Mkuu wana JF wengi wanapenda ku escalate mambo,mbwa wa polisi si issue kivile kumpata ukiwa dar,anapatikana,ila tatizo ni bei zake,Germany sherpher pure pupy ana range kuanzia laki 3 hadi laki 5,hapo unaongelea mbwa wa miezi mitatu tuu,ukitaka chini ya hapo unaweza kuingizwa mjini kwa kuuziwa brand ya Iringa,ipo like GSP lakini ni feki.
Mimi ni mfugaji mzuri wa mbwa,ninao GSP watatu,ila bado hawajaaliwa kuzaa,mwana JF mwenzangu ningekuzawadia kitoto bure!nisingechukua hata senti tano kutoka kwako.
Kwa hiyo kama upo serious na hela unayo,ni PM ili nimtafuta askari mmoja hivi yupo hapo Kurasini kwenye kikosi cha mbwa na farasi ndani ya week moja kitoto kitakua kimepatakana.Ila tafadhali usianze kuzingua manake kuna jamaa nilimuunganisha na huyo afande mara akaanza kumkimbia,sie wengine hatupendagi usanii.
Kila la heri na ufugaji mkuu.