passioner255
JF-Expert Member
- Apr 22, 2019
- 6,784
- 13,007
Natumaini kila mmoja kuanzia serikali, viongozi wa dini na watanzania wote mmeona Kwa kiasi gani watanzania wamegawanyika Kwa Sababu ya maneno na matendo ya wanasiasa.Imefika wakati mwanasiasa mmoja akifariki watu wengine wanafurahi na kufanya mpaka sherehe.Juzi mwanasiasa mmoja alifariki natumaini kila mmoja aliona comments za watu.Watanzania wengi walifurahia kifo cha mtu huyo.Mimi nashauri serikali isiruhusu matamko tata ya hao wanasiasa Kwa Sababu Taifa liligawanyika baada ya kauli za kufuru zilizotolewa na baadhi ya wanasiasa baada ya kifo cha Rais Magufuli,pia hao wanasiasa waombe msamaha Kwa maneno Yao Ili kuleta umoja na pia viongozi wa dini waiombee nchi Sana. Hali hii ikiacha iendelee itasababisha nguzo mojawapo ya nchi yetu yaani 'umoja' kuhatarishwa.Nashauri pia viongozi wabadhilifu watokomezwe Katika nchi yetu Kwa Sababu hao ndo wanakuja na matamko tata baada ya kubanwa. Pia wanasiasa nawaasa wawe makini na kauli zao maana zinahatarisha umoja wa watanzania pia wajue kuwa malipo ni hapahapa dunia yaani kauli zao zinawarudia wakiwa hapahapa duniani yaani ukitoa kauli za laana na wewe utapata laana.