Kufuga mbwa

Kufuga mbwa

kaka na mimi nataka uniunganishe kwa huyo askari nipate female GSD puppy. niko dar.
 
Ndugu yangu LEE VAN CLEEF usiumize sana kichwa !!
Kuna aina nyingi ya mbwa ila kama unahitaji mbwa kwa ajili ya ulinzi basi nakushauri tafuta hata hii mbegu ya kienyeji,awe ni dume ,kisha unamuhashi,kama hapo unapoishi kuna bucha jirani,ongea na mtu wa buchani kila siku awe anakukusanyia ile mifupa midogo midogo kisha unamchemshia, unachanganya na chakula cha dukani kinaitwa '' DOG SPECIAL DIETY''.
Baada ya miezi kadhaa utaniambia, ila kuna dondoo kadhaa za kumtunza mbwa ili awe mkali mfano
1. Mbwa anakula mara moja tu kwa siku,mfano mimi wa kwangu ni saa mbili usiku hadi saa mbili usiku, chakula na maji ya kutosha.
2.Mbwa mwiko kuona watu ovyo yaani anatakiwa kukaa kwenye banda mda wote isipokuwa usiku tu.
3.Zingatia sana dawa kama vile za minyoo,viroboto,kupe nk pia bila kusahau chanjo ya kichaa cha mbwa !!
NB,hizi njia ni kwa mujibu wangu mwenyewe wajuzi fungukeni zaidi tuelimishane !!

Naongeza kidogo,,,,, mda mzuri wa kumpa mbwa chakula ni saa 9-10 jion, ili usiku aweze kufanya kazi yake ya ulinzi vizuri
 
Lee van cleef
Nimefurahi kusoma unataka kufuga mbwa mkali kama wa polisi.
Kwanza unahitaji kupata watu waaminifu sana wenye uelewa wa hali ya juu kuhusu hawa mbwa. Wafuatao hutumika zaidi kama police dogs..german shephard (gs). Belgian shephard (hawa wanahitaji sana umakini mkubwa wamegawanyika makundi 3) ikiwa ikiwa wataka elimu zaidi npm
 
Ogopa sana dalali wa mbwa...ni hatari kushinda hatari yenyewe..kama unataka kufuga mbwa hasa wa kigeni jifunze vya kutosha usiingizwe chaka
 
Mkuu kama unahera ya kutosha na unataka mbwa wa ukweli pure breed yoyote wasiliana na Mwimbaji mmoja anaitwa Ado November mcheki facebook,huyu jamaa huwa anaimport mbwa
 
Sema ulipo ili uambiwe uende wapi. Ukiandika, kabla hujapost soma ili uone kama swali lako likijibiwa utapata msaada sitahiki. Nikikuambia njoo hapa Namanyele kibaoni utaweza fika? Au umo kwenye kundi la wale wanaunda tume halafu ripoti ikiletwa hawakumbuka waliunda tume ya nini! Halafu ujue kuanzia leo kwamba si mbwa wote wa polisi ni wakali

Tume inaundiwa Tume.
 
Usisahau kumvutisha na bhangi, huwa nawaona vijana hapa jeshini wana fanya hivo.
 
Sawa mkuu nimekuelewa nipo Dar, na kuhusu kujua kama mbwa wote wa polisi si wakali ndo maana nimekuja humu jf ili nipate elimu.

Ngoja nikusaidie kwa hapa Dar. Ukiwa mwenge kama unaenda mliman city kuna kituo kinaitwa mpakan unaingia kama unaenda survey kwa mbele kuna ile njia kama unaenda brajec pale kiwanja cha vijana, sasa hapo hapo kabla ujafika hapo brajec utakuta mashine mbele yake utakuta geti kushoto. Ambalo
Ukiingia ndan nyumban kwa Dr mmoja anamradi mkubwa kabisa wa ufugaji wa mbwa aina zote. Mimi niliwapata wangu hapo na jins ya kuwatunza na mambo mengine mengi.
 
Mkuu huyo jamaa wa survey bado yupo? Nahitaji nkamuone mkuu
 
Back
Top Bottom