Kufutwa kwa matokeo ya Urais Kenya ndio kuwafanye wabunge wetu wa upinzani wavae suti nyeusi?

Mtanzania hata awe hajala chakula siku tatu nzima ukimuuliza 'mambo atajibu safi'.
Hivyo hivyo ukimuuuliza Ndugai 'are you OK' atakujibu 'yes'.
Nimesikia tu juzi USA wanataka kupeleka hoja bungeni ili kumpima mambo fulani fulani rais wao, unfortunate hilo haliwezekani hapa!
 
Sio kila taarifa unayoletewa mezani kwako unaweza kuisoma mbele ya bunge, nina imani kuna hoja nyingi na za msingi kabisa huwa unaletewa na kutia kapuni. Unaendesha bunge kwa misingi ya kishabiki na ubaguzi usioendana na ueledi wa majukumu yako kiongozi.

Unaelewa kabisa kua suala la Kenya liko hot hasa kwenye kanda yetu ya Maziwa makuu na dunia kwa ujumla. Taarifa uliyoletewa na mbunge kuuliza kwanini wabunge wa upande flani wamevalia suti nyeusi? Kufutwa kwa matokeo ya Urais Kenya ndio kuwafanye wabunge wetu wa upinzani wavae suti nyeusi? Wewe Kenya umeona hata mfuasi mmoja wa Jubilee amevaa nguo yeyote nyeusi?

Umeletewa taarifa iliyojaa unafki,uchonganishi na ufitini na wewe ukapoteza muda wa bunge kuisoma hivyo hivyo. Unafikiri wenzetu wa Kenya wakilisikia hili wanajisikiaje? Kumbe yaliyowatokea wenzetu 2007 kuna watu hakuguswa kabisa.


Badala ya wewe kusimama na kukemea upuuzi huu au kuitupa taarifa hiyo wewe unapoteza muda kuisoma kishabiki. Yaani mtu kama Lusinde au Msukuma akuletee taarifa kama hiyo na uisome, hivi jamii itakuchukuliaje jamani?


Tumewachokoza wakenya hasa Rais aliyekalia kiti hivi sasa, uchokozi tunawafanyia kwa kuingiza siasa zetu uchwara, baadaye muda utazungumza.
Spika dishi limeyumba

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ninavyowajua wakenya huwa hawakopeshi na wameshaanza kumjibu kwenye mitandao yao.

Taarifa yeyote inayotolewa bungeni hasa na Spika wa bunge ni taarifa rasmi, huwa inachukuliwa kwa uzito wake hasa na nchi za nje.

Taarifa aliyoisoma leo Ndugai kuhusu uchaguzi wa Kenya si tu unaingilia mambo ya ndani ya Kenya bali unaweza kuhatarisha uhusiano na majirani zetu.

Tunaweza kuchukulia jambo hili kimzaha lakini hatuwezi kujua wakenya watalipa uzito ganu na litawaathiri kwa kiwango gani.

Please, Ndugai kama siasa za majitaka tuchezeane wenyewe kwa wenyewe tusiingilie siasa za majirani zetu. Nakuumbusha kauli aliyoitoa rais mstaafu Kikwete kumshauri Kagame kuongea na mahasimu wake FDLR ilivyotu cost.

Unapokalia kiti jaribu kuchagua maneno ya kusema, usidhani timbwili la nchi na nchi ni sawa na timbwili la CCM na Chadema.

Ushauri tu hutaki unaacha.
 
Back
Top Bottom