Kufika Desemba njaa itaua watu, Serikali ichukue hatua haraka

Kufika Desemba njaa itaua watu, Serikali ichukue hatua haraka

twende wote

Member
Joined
Mar 29, 2021
Posts
50
Reaction score
84
Waziri Bashe chakula ni uti wa mgongo, leo msimu wa mavuno mahindi yamefika laki na 20, na bado yanapanda, sawa achieni watu wapate pesa, lakini pesa haina maana kama kuna mfumuko, zuieni mipaka, tengeneza soko la ndani, kweli nawaambia, viongozi wangu mtakosa majibu ya wananchi, muda ni mwalimu....

Nakimbiza bawa langu, kalamu mdomoni, huyoooo!
 
Huyu jamaa alisema nchi ina akiba ya nafaka ya kutosha kwahio wakulima wauze tu mazao popote
 
Wewe mpuuzi ulikuwa wapi kupiga kelele wakulima wapewe ruzuku wakati mvua zinakatika?
 
Narudia tena kwa mara nyingine, hii ndiyo fursa pekee kwa mkulima kuuza mazao yake kwa bei nzuri ili na yeye afurahie matunda ya kazi yake. Mkulima halimi ili wewe na wenzako msife njaa bali analima ili apate chakula chake na ziada auze ili apate pesa sawa?? Ukitaka usife njaa na wewe kalume au nunua uweke stock/akiba Sawa??
 
Uko sahihi Kam mkulima kweli atauza mahindi yake kwa laki 120 sioni tatizo kila mtu akapige kazi serekali isimamie hili mamb ya kuuza gunia elf 40 kwa mkulima Ni kumdidimiza na asitoke
 
Hao unao waambia hawana habari na sisi, wao hawajui njaa mpaka wanakufa waje wakuwazie wewe. Wewe kama Mwenyezi Mungu amekufahamisha hivyo fanya kwa ajili yako na jirani zako. Usitegemee hao jamaa
 
lakini mvua mwaka huu ilikua jau sana mliopata kidogo huko mashambani tuhifadhi chakula tukiuza tukumbuke na kuweka akiba
 
Musimu wa kilimu ujao mapema tu shambani maaana nishaanza kuona cha mtema kuni, kilo ya sembe 1800 /= kweli
 
Waziri Bashe chakula ni uti wa mgongo, leo msimu wa mavuno mahindi yamefika laki na 20, na bado yanapanda, sawa achieni watu wapate pesa, lakini pesa haina maana kama kuna mfumuko, zuieni mipaka, tengeneza soko la ndani, kweli nawaambia, viongozi wangu mtakosa majibu ya wananchi, muda ni mwalimu....

Nakimbiza bawa langu, kalamu mdomoni, huyoooo!
Bei ikishuka mnalia , ikipanda mnalia. Sasa kama mtu kawekeza kwenye kilimo na ametumia pesa kulima, basi mwache apate pesa , kwanini na wewe hukulima kama uona wanapata sana?
 
Huoni kuwa hiyo ni Fursa ya wewe kuingia shamba na kulima kwa wingi, maana demand ni kubwa sababu soko limetanuka zaidi?
Kilimo siyo kama unavyokichukulia. Lazima serikali irahisishe mazingira.

Ni kwamba, mwaka jana pembejeo za kilimo hasa mbolea zilikuwa juu, hivyo wakulima wengi walishindwa kulima + mvua kuwa chache.

Kwa msimu ujao wa kilimo serikali imesema imetenga ruzuku kwa ajili ya mbolea.

Baadhi ya mikoa msimu wa kilimo upo kwenye mavuno, na mavuno ni machache!
 
Naona watu wengine hawajui ukweli, bali wanamtetea mkulima anufaike.

Ukweli ni kwamba, njaa ikitokea, wakulima wengi wa Tanzania ndio watakuwa wa kwanza kuathirika na njaa.

Ukweli ni kwamba, mazao yakienda nje, wanufaika wakubwa ni wafanyabiashara walanguzi wakubwa na madalali wa mazao kuliko huyo mkulima wa huko kijijini.

Ukweli ni kwamba, asilimia kubwa ya wakulima wa Tanzania wanalima kujikimu kama vile kutumia jembe la mkono, mfano mkulima anapata gunia tano za mahindi, hivyo akiziuza zote huyo huyo atakuja kufa njaa na familia yake.

Ukweli ni kwamba, hao madalali wa mazao siyo kwamba wanaenda vijijini kukusanya mzigo wa mazao na kutoa hela nyingi kwa wakulima. La hasha! mwendo ni ule ule wa kumdalalia bei mkulima.

Ukweli ni kwamba, hakuna mkulima Tanzania anayeendesha kilimo cha mkono na kupata gunia hata 200. Ili upate hizo gunia unahitaji mtaji wa kutosha, kitu ambacho wakulima wa huko vijijini ni maskini.

Lazima uwepo mkakati wa kuzuia utokaji wa chakula nje ya nchi, la sivyo mkulima atakuja kulalamika mwenyewe.

Wale wakulima wakubwa ambao wamelima kibiashara mfano gunia 1000 za mahindi, hao ruksa kutoa mazao yao nje.

Sasa mkulima huko kijijini amepata gunia 3 za mahindi anataka aziuze zote, huyu atakuja kuilaumu tu serikali njaa ikimkamata
 
Back
Top Bottom