Ikiwa unafanyaga ngono katika ndoto hutaoa wala kuolewa ama kupata mafanikio yoyote

Kambi ya Fisi

JF-Expert Member
Feb 3, 2018
13,525
22,015
Kuna watu huwa wanapendwa na mapepo (roho chafu) hadi wanafikia hatua ya kuungana kimwili na roho hizo.

Hakuna kitu duniani chenye wivu mbaya zaidi ya mume au mke wa kiroho, ukifanya mapenzi kwenye ndoto hakuna kitakachofanya kazi kimwili kwako, maana upo chini ya utawala wa roho chafu.

Mara unapofanya mapenzi katika ndoto, unakuwa umeacha damu yako ndani ya pepo kama mwanaume na kama mwanamke pepo ameiacha damu yake ndani yako.

Popote unapokwenda, umebeba pepo ndani yako ndiyo maana kila unachojaribu kufanya kinashindikana. Hutaoa wala kuolewa na mwanadamu mwenzio chini ya jua bali utakuwa chakula cha mapepo siku zote.

Maisha yako yatafadhaika hadi uulize kama kweli Mungu yupo au la.

Ikiwa unaota au umewahi kuota ndotoni unafanya ngono, tafuta msaada wa kiroho ufunguliwe kabla hujatekwa mazima.

Maombi na maombezi sio huduma za kubeza, wapo waombaji wenye nguvu za Mungu wasio wasanii watakusaidia.
 
hapana mkuu. Ugumu wa maisha yako na fikra zako finyu usitake kuwaaminisha na watu wengine. Wote tushaota ndoto nyevu kipindi cha balehe na wengine hata baada ya balehe kwaiyo wote hatuto oa wala kufanikiwa?
 
Hivi vitu sijui mapepo majini sijawahi kuviogopa, japo kwa mbali huwa nahisi wahaya washajaribu kunitupia.
Binadamu Ana uwezo mkubwa kama atajua potential yake Ana uwezo wa Kuya control hayo mapepo na mjini ukitaka kuyafukuza unaweza ukitaka kuishi nayo, kuyatumilkisha kivyovyote inawezekana.
 
Ishanitokea mara nyingi sana kipindi fulani ila siku hizi sioti tena kabisaa
sijui mpenzi wangu wa ndoto kafa🤷‍♂️.
ila ile starehe isikie tu.
 
Acha upotoshaji bana we
Hizo ni (wet dream) na zinampata yoyote aliebalehe au kuvunja ungo!

Mambo ya kusema wet dreams ni majini ni UJINGA MTUPU
ah mkuu kumbe sasa uko huru!

Nilikuwa nafuatilialia sana uzi wako kule stories of change nikikuona banned! HONGERA MKUU
 
Hauwezi ukafanya ngono na jini au na Pepo ni ngano tu hizo ila kuota kupo ila hakuna uhalisia wa pepo au jini
 
Back
Top Bottom