Kufeli kwa Serikali kuhamia Dodoma


Taifa lenye watu million 50+ halitarajiwi kuwa na mawazo yanayofanana. Kama ambavyo wewe hujaridhika na uamuzi wa kuhamia Dodoma, wapo wengi ambao watayaona mawazo yako kuwa hayana mashiko hata kidogo.

Mjadala kama huu kwa sasa hauna tija sana. Ungekuwa na maana kama uamuzi wa kuhamia Dodoma ungekuwa haujafanyika. Subiri watafiti wafanye tathimini ya huo uamuzi miaka 30-50 baadaye.

Kushindwa au kufanikiwa kwa mambo mengi ni matokeo ya self-fulfilling prophecies. On the one hand, if you’re overly pessimistic about a given project, you aren’t likely to give it your all, thereby guaranteeing the potential project failure. On the other hand, if you’re very optimistic about the project, your actions will (most of the time) be a positive (rather than a negative) contributory factor!
 
dodoma kwa kwa kweli miaka buku hakutabadilika,mchonga meno alitangaza halafu akastuka na kupapotezea kiaina.wewe mji gani watu kutwa wanatoa tongotongo kwa ugonjwa wa macho.
Bado Dar unforgetable.
 
Bwana we DSM ndio ishapotea hivyo watu watamiminika Dodoma yaani kufikia 2025 mji uta"double" kama sio ku"triple" kabisa
Dar haiwezi potea katika historia ya nchi hii.....yaani utabaki ni mji mkuu usiotambulika...Dodoma ni makao makuu ya CCM tu
 
Mimi nahisi katika hili swala kuna kitu hamjaelewa
Dodoma ni makao makuu ya serikali hakuitajiki kuwe na vivutio vya uchumi kuna takiwa kuwe na utulivu wa hali ya juu sana
Na ndio maana Dar kuna fujo lakini ukipita maeneo ya Ikulu mda wote kupo kimya utulivu Dar haupo tena na ndio maana serikali imeamua kuhamisha makao yake

Na Dar es salaam litabaki kuwa jiji la biashara
Duniani kote majiji ya biashara huwa kuna kuwa na fujo sana kwa sababu mda wote watu wapo bize na kutafuta pesa kitu ambacho Dodoma hakitapatikana na hakihitajiki
 
Sisi tuliosoma zamani vitabu vyetu vya Geographia ilikuwa mkiichambua nchi mnaangalia mji wa makao makuu ya serikali na mji mkuu wa biashara

Dodoma ni mji mkuu wa serikali yani kutakuwa kunapatikana Ikulu ,mawizara na maofisi mengine muhimu ya serikali

Dar es salaam ni jiji la biashara kuna bandari kuu na international airport
Na makampuni kibao

Sasa nyi vijana sijui mnafeli wapi mnataka mji wa makao makuu ya serikali uwe sawa na mji mkuu wa biashara yani ina maana hamjui tofauti na tabia za miji ya aina hii kweli kiwango cha elimu Tanzania kimeshuka
 
Mkuu unajua kuwa unajiabisha sana? Au hujui
 
Pumba tupu hujui kujenga hoja watu walifocus usalama zaidi afu watu wa Dar ni tabu tupu ukiwa Dar ni full foleni full stress makazi duni joto Kali shida tupu
Usalama wa nn mkuu dunia ya leo ni utandawazi ina maana mji ukiwa kando ya bahari sio salama nikuafahamishe tu dodoma ilianza kuwa makao makuu toka 1973 mpaka sasa hakuna cha maana zaidi ya siasa uchwara tu
Kama serikali ilikua na nia ya dhati 1973 mpaka leo 2019 dodoma ingekuwa mbali lakini kinachotekea sasa ni kupoteza hela kwa kitu ambacho kilisha shindikana kuwa best city
Ref. Dar salaam city
Younde capital city
Bamako capita city na miji mingine mingi tu ipo mbali
 
Makao makuu ya miji kibao mkuu imechangamka sana sisi miaka yote tulikuwa wapi na kwann ijengwe kwa haraka haraka kwa miaka mitatu ya ujenzi tu haitaifanya ichangamke
 
Nyerere kufanya Dodoma kuwa mji mkuu naungana nae miaka mia saba.Alikuwa na uwezo uwe kwao Mara lakini Kwa sababu alikuwa na maslahi ya Tanzania kwanza yeye baadae akachagua Dodoma Kwa vigezo vingi vya kisayansi.
 
Makao makuu ya miji kibao mkuu imechangamka sana sisi miaka yote tulikuwa wapi na kwann ijengwe kwa haraka haraka kwa miaka mitatu ya ujenzi tu haitaifanya ichangamke
Dar es salaam ilipewa majukumu yote kama makao makuu ya serikali pia ni kama jiji la biashara lakini sasa Dar imesha jaa sana hivyo hakuna namna lazima serikali irudi Dodoma

Kuhusu kuchangamka kwa Dom sio lazima na ndio maana hata eneo la Ikulu Dar hadi Leo hakuja changamka cha muhimu kuwe na miundo mbinu ya kutosha

Ukitaka kuwa muajiliwa wa serikali kaa Dodoma na ukitaka kuwa mfanya biashara kama Manji kaa Dar es salaam
 
MARA MIA MJI UNGEJENGWA MOROGORO KWA KUIKATA KATIKATI UKATENGENGWA MKOA MMOJA UKAITWA MAKAO MAKUU
KWASABABU NI KARIBU NA DAR ES SALAAM
Mkuu unajua sababu ya kupeleka makao makuu Dodoma?
Eti unasema ingekuwa Morogoro sababu karibu na Dar es Salaam!!!

Makao makuu yalipendekezwa yawe Dodoma sababu ni katikati kutoka mikoa yote, inakuwa rahisi wote kufika makao makuu kufuata huduma flani hasa ofisi za umma. Hii ndiyo sababu pamoja na sababu zingine zitafute mwenyewe.
 
JAMAA ITAKUWA NI MTUMISHI WA UMMA HUYU,WATUMISHI WA UMA SIJUI WAMEINGILIWA NA MDUDU GANI VICHWANI MWAO YANI UWEZO WA KUFIKIRI NA KUCHANGANUA MAMBO UMEKUWA TATIZO KWAO,NA NDIO MAANA AWAMU HII HAWANA NAFASI KABISAMWALISHAONEKANA NI MZIGO
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…