Mkuu Next Level,
Kuna wakati flani ubabe hutumika kwa manufaa ya wengi... Kuitisha kura kule ni kutekeleza wajibu lakini just imagine ndani ya kura yenyewe ukaingia mhadhara!
Sawa yataisha haya. Na wallahi- wanangu hamtowachagulia viongozi. Wataamua wenyewe.Mkuu Invisible,
SASA naanza kuelewa kwa nini CCM inawachagulia viongozi ndugu zetu kule Zanzibar....Lol!
Sio lazima yaletwe malalamiko wewe unajua kuwa jukwaa lile liko kinyume na mila zetu watanzania....na JF ni kioo cha jamii..wewe kama una mtoto ukimkuta kule anaangalia mapicha yale utafurahi?Mkuu Mchukia Fisadi,
Mambo ya Kikubwa sijapata lawama hata kidogo... Kama linakusumbua basi mkuu wacha nikuondoshee access haraka kabla hujakosa exit door!
Kwani wanaoshiriki jukwaa la Dini si wako hata katika majukwaa mengine nayo wanashiriki. Ama unataka sema wao walikuwa kule tu. Yani sijui itamchukua siku ngapi Invisible na timu yake kumaliza kulikarabati jukwaa lile ADHIMU, manake raha ya JF inapungua bila kutoa kuwaidhisha yaleyatokayo kwa Mola.Na sasa wameondolewa jukwaa lao watakuja kuleta tabu kwenye fora nyingine huku.
Miaka 15 imepita sasa, lirudisheni jukwaa la dini liwe public na malalamiko yote yashugulikiwe kama mnavyofanya katika majukwaa mengine yote.Wakuu,
Nasikitika kutangaza kufungwa kwa Jukwaa la Dini.
Malalamiko dhidi ya jukwaa hili yamekuwa mengi na moderators hawataweza kuvumilia kero zinazotokana na malalamiko haya.
Ukweli ni kwamba malalamiko yote yako sahihi na pia LILIKUWA NA MATATIZO ambayo dawa yake ni kulipitia upya na kuchukua hatua muhimu kwa manufaa ya wote wanaolitumia.
Izingatiwe kuwa, sheria zitazingatiwa katika kulipitia upya na lugha yoyote itakayoonekana kuwa CHAFU ama kejeli zisizo za lazima zitafutiliwa mbali na wahusika watafahamishwa.
Baada ya kulipitia jukwaa hili, litakuwa public na litakuwa chini ya uangalizi wangu na moderators wengine wawili wapya watakaotambulishwa kwenu.
Nasikitika kwa usumbufu utakaojitokeza kwa YEYOTE. Ni hatua ambayo kwa sasa haikwepeki na ni LAZIMA iwe ilivyo sasa.
Ahsanteni