Kufungiwa kwenye vyombo vya habari na kufanyiwa vurugu, CHADEMA wanasaidiwa sana

Mwingereza

JF-Expert Member
Jan 21, 2014
1,111
2,752
Kama Mwana CCM, tena mbunge mstaafu anayetetea kiti chake kwa mara nyingine, napata wakati mgumu sana jimboni ninapokutana na wapiga kura na washabiki wa CCM. Inaonekana wazi kabisa kwamba tunapoteza wanachama wetu wengi mno, kitendo ambacho kitatutia aibu ifikapo kipindi cha uchaguzi. Majuzi hapa Morogoro CCM mkoa, niliwakuta wana CCM kama 7 wamekaa wanasikiliza hotuba ya Lissu aliyoitoa BUNDA kutumia simu ya mkononi. Walimalizia kwa kuweka vichwa chini, na kudai tutawajibu, ila tutajibu nini?

Moto wa Tindu Lissu umezua mijadala mizito nchini kote, na wanachama wa CCM walio wengi wanataka CCM tuwajibu CHADEMA kwa hoja, matokeo yake tunawajibu kwa hoja mfu na propaganda za hovyo. Hata mtoto wa Darasa la kwanza hawezi kukubali hoja ya kuvunjwa kwa Flyover na kuuza Vyuma kama Skrepa.

Mbaya zaidi ni kuvurugwa kwa Tasnia ya habari. Kuwanyima hawa watu nafasi ya kuonekana kwenye vyombo vya habari imewapa umaarufu mkubwa sana na huruma ya kutisha kutoka kwa wananchi, na imeonekana wazi kabisa kwamba serikali ya CCM imekuwa ikiwaonea.Kitendo hiki kimewafanya wananchi walio wengi wahache kabisa kuangalia TV na kuamia kenye mitandao ya kijamii, WhatsApp, Facebook na Instagram ambako habari za Lissu zinasambaa kwa kasi ya ajabu. Kimataifa ndio usiombe, vyombo vya kimataifa inaonyesha serikali ya CCM ilivyo Serikali ya hovyo.

Mbaya zaidi ambayo inahitaji kukemewa ni hii ya kuwafanyia hawa watani wetu wa jadi fujo. Hii ni mbaya sana. Inahitaji kukemewa kwa nguvu zote na wahusika wote wakamatwe na wafikishwe kwenye vyombo vya sheria, pamoja na polisi walioshiriki kwenye hizi vurugu. Vinginevyo dhana ya CCM kuwatumia polisi itakuwa imehalalishwa kwa maana hiyo, uchaguzi wa October utakuwa ni Raia Vs. PoliciCCM
 
Hongera umeliona hilo. Ukweli ni kuwa CCM hamshindi uchaguzi wa mwaka huu vyovyote vile. Watanzania wengi wamewakaa na sababu kuu ni udhalimu wenu!

Kwa kitendo cha jana cha Hai na Arusha , Sabaya kuongoza vijana kuchoma ofisi za Chadema Arusha na kumfanyia fujo Lissu, nilitegemea Leo Bashiru aongee ili at least CCM ijisafishe kwa umma Ila wapi!

Kweli mwaka huu CCM lazima itoke madarakani.
 
Hongera umeliona hilo. Ukweli ni kuwa CCM hamshindi uchaguzi wa mwaka huu vyovyote vile. Watanzania wengi wamewakaa na sababu kuu ni udhalimu wenu!!!

Kwa kitendo cha jana cha Hai na Arusha , Sabaya kuongoza vijana kuchoma ofisi za Chadema Arusha na kumfanyia fujo Lisse, nilitegemea Leo Bashiru aongee ili at least CCM ijisafishe kwa umma Ila wapi!!!

kweli mwaka huu CCM lazima itoke madarakani
Mkuu, mimi Mbunge tena mwandamizi. Bahati mbaya hujuma za polisi na watumishi itatunyima ushindi. Jimbo langu limekuwa CCM tangu tupaje Uhuru, ila na wasiwasi. Wananchi wana hasira na uminywaji wa habari na uonevu wa polisi.
 
Acha uzushi wewe na propaganda zako za kipumbavu. Tundu Lissu ana kitu gani alichoongea cha kumjibu so far. Yaani umekaa ukaamua ujifanye eti mwanaccm ulieguswa na Hotuba za Tundu Lissu.
 
Bora pumba. Wewe ongea cha maana tusikie
Anacho cha maana cha kuandika basi? Hayo ndio majinga tunayoyafuka humu JF mkuu.

Usemacho ndicho kinawakwaza wana CCM wengi wenye akili zao, lakini wa aina hii hilo hawalioni maana ni mavuvuzela tu
 
na imeonekana wazi kabisa kwamba serikali ya CCM imekuwa ikiwaonea. Kitendo hiki kimewafanya wananchi walio wengi waache kabisa kuangalia TV na kuhamia kwenye mitandao ya kijamii, WhatsApp, Facebook
Nakubaliana na wewe mleta mada.
 
Mkuu, mimi Mbunge tena mwandamizi. Bahati mbaya hujuma za polisi na watumishi itatunyima ushindi. Jimbo langu limekuwa CCM tangu tupaje Uhuru, ila na wasiwasi. Wananchi wana hasira na uminywaji wa habari na uonevu wa polisi.
Kabunge ka wapi wewe wacha kutuzuga hapa!
 
Back
Top Bottom