Kufunguliwa kutoka katika ndoa ya mapepo au majini mahaba! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kufunguliwa kutoka katika ndoa ya mapepo au majini mahaba!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Felixonfellix, Oct 6, 2011.

 1. Felixonfellix

  Felixonfellix JF-Expert Member

  #1
  Oct 6, 2011
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 1,680
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Biblia inatuambia
  Nami nimeona lililo na uchungu kupita mauti yaani,Mwanamke ambaye moyo wake ni mtego na tanzi na mikono yake ni kama vifungo; Yeye ampendezaye mungu atamponyoka,bali mwenye dhambi atanaswa na yeye"(Mhubiri 7:26)
  Mpendwa mapepo dume na mapepo jike yapo na ni halisi.pepo mahaba dume kwa kiingereza linaitwa incubus. Pepo jike linaitwa sacubus. pepo dume linauwezo wa kulala na mwanamke kadhalika na pepo jike lina uwezo wa kulala na mwanaume katika ndoto.
  Mapepo mahaba yanatoka baharini au kwenye mito au kwenye maziwa.(wote niwatendakazi wa shetani asili yao kuzimu)kuna wanaume ambao wameoa katika hali halisi na pia wameoa katika ulimwengu wa roho.hivyo kunauwezekano wamtu kuwa na mwanamke katika halihalisi na kuwa na kuwa mwanamke katika ulimwengu wa roho.
  Solomoni anasema "Nami nimeona lililo na uchungu kupita mauti,yaani mwanamke ambaye moyo wake ni mtego na tanzi,na mikono yake nikama vifungo; yeye ampendezaye mungu atamponyoka,bali mwenye dhambi atanasw na yeye" (Mhubiri 7:26).

  Andiko hili linatuonyesha picha ya utendaji kazi wa mapepo mahaba.Na haya mapepo yapo katika jinsia zote.kwahiyo ukipenda dhambi utanaswa na ukichagua kumpendeza mungu utaponyoka.uamuzi ni wako kunaswa au kuponyoka (nimeshakupa maarifa).
  Mungu akusaidie uponyoke ndiyo sababu nimeleta kwako samo hili iliujue dalili za mapepo mahaba na ufunguliwe kutoka katika kifungo cha ndoa za mapepo mahaba.
  Pepo mahaba ni pepo awezaye kumtawala mwanaume au mwanamke katika ulimwengu wa roho, pepo huyu mchafu ana madhara mengi sana mfano kuzuia kushika mimba au kuharibu mimba,au kuzuia kuoa au kuolewa (kuvunjika uchumba/ndoa) pepo mahaba hujidhihirisha katika ndoto,kwani mtu aliyenaswa na pepo mahaba huota ndoto akifanya ngono.
   
 2. hashycool

  hashycool JF-Expert Member

  #2
  Oct 6, 2011
  Joined: Oct 2, 2010
  Messages: 5,899
  Likes Received: 442
  Trophy Points: 180
  duh....kichiiiiiina.
   
Loading...