Kugombana na mpenzi

Wakuu habari zenu,
Naombeni ushauri,nina best yangu mmoja alikuwa kwenye mahusiano na binti wa kichaga almost 5 yrs,sasa huyo binti alikuwa mtu wa kubebelea pale alipokuwa anaudhiwa pamoja na kuwa jamaa alikuwa anaapologize,sasa kama miezi miwili imepita binti anamwambia jamaa atamtesa na kumuumiza kama alivyomuumiza,sasa now the girl hapatkani hewani,na anajua jamaa anampenda sana,nimeshindwa xga kumahauri,je amuangaikie au ampotezee,..Ila jamaa anaumua sana
Tumsaidieni huyu kijana.

Mzee hawa watu hawafugiki kabisa na ni watu hatari sana. Hawajui mapenzi na hawajui utu, wao ni pesa tu. Ni bora ameondoka amuache tu. Akimtafuta akampata atakuja kujuta mbeleni.
 
Kwanza, ningeweza kuanzia kwenye historia ya huyo dada kwenye suala la mahusiano. Inawezekana huyo dada aliwahi kuumizwa sana kabla hajakutana na huyo kijana. Sasa yale maumivu yakaweka jeraha ndani ya moyo, jeraha ambalo bado halijapona. Ndiyo maana, likitokea jingine la kumuumiza hata kama ni dogo, yeye anaunganisha na alipotoka, alivyoumizwa, na kuona hakuna haja tena ya kuendelea. Ndiyo maana anafunga na simu kabisa ili asipatikane.

Pili, ningeweza kuangalia huyu dada amekutana na huyu kijana kipindi gani. Kwa mfano: Kama huyu dada aliumizwa kwenye mahusiano yaliyopita, halafu ndani ya kipindi kifupi akaingia kwenye uhusiano wa sasa, basi hapo ndipo shida ilipoanzia.
Watu wengi, wakiumizwa, wanaingia kwenye uhusiano mpya haraka ili kupoza maumivu waliyoyapata walikotoka (rebound relationship), huku wakiamini kupata pumziko. Sasa inapotokea mtu wa namna hiyo akakutana na mambo yale yale yaliyomuumiza hapo kwanza, ni lazima ataanza tabia hiyo kama ya huyo dada.

Tatu, kitendo anachofanya huyo dada, maana yake nini? Huyo dada anatafuta namna ya kujilinda ili asiumie kama alivyoumia hapo kabla. Kwa kawaida, moyo unapoumizwa kwa kiwango cha juu, huwa una tabia ya kujifunga. Sasa, mtu wa namna hii, asipopata msaada, anaweza kufika hatua ya kutopokea upendo tena, kwa sababu ya hofu ya kuumizwa. Kwa hivyo basi, huyu dada anahitaji msaada, kuondolewa hofu iliyopo ndani yake. Kwa sababu, hofu ya kuumizwa ni mbaya kuliko kuumizwa kwenyewe.

Cha kufanya: Kwa kuwa huyu dada amezima simu yake, namshauri huyo kijana asimtafute. Atulie kwanza, ampe muda huyo dada wa kujitafakari. Maadamu, ameshaomba msamaha kwenye jambo ambalo huyu dada hakulipenda, basi ampe muda. Asimtumie message, wala kumpigia simu. Amuache kwanza.
Huyu dada atakapokuwa tayari, ataona umuhimu wa huyu kijana, na ndipo atamtafuta yeye. Sasa ikifika hapo, namshauri huyo kijana azungumze na huyu dada. Amuondolee hofu zozote ambazo huyu dada amezijenga juu ya mahusiano. Ninaamini, baada ya hapo, mambo yao yatakwenda vizuri.
 
Asipopatikana kwa muda mrefu maana yake hana muda na jamaa maana mapenzi ni mawasiliano hvyo jamaa ajikaze kisabuni ampotezee na baada ya muda atafute mwingine
 
Shukrani kwa ushauri mkuu,maana wamedumu kwente mahusiano kwa mda sana,na hata pande mbili zote za familia zinafaham..Na huyu kijana anampenda sana
 
Na hata hivyo huyo binti,huyo jamaa ni mtu waje wa kwanza kwenye mahusiano
 
Sawa mkuu, kama ni mtu wake wa kwanza, basi cha kufanya hapo huyu kijana ajitahidi sana kumtia moyo huyu dada kuwa safari ya mapenzi ni safari yenye changamoto na inahitaji uvumilivu. Kwa sababu mara nyingi mtu anapoingia kwenye mapenzi kwa mara ya kwanza, anategemea kila siku itakuwa ni furaha na vicheko. Sasa akikuta tofauti na hapo, anaanza kuona vibaya. Mimi ninaamini huyu kijana yupo kwenye nafasi nzuri sana ya kumfanya huyu dada awe vile anavyotaka. Ninamsihi tu, asimuache huyu dada, aendelee naye, na watafika mbali, na Mungu awasaidie.
 
Shukrani sana mkuu kwa ushauri,sasa hapo njia iliyobaki ya kumpata itabidi amtaute waonane face to face
 
Naam, kabisa. La muhimu hapo amtafute, waonane na wayazungumze. Mimi bado naamini mambo yao yatakwenda vizuri sana.
 
Mwambie mchiz amwache aende. Najua huyo dada ameondoka na akili nusu... nakwambia atarudi na sababu kibao....
Ww utaona mwenyewe..
 
So miss chaga unaweza ukamwacha mwanaume ambaye mnapendana kisa pesa??
yani nakuambia ukweli namuacha tena bila kupepesa macho nitakuala mapenzi mimi? nitaendesha mapenzi we pesa kwanza nitajifunza kupenda huko huko..
 
Back
Top Bottom