Kuhamia Dodoma: Bajeti kuvurugwa ili kuhamisha maelfu ya watumishi, wadau wasema bunge hakuna fungu

Nimesikia wizara ya kilimo,mifugo na uvuvi inaanza kuhamia wiki ijayo ikifuatiwa na wizara ya Nishati na Madini
 
Baada ya mh. Rais kutangaza serikali kuhamia Dodoma katika kipindi chake hiki cha miaka mitano, tayari idara na wizara mbalimbali zimetangaza kuhamia Dodoma ndani ya kipindi hiki cha bajeti hii. Moja ya wizara hiyo ni wizara ya kilimo ambayo imetangaza kuhamia Dodoma wiki ijayo.
Pia, ofisi ya waziri mkuu imepanga kuhamia Dodoma mwezi september mwaka huu.
My take:
Hivi Bajeti hii tulipanga hii mihamo ya kuhamia Dodoma? Kama hatukupanga pesa zinatoka wapi?
Wizara zote wana ofisi zao Dodoma japo si kubwa lakini zinafanya kazi kipindi mawaziri wanapokuwa kwenye vikao Dodoma .
 
Kwa nini bavicha mko negative sana, hamuoni vitu on a positive side? Mmerogwa!!


kabisa wakihamia dodoma tutakuwa na uhakika wa kufufua hata ka kiwanda kamoja kuhama ni moja ya maendeleo na nchi itapiga hatua kiuchumi.
 
Tuweke Orodha Ya Wateuliwa Wa Rais Ambao Kimsingi Na Agizo Lake Lazima Aende Nao Dodoma Kule:-
Makamu Wa Rais
Waziri Mkuu
Mkuu Wa Majeshi (CDF)
Mkuu Wa Jeshi La Police
Mkuu Wa Usalama Wa Taifa
Mkuu Wa Takukuru
Mkuu Wa Jeshi La Magereza
Ongozeeni Orodha

mkuu wa mkoa wa Dar es salaam
 
Ni wazi kwamba bajeti inaelekea kuvurugwa ili kuhamisha maelfu kama si malaki ya watumishi wa umma kuelekea Dodoma.

Bunge la bajeti halikupitisha wala kujadili fungu la pesa ili kuhamisha maelfu ya watumishi, kujenga majengo, kukodi majengo, kuhamisha mali za wizara zilizoko Dar es salaam.

Mvurugano huu unatibua hata kile kidogo kinachotarajiwa kutoka awamu ya tano!

Fungu lipi litabanwa? La kuajiri? La Miundombinu? Au Posho za Watumishi?
China na baadhi ya nchi za ulaya na America watatoa fungu
 
Kwa nini bavicha mko negative sana, hamuoni vitu on a positive side? Mmerogwa!!
Hoja yako ni nini? Hivi haya ni Mawazo ya ccm au yako binafsi?
What is the positive side? It is prudent to keep quiet if you are ignorant. Absence of that you may seem stupid.
 
Ofisi ya PM ilihamishiwa Dodoma wakati wa Sokoine (~miaka 34 iliyopita) lakini PM mwenyewe hakuhama hadi leo! Kiutaratibu, ofisi zote za kibalozi na za mashirika ya kimataifa yenye hadhi ya kibalozi zinapaswa kuwa pale makao makuu ya serikali yalipo. Balozi zenye majengo makubwa na ya kudumu kama Marekani, Kenya, Zambia na nchi za Umoja wa Ulaya (EU) hazina namna itabidi watafute viwanja na kujenga upya Dodoma!

Ndio maana kunahitajika mpango ambao utashirikisha wadau wote, huwezi kuhamisha makao makuu bila kuwa na sera na mpango madhubuti. Hakuna anayepinga uamuzi huu kinachotakiwa na ujadiliwe kwa kina na kufanyike impact assessment.
 
Mpango wa kuhamisha makao makuu ulipangwa mwaka 1974 ambao ulikuwa unaitwa ''Plan for the New Capital of Tanzania'' . Mpango huo ulifanywa na International consulting organization inayitwa Project Planning Associates Limited of Toronto, Canada.

Serikali inatakiwa ifanye marekebisho ya mpango huo kwani utakuwa umepitwa na wakati. na marekebisho yanatakiwa yashirikishe wadau muhimu kama balozi ambazo kisheria zinatakiwa kuwa karibu na makao makuu ya nchi. Na ikumbukwe kwamba balozi nyingi zimeshajenga majengo yao pamoja na kuweka miundombinu ya kiusalama, hivyo iyakuwa ngumu kuwahamisha kwa haraka kwani pia wanahitaji muda wa kufanya mipango huko kwao.
 
Kwa nini bavicha mko negative sana, hamuoni vitu on a positive side? Mmerogwa!!

Ni vema viongozi watende kama wanavyowatamkia wanaowaongoza, huwezi ku ''advocate good governance and rule of law'' halafu unatenda exactly the opposite...moja ya misingi ya utawala wa sheria ni separation of power kati ya serikali na bunge ambapo matumizi yote ya fedha zinazoombwa na serikali NI LAZIMA ZIIDHINISHWE NA BUNGE. Je kwenye bunge lililoisha juzi kuna fedha zimeidhinishwa kwa wizara na taasisi zake kuhamia Dodoma? Kama serikali inaamka tuu asubuhi na kwenda Hazina kuchukua fedha na kuzitumia pasi na kufuata bajeti iliyopitishwa na bunge basi hakuna haja ya kuwa na bunge tena.
 
Back
Top Bottom