Kugawanyika Kwa watanzania

Kugawanyika Kwa watanzania

Kinawatu wanajifanya miungu watu kwamba nchi niyao na wanaweza kuitafuna bila kuulizwa.

Jembe alivunja huo umunguwao nakuweka ugumu kwenye upigajj hali iliyowafanya kuchukizwa sana na hatimaye wakafurahia kifochake.

Hawa unaowaona humu ni dagaaa waganga njaa tu waliokuwa wanaokota angalau makombo ya mafisadi.
Wao pia maisha yalikuwa magumu baada ya bwanazao kubanwa na hawata sahau milele.

Ukiona mtu anajaribu kumchafua Jembe ujue aidha alikuwa mkwepa Kodi, mlarushwa, cheti feki ama alikuwa na kamrija kwenye mtungi wa fisadi.

Nawanufaika waufisadi wapo mpaka wapinzani uchwara wote wakina zzk walio kataa kuzikwa lirondo pia ndio wahusika wenyewe.

R.I P Jembe wananchi wazalendo wanakukumbuka milele.
Walifanya sherehe kwakuwa waliona Wanaenda kuwa huru kufanya wanayotaka Ila Mungu yupo upande wa watanzania.
 
Kama serikali saa100 hawaelewani raisi akisema hata amna anayemsikiliza unategemea nini
Unajua hata maagizo ya Rais sikuhizi watu hawaogopi Yani hawana viongozi wenyewe hawana umoja.
 
Natumaini kila mmoja kuanzia serikali, viongozi wa dini na watanzania wote mmeona Kwa kiasi gani watanzania wamegawanyika Kwa Sababu ya maneno na matendo ya wanasiasa.Imefika wakati mwanasiasa mmoja akifariki watu wengine wanafurahi na kufanya mpaka sherehe.Juzi mwanasiasa mmoja alifariki natumaini kila mmoja aliona comments za watu.Watanzania wengi walifurahia kifo cha mtu huyo.Mimi nashauri serikali isiruhusu matamko tata ya hao wanasiasa Kwa Sababu Taifa liligawanyika baada ya kauli za kufuru zilizotolewa na baadhi ya wanasiasa baada ya kifo cha Rais Magufuli,pia hao wanasiasa waombe msamaha Kwa maneno Yao Ili kuleta umoja na pia viongozi wa dini waiombee nchi Sana. Hali hii ikiacha iendelee itasababisha nguzo mojawapo ya nchi yetu yaani 'umoja' kuhatarishwa.Nashauri pia viongozi wabadhilifu watokomezwe Katika nchi yetu Kwa Sababu hao ndo wanakuja na matamko tata baada ya kubanwa. Pia wanasiasa nawaasa wawe makini na kauli zao maana zinahatarisha umoja wa watanzania pia wajue kuwa malipo ni hapahapa dunia yaani kauli zao zinawarudia wakiwa hapahapa duniani yaani ukitoa kauli za laana na wewe utapata laana.
Tusizunguke mbuyu hapa. Magufuli ndiye muasisi wa haya mambo. Yeye ndio alikuwa mbaguzi #1. Tatizo hawezi kufufuka akemewe. Hao wabadhirifu aliowabana ni wepi? Inner circle ya magufuli- makonda, sabaya, Ali hapi, biswalo etc unajua ukwasi waliojikusanyia ndani ya muda mfupi?
 
Uzuri hata marehemu baba yako hakupendwa na watu wote, wapo waliomchukia, vilevile hata mume wako hapendwi na watu wote wapo watakaodurahia kifo chake.

Hata wewe hupendwi na watu wote wapo watàkao furahia kuona maiti yako dada.

Kama Yesu na Mtume Muhamad hawakupendwa na watu wote JPM yeye ni nani mpaka apendwe na watu wote?

Unayohaki ya kumtukana na kumdhihaki upendavyo lakin tunaompenda JPM tutaendelea kumpenda daima na daima.
Saa 100 yeye anspendwa
Wabadhirifu
Wenye vyeti fyeki waliolipwa na yeye
Matajir wiodhulum hii nchi
Wauza ng'anda
 
Tusizunguke mbuyu hapa. Magufuli ndiye muasisi wa haya mambo. Yeye ndio alikuwa mbaguzi #1. Tatizo hawezi kufufuka akemewe. Hao wabadhirifu aliowabana ni wepi? Inner circle ya magufuli- makonda, sabaya, Ali hapi, biswalo etc unajua ukwasi waliojikusanyia ndani ya muda mfupi?
Weka evidence ya unachokisema
 
Kwa Sababu inaonekana wanahusika Kwa kuondoka Kwa Magufuli kutoka na matamko Yao Kwa hiyo na wenyewe hawatabaki.moja alisema kabisa waliingilia wenyewe waliingilia Kati Kwa hiyo wameshajipatia laana Kwa Sababu kiongozi wa nchi anawekwa na Mungu sasa wewe binadamu unathubutu vipi kumdhuru kiongozi aliyewekwa na Mungu tena kwenye nchi ambayo Mungu anakazi nayo?laana zao zimeshaanza kuwamaliza na huu ndo mwanzo Tu.
Wale walionajisi uchaguzi wamewekwa na Mungu? Tuache dhihaka dhidi ya Mungu.
 
Wale waliokuwa wanasherekea wakati ule ilikuwa ni watu wachache mafisadi yaliyobanwa enzi za Magufuli yanafurahia Kwamba Wanaenda kupata ahueni,pia wale vyeti feki na wapenda magendo lakini hata wewe unajua watanzania wengi walilia na kuumia lakini sasa hivi watanzania wengi wanafurahi wakiona watu wa kikundi kile wamepata matatizo.yaani sio Facebook, Instagram na mitandao yote watu walifurahia hiyo juzi.
Hao wa vyeti feki ndo mama juzi amewaliPa eti walionewa khaa
 
Tusizunguke mbuyu hapa. Magufuli ndiye muasisi wa haya mambo. Yeye ndio alikuwa mbaguzi #1. Tatizo hawezi kufufuka akemewe. Hao wabadhirifu aliowabana ni wepi? Inner circle ya magufuli- makonda, sabaya, Ali hapi, biswalo etc unajua ukwasi waliojikusanyia ndani ya muda mfupi?
Weka evidence Kwamba hao wamekuwa matajiri Enzi za Magufuli weka evidence Kwamba Magufuli alikuwa mbaguzi Ili nikuelewe
 
Wacha uwongo Tindo Lisssu. Hakuna kikundi au genge lelote Tanzania linaloitwa 'Sukuma Gang' kuna Kabila la Wasukuma.

CHADEMA mnatumia siasa za kiutenganishi, (secession) yaani mavitu mnayofundishwa na mabeberu. Sasa ndio mmeng'ang'ania Majimbo ili mje muuze nchi mazima kwa Mababeru.

CHADEMA, mna mipango na mabeberu kuja kuangamiza Kabila la Wasukuma kwa sababu ya Visasi vyenu binafsi, tena visasi vya Mbowe na Lissu dhidi ya Hayati Raisi ambaye alikuwa Msukuma. Wacheni Ugaidi na Genocide dhidi ya Kabila la Wasukuma.

Nani kakuambia Magufuli alikuwa msukuma?
 
Wale walionajisi uchaguzi wamewekwa na Mungu? Tuache dhihaka dhidi ya Mungu.
Uchaguzi wa mwaka gani wapinzani hawakulalamika?kila uchaguzi wapinzani Walalamika hata enzi za kikwete.ila hauhakika kwenye urais hakuna mpinzani anaweza kupata Kura nyingi dhidi ya mgombea wa CCM.
 
Unajua hata maagizo ya Rais sikuhizi watu hawaogopi Yani hawana viongozi wenyewe hawana umoja.
Raisi inabidi akae na washauri wake tena mvuto wa saa100 aijui haupo kabisa .juzi alikuwa anahotubia sijui kufungua minara ya sim wala amna mtu mwenye habari naye
 
Wale waliokuwa wanasherekea wakati ule ilikuwa ni watu wachache mafisadi yaliyobanwa enzi za Magufuli yanafurahia Kwamba Wanaenda kupata ahueni,pia wale vyeti feki na wapenda magendo lakini hata wewe unajua watanzania wengi walilia na kuumia lakini sasa hivi watanzania wengi wanafurahi wakiona watu wa kikundi kile wamepata matatizo.yaani sio Facebook, Instagram na mitandao yote watu walifurahia hiyo juzi.
Haya ndio matamanio ya kila sukuma gang. Hamna impact hiyo. Naona umekuja kupima upepo kama kuna aliyetishika na hii mikwara mbuzi yenu. Ni hivi, dhalimu ni dhalimu tu hata mjilize vipi.
 
Weka evidence ya unachokisema
Sijajua unataka evidence ya lipi! Au unafikri magufuli anaweza kufufuka? Au evidence ya rushwa, wizi, unyang'anyi waliofanya hao jamaa? Kama hujui kusoma hata picha huoni?
 
Sijajua unataka evidence ya lipi! Au unafikri magufuli anaweza kufufuka? Au evidence ya rushwa, wizi, unyang'anyi waliofanya hao jamaa? Kama hujui kusoma hata picha huoni?
Ukisema mtu ni mwizi unatakiwa kuleta evidence mpaka Leo hamjaleta evidence kuwa Magufuli aliiba 1.5t
 
Uchaguzi wa mwaka gani wapinzani hawakulalamika?kila uchaguzi wapinzani Walalamika hata enzi za kikwete.ila hauhakika kwenye urais hakuna mpinzani anaweza kupata Kura nyingi dhidi ya mgombea wa CCM.
Kama hakuna mpinzani anaweza kumshinda mgombea wa CCM, kipi kinafanya CCM izidi kutegemea vyombo vya dola tena wazi wazi? Wapinzani wamekuwa wakilalamika wizi wa kura kabla ya dhalimu kuingia madarakani, lakini dhalimu yeye hakuiba kura, bali alipora mchakato wa uchaguzi.
 
Haya ndio matamanio ya kila sukuma gang. Hamna impact hiyo. Naona umekuja kupima upepo kama kuna aliyetishika na hii mikwara mbuzi yenu. Ni hivi, dhalimu ni dhalimu tu hata mjilize vipi.
Hakuna kitu kinaitwa sukuma gang Magufuli anapendwa kote bara na visiwani na pia nchi za nje.
 
Weka evidence Kwamba hao wamekuwa matajiri Enzi za Magufuli weka evidence Kwamba Magufuli alikuwa mbaguzi Ili nikuelewe
Ukichagua mpinzani sileti maendeleo. Tuendelee? Huo ni mfano mmoja halisi.
 
Kama hakuna mpinzani anaweza kumshinda mgombea wa CCM, kipi kinafanya CCM izidi kutegemea vyombo vya dola tena wazi wazi? Wapinzani wamekuwa wakilalamika wizi wa kura kabla ya dhalimu kuingia madarakani, lakini dhalimu yeye hakuiba kura, bali alipora mchakato wa uchaguzi.
Kwanza CCM ni chama ambacho kina wafuasi wengi kuanzia ngazi ya Chini kina wapiga Kura wengi hiyo ni Imani yenu Tu kuwa CCM inatumia vyombo vya Dola Kwa Sababu CCM wanawatu wengi Sana
 
Hakuna kitu kinaitwa sukuma gang Magufuli anapendwa kote bara na visiwani na pia nchi za nje.
Anapendwa kisha ikifika kipimo cha kupendwa anapora uchaguzi, uza ubongo huo. Angeheshimu matokeo halali ya uchaguzi tungemaliza huo uongo wa kupika kuwa anapendwa sana.

Ni kweli mliokuwa mnaompenda mlimpenda sana, lakini sio kuwa alikuwa anapendwa sana na wengi, na hiyo ndiyo sababu alipora uchaguzi ili kupata matokeo aliyokuwa anaongepea watu.
 
Back
Top Bottom