu ya kupima muda bali hata kujua muda uliopita na kuuhifadhi tofauti na ilivyokuwa karne zilizopita, leo kuna "nuclear clock" saa inayolinda muda kwa usahihi zaidi kuliko saa zote duniani (karibu saa zote zinapoteza majira kadiri muda unavyopita). Bado uvumbuzi unaendelea kila uchao na mambo yasiyokuwa na manufaa binadamu huyaacha na hubaki na yale yenye manufaa tu ndivyo Mungu alipanga hivyo.
Muda ni nini?, hakuna definition maalumu ya muda, ila A, Einstein mwanafizikia maarufu akitoa definition ya muda na alisema; "time is what stops two things from happening at the same time"--- yaani; muda ni ile hali inayozuia vitu viwili visitokee kipindi kimoja. Mfano kama vitu viwili vitasnza kutenda kazi kwa pamoja na kuacha kutenda kwa pamoja na ukaulizwa utoe utofauti wa muda kati ya vitu hivyo vilipoanza kutenda kazi na kumaliza utaona muda ni sufuri lakini vingeanza kipindi tofauti hapo ungepata muda uliokuwa tofauti--- hiyo ndiyo definition ya muda/wakati iliyotolewa na A. Einstein.
Mungu ni wa kushukuriwa aliyeweka mazingira hadi sisi binadamu tukaweza kupima muda kwa faida yetu.
There is no place in this world in which there is no time; rather that cannot be imagined, for time and place are bound together. Time is the duration of the existence of this universe, and place is the space that is occupied by created entities when they exist. If they stop occupying space, then this means that they have ceased to exist and no longer exist. Similarly, if no time passes for them, then they never existed in the first place.
Sasa mkuu tunaipataje maana ya muda yaaani Muda ni nini kwa maana ya muda?[emoji1312]Maelezo hayo nimeyaona kwa kiasi fulani ndiyo yanakaribia kujibu msingi wa maswali yaliyoulizwa na mleta mada, na hapa chini nimejaribu kutafsiri kwa kiswahili na kama atakuwepo mjuzi zaidi naye anakaribishwa kutoa tafsiri nzuri zaudi.
" hakuna mahali katika dunia hii ambapo hakuna muda,tuseme haiwezi kufikiriwa kwa sababu muda na mahali vimeshikamana pamoja. Muda ni kipindi cha kuwepo kwa huu ulimwengu na mahali ni anga iliyokaliwa na vitu vilivyoumbwa katika kipindi vinapokuwepo. Kama (vitu hivyo) vitaacha kuikalia anga (space) basi maana yakeni kwamba vimeacha kuwepo na havipo tena, halikadhalika, kama hakuna muda utakaotumiwa na hivyo vitu (basi ni wazi) kamwe vitu hivyo havikuwahi kuwepo.
Ahahahahahaahahhhahha aiseeee hatari sana.
Sasa mkuu tunaipataje maana ya muda yaaani Muda ni nini kwa maana ya muda?
Je sekunde,dakika,lisaa ni katika muda ?
Naam mkuu nakupata pata kwa mbali..Mkuu maana (definition) ya muda ni ngumu sana, yaani hakuna definition maalumu, hata wanasayansi wakubwa wameshindwa kupata definition inayokubaliana kwa pamoja, lakini kila mmoja amejaribu kutoa definition kulingana na jinsi yeye anavyoelewa "Muda".
Kuna definition moja ya Albert Einstein (mwanafizikia mnadharia), yeye ndiye aliyekokotoa nadharia ya "special theory of relativity" (nadharia maalumu ya mahusiano) kati ya anga (space) na muda.
Kuna mahusuano kati ya anga na muna vitu vilivyopo katika ulimwengu na nishati.
Einstein anasema; "Muda ni ile hali inayotenganisha matukio mawili yasifanyike kwa pamoja"
Jambo la msingi hapo ni kwamba huwezi kuongelea kuhusu muda na anga bila kuwa na matter (viumbe), kama jinsi katika ile tafsiri yule mtaalamu alivyosema.
Equation yenyewe ni hii:-
E=mC²
Hapo utaona mahusiano ya E=nishati, m=mass, C= velocity of light, ambapo katika C kuna umbali (space) na muda.
Hiyo ni theory wala sio princple..wala ucjali ..hayo ni mawazo yake yeye aliyesema. Ww unaweza ukasema yakoNaam mkuu nakupata pata kwa mbali..
Ila hyo tafsiri ya huyo bwana kwamba ""Muda ni ile hali inayotenganisha matukio mawili yasifanyike kwa pamoja"
Sasa hapa mimi ninaomba kuuliza kwa njia ya kuelezea.
Kutokana naa maana ya Albelt hii maana yake ...
Kwanza kila tukio lazima liwe na mfanyaji wake
Hakuna tukio litafanyika bila mtendaji wake.
Pili tunapoona tukio lolote mfano tukisikia sauuti ya viatu.basi tunajua kuna mtu anatembea n.k.
Sasa kwa maana ya bwana albelt. ""Muda ni ile hali inayotenganisha matukio mawili yasifanyike kwa pamoja"
Ina maana matukio mawili yakifanyika kwa pamoja hatupati kitu kinaitwa muda?
na je matukio hayo mawili ni sharti yatokane na sababu moja?
Mfano sasa...
Mimi naweza nikawa natembea huku naimba.
Hapa kuna matukio mawili nimeyafanya kwa pamoja.
1.natembea (T1)
2.Naimba (T2)
Sasa hapa hakuna hali ambayo imezuwia T1 na T2 yasifanyike kwa pamojaa.
Sasa je KWA MUJIBU WA ALBET KUTOKANA NA kutokuwepo kwa pingamizi la kufanya T1 na T2 kutokea ina maana hapo hatuwezi kupata maana ya muda kwa kuwa hakuna kilichozuwia T2 NA T2 visifanyike kwa wakati mmoja?
Au unaweza kunipa mfano wako ambao unawezaa kuelezea vizuri hii theory
Hiyo ni theory wala sio princple..wala ucjali ..hayo ni mawazo yake yeye aliyesema. Ww unaweza ukasema yako
Kama ulichokusudia kuuliza muda huu ambao ni sekunde,dakika,saa,masaa basi muda huu haupo.Nahic unakitu nachotafta mkuu, fungua box
Naam mkuu nakupata pata kwa mbali..
Ila hyo tafsiri ya huyo bwana kwamba ""Muda ni ile hali inayotenganisha matukio mawili yasifanyike kwa pamoja"
Sasa hapa mimi ninaomba kuuliza kwa njia ya kuelezea.
Kutokana naa maana ya Albelt hii maana yake ...
Kwanza kila tukio lazima liwe na mfanyaji wake
Hakuna tukio litafanyika bila mtendaji wake.
Pili tunapoona tukio lolote mfano tukisikia sauuti ya viatu.basi tunajua kuna mtu anatembea n.k.
Sasa kwa maana ya bwana albelt. ""Muda ni ile hali inayotenganisha matukio mawili yasifanyike kwa pamoja"
Ina maana matukio mawili yakifanyika kwa pamoja hatupati kitu kinaitwa muda?
na je matukio hayo mawili ni sharti yatokane na sababu moja?
Mfano sasa...
Mimi naweza nikawa natembea huku naimba.
Hapa kuna matukio mawili nimeyafanya kwa pamoja.
1.natembea (T1)
2.Naimba (T2)
Sasa hapa hakuna hali ambayo imezuwia T1 na T2 yasifanyike kwa pamojaa.
Sasa je KWA MUJIBU WA ALBET KUTOKANA NA kutokuwepo kwa pingamizi la kufanya T1 na T2 kutokea ina maana hapo hatuwezi kupata maana ya muda kwa kuwa hakuna kilichozuwia T2 NA T2 visifanyike kwa wakati mmoja?
Au unaweza kunipa mfano wako ambao unawezaa kuelezea vizuri hii theory
Ukitoka nje ya dunia(bila kifaa chakuhesabu muda) ukaingia universe huko ambako hakuna day and nights je kuna Muda ?Kama ulichokusudia kuuliza muda huu ambao ni sekunde,dakika,saa,masaa basi muda huu haupo.
Bali hizo sekunde dakika na saa ndio zipo.
Hakuna kiashiria chochote kile ambacho kinaweza kutufahamisha kwamba sasa hivi ni saa ngapi na dakiks ngapi isipokuwa hivyo vifaa vyenye mishale na namba(saa).na wala hakuna kiashiria wsla ishara ya kilimwengu itakujulisha kwamba sasa hivi ni sekunde kumi,ama saa moja limepita.
yaani kwa maana hatuwezi kuitambua dakika mpaka tuangalie kifaa kinachoitwa saa.
Hatuwezi kutambua saa ngapi mpaka tuangalie saa
Hatuwezi kutambua sasa ni sekunde ngapi mpaka tuangaliee saa.
Yaani kuitambua saa inabidi urejee kwenye saa hiyo hiyo utizame inacheza vipi na vipi.
Sasa kama saa ni kitu kipo katika ulimwengu basi ingekuwa bila saa hiyo tunaweza kutambua sasa ni saa ngapi na dakika ngapi.
Kilichokuwepi ni majira tu.
Kuna majira ya mchana.
Jioni
Asubuhi
N.k
Haya hata iweje lazima tujue kwamba haya ni majira ya mda fulani na fulani.
Jaribu kufukiria wazee wazamani ambao walikuwa wanavaa magome ya miti na kuishi kiasili unadhani walikuwa wanajua sekunde ama dakika ama saa?
Kama walikuwa hawajui unadhani vilikuwepo hvyo visekunde dakika na saa vilikuepo?
Sekunde dakika na saa ni mawazo ya mtu tu ambayo alitengeneza kifaa kiawaa kijajihesabu namba na kujizungusha mshale akaita hapa sekunde ama dakika.
Saa haina mahusiano na ulimwengu wetu ama dunia yetu.
Ili uitambue saa na dakika maalum na sekunde maalum basi huwe,i kutambua mpaka uitizame hiyo saa.
Dunia haipo kwenye saa,bali saa ndo ipo katika dunia.
Alhamdulillah, kidogo utakuwa hujanielewa, tuchukue mfano wako huohuo wa kutembea na kuimba,mtu anatembea huku anaimba, halafu mtu akamuuliza ataje tofauti kati ya muda anaotembea na muda anaoimba.
Kwakuwa anafanya vitendo vyote kwa pamoja hapo katikati hakuna muda au unaweza kusema muda ni sifuri, lakini kama alianza kutembea bila kuimba na baadaye akasimama na akaanza kuimba hapo muda upo kati ya hayo matendo mawili ambayo yametendeka kwa muda tofauti.
Hiyo ndiyo definition ya muda aliyojaribu kufafanua Albert Einstein. Katika tukio la kwanza muda ni sufuri na katika tukio la pili muda upo (siyo sifuri).
Ukitoka nje ya dunia(bila kifaa chakuhesabu muda) ukaingia universe huko ambako hakuna day and nights je kuna Muda ?
Utasemaje kutembea na kuimba kwa pamoja hakuna muda, ilihali cku nzima adi Giza linaingia natembea nakuimba
Ni ngumu sana kueleweka[emoji16][emoji16], ni hivi; muda unapimwa au unapatikana kutokana na matukio yanapoanza na kuishia---- hapa ikumbukwe kwamba watu walimuuliza Einstein kwamba muda ni nini ?? Ndipo alipojaribu kuleta hiyo concept rahisi ili watu wote wapate kuelewa.
Ukitembea na hapohapo ukiimba, muda wako utauhesabu toka ulipoanza kutenda hayo matendo na hadi ulipoacha.
Muda= muda ulipomaliza kutenda toa muda ulioanza kutenda.
[emoji1312]Hapo unaona ni lazima matukio yawepo. Yaani utahesabu muda kutoka mahali fulani hadi mahali fulani hiyo ni lazima.
Au ukumuuliza mtu amelala masaa mangapi, ataanza kuhesabu muda alianza kulala hadi muda alioamka--- hapo kuna matendo mawili kulala na kuamka.
BA's tuchukue iyo ya mwanzo wa kitu na mwisho ndio huunda muda, kwaiyo hata nikifanya vitu nane kwa wakat mmoja bado ntatengeneza muda maana nilianza nkamaliza
But iyo theory haijakaa vzur au bado hatujaielewa

Sasa nimeamini kuwa physics ni ngumu, A Einstein alijaribu kudadavua kwa njia rahisi ili watu wajue muda ni nini?, kwa sababu hakuna definition ya "muda" iliyopo sasa hivi na ndio maana akachukua matukio kama njia ya kujua "muda"--- kati ya tukio moja na jingine hapo utapata muda unaotenganisha hayo matukio na kama hayo matukio yatatokea kwa wakati mmoja na kumalizika kwa pamoja hapo katikati ya hayo matukio huwezi kupima muda yaani muda ni sifuri lakini unaweza kupima muda wa hayo matukio kwa kupima utifautwa muda wa kuanzia na na muda wa kumalizikia kwa maana hiyo hapo kutakuwa bado kuna matukio/matendo mawili tendo la kuanza na tendo la kumalizikia.
Muda unapimwa au upo baina ya matukio mawili, --- hiyo ndiyo ilikuwa ufafanuzi wa concept ya Einstein.
Waswahili husema; usiku wa deni uchwa haraka/mapema. Yaani unapokuwa unadaiwa na unaambiwa kesho mkopi wako anakuja utaona usiku umekuwa mfupi kuchwa hapo ni kwamba muda ni hesabu ya ubongo yaani toka ulipo lala na mawazo ya deni hadi ulipoamka na mawazo hayohayo basi akili inajenga hisia kwamba muda umekuwa japo ni masaa yaleyale unayolala siku zote, au kinyume chake "usiku wa shida huchelewa kuchwa". hiyo ndiyo concept ya relativity ya Einstein kuhusu muda na akili ya mtu.
Hivyo "muda" ni dhana inayoweza kutafsiriwa kirahisi kutokana na matukio/matendo. Muda umo au unahesabiwa katikati ya matukio.