Kufutwa kwa matokeo ya Urais Kenya ndio kuwafanye wabunge wetu wa upinzani wavae suti nyeusi?

Niliwahi kuomba humu turekebishe katiba na tubaki na mihimili miwili tu ya dola.

Hatuwezi kuwa na kikundi cha watu waliojikusanya sehemu moja na kuzitafuna sawasawa kodi za wavuja jasho wa nchi hii bila manufaa yoyote yale!

Ni aibu, pesa wanazolipwa hawa wabunge pamoja na mishahara ya wafanyakazi wote wa bunge tungeweza kuzitumia kuwapelekea maji na huduma nyingi huko vijijini.

Lile jengo tukufu linaweza kubaki kwaajili ya vitukuu wetu kama ukumbusho tu!
 
Sio kila taarifa unayoletewa mezani kwako unaweza kuisoma mbele ya bunge, nina imani kuna hoja nyingi na za msingi kabisa huwa unaletewa na kutia kapuni. Unaendesha bunge kwa misingi ya kishabiki na ubaguzi usioendana na ueledi wa majukumu yako kiongozi.

Unaelewa kabisa kua suala la Kenya liko hot hasa kwenye kanda yetu ya Maziwa makuu na dunia kwa ujumla. Taarifa uliyoletewa na mbunge kuuliza kwanini wabunge wa upande flani wamevalia suti nyeusi? Kufutwa kwa matokeo ya Urais Kenya ndio kuwafanye wabunge wetu wa upinzani wavae suti nyeusi? Wewe Kenya umeona hata mfuasi mmoja wa Jubilee amevaa nguo yeyote nyeusi?

Umeletewa taarifa iliyojaa unafki,uchonganishi na ufitini na wewe ukapoteza muda wa bunge kuisoma hivyo hivyo. Unafikiri wenzetu wa Kenya wakilisikia hili wanajisikiaje? Kumbe yaliyowatokea wenzetu 2007 kuna watu hakuguswa kabisa.


Badala ya wewe kusimama na kukemea upuuzi huu au kuitupa taarifa hiyo wewe unapoteza muda kuisoma kishabiki. Yaani mtu kama Lusinde au Msukuma akuletee taarifa kama hiyo na uisome, hivi jamii itakuchukuliaje jamani?


Tumewachokoza wakenya hasa Rais aliyekalia kiti hivi sasa, uchokozi tunawafanyia kwa kuingiza siasa zetu uchwara, baadaye muda utazungumza.
Ukiachilia mbali Ndugai kuchemsha je ni kweli wabunge wote wa upinzani wevaa suti nyeusi na kama ni kweli inaashiria nini?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tumewachokoza wakenya hasa Rais aliyekalia kiti hivi sasa, uchokozi tunawafanyia kwa kuingiza siasa zetu uchwara, baadaye muda utazungumza.
kwani vipi?ungeeleza basi kwa nini wabunge wamevaa nyeusi
 
Hata mimi nimeshangaa mno spika kufanya hicho kitendo

Kile kiti kinaanza kumpwaya
Sio kimeanza kumpwaya, Bali kinampwaya kabisa. Ni kama mtu mwenye kiuno 36 akavaa chu.i size 42, ni lazima imvuke tuu na kuacha makalio wazi.
Anatuaibisha sana huyu agwe!
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom