Kufunda ina maana gani?

mzenjiboy

JF-Expert Member
Aug 28, 2010
907
382
Hili neno “kufunda” huwa nalisikia kutoka tv za kibongo sio zetu za hapa Ungujani, au pia kwenye magazeti.

Maana ya neno hili kwa hapa kwetu kufunda ni kupiga kwa nguvu au kwa hasira lakini hii kufunda kwa kibongo lina maana gani ?
 
Nadhani ni kufundisha...

Hasa jinsia ya ke ndio hufundwa\kufundishwa kutunza wenza wao
 
Kumfundisha/kumuandaa (hasa jinsia ya kike) kujitambua, kujithamin na kujua nafas yake katika nyaja mbali mbali za kijamii hasa mahusiano na ndoa(hasa upande wa mahadiri)

Hiv ndivyo ninavyo jua
 
Hili neno “kufunda” huwa nalisikia kutoka tv za kibongo sio zetu za hapa Ungujani, au pia kwenye magazeti.

Maana ya neno hili kwa hapa kwetu kufunda ni kupiga kwa nguvu au kwa hasira lakini hii kufunda kwa kibongo lina maana gani ?
*Mfunde mwanao adamu!.
*mfunze mwanao adabu!.
*usipo fundwa na wazazi, dunia itakufunda!.
*Usipo funzwa na wazazi, dunia itakufunza!
 
Wote hamjui kufundwa hutumika kwa wanawali mabint waliovunja ungo wako unyagoni au vijana walio jando la kimila polini mafunzo wanaopata kule ndo inaitwa kufundwa
 
Back
Top Bottom