Kufeli kwa Serikali kuhamia Dodoma

Mkuu hapo hakuna link ya information zako na kukosewa kwa Dodoma kuwa makao makuu
 
Mkuu hapo hakuna link ya information zako na kukosewa kwa Dodoma kuwa makao makuu

Picha hapo juu ni mji mkuu wa tanzania dodoma kwa haraka haraka ukiitafsiri hiyo picha ni eneo ambalo kwa muda picha ilivyopigwa ina onyesha hakuna kivutio cha kiuchumi hapo



Hili ni jiji la kampala ya uganda jiji cairo
nadhani kwa picha umeshanielewa
 
Wee jamaa hoja yako Dhaifu sana, kwa hiyo ulitaka mji uandaliwe kwanza ndo serikali ihamie?
 
Kupanga ni Kuchagua,hata Dar eS Salaam kuna watu walipanga iwe hivyo ilivyo leo na ikawa haijatokea tu from no where ikawa hivyo ilivyo.

Unaweza sema sababu ya bahari ndio inaibeba Dar kumbuka Lindi,Mtwara na Tanga pia bahari ipo ila miji hiyo haiko kama Dar so issue ya bahari sio kigezo kikuu kilichoibeba Dar kuwa ilivyo leo.

Kama tumeamua kuifanya Dodoma kuwa Mji mkuu wa kiserikali na kuipa hadhi ya Jiji kwa malengo ya kusogeza huduma kiurahisi ktk mikoa mingine basi tusirudi nyuma kwa sababu Dodoma pia ni sehem ya Tanzania inayohitaji maendeleo kama ilivyo Dar na kwingineko.

Suala la Ukame,sijui Jangwa hizo hazina tija hakuna sehem ambayo hakuna changamoto ktk Nchi yetu kila sehem ina changamoto zake.kukimbia changomoto zilizopo ndani ya Nchi yetu ni kudhihirisha Uwezo wetu mdogo wa Kifikra ktk kupambana na mazingira yanayotuzunguka.

Dubai,Tripoli na kwingineko kwenye hali ya Ukame wangekuwa na mawazo mepesi na laini kama haya ya kusingizia Ukame pengine hata sisi tusingekimbilia huko kupiga picha na video kwa wasanii wetu bali walipambana na kuzishinda..

Hakuna kinachokuja kirahisi bila kuvuja jasho,kukimbilia sehem rahisi zisizo na changamoto huo ni Uvivu wa kufikiri na kutotaka kuitumia akili tuliyopewa na MwenyeziMungu.

Istoshe hata Dodoma pia wanataka iwe kama Dar so tutamwachia nani aje aibadilishe kama sio sisi wenyewe?embu tuache wivu wa kike tuiache serikali ifanye kazi yake...








Mungu Ibariki Tanzania[emoji1241][emoji1241][emoji1241]
Mungu Ibariki Chakwale
Mungu Ibariki Gairo
 
Wee jamaa hoja yako Dhaifu sana, kwa hiyo ulitaka mji uandaliwe kwanza ndo serikali ihamie?
Sio kuandaliwa mkuu kimazingira kuufanya uwe mji wa kisasa unahitaji gharama kubwa sana mkuu elewa
 
Ni jambo zuri Kwa Mji Mkuu DODOMA lakini kila jambo lazima lipewe nafasi yake ya kipekee, Kupeleka mji dodoma hakuihitaji pesa tu bali Muda, na nafasi pia. Dar es salaam ina kila namna ya nyingi ya kuelezea kuwa Bado utadumu kuwa mji mkubwa kwa kipindi kirefu tu bila strategies nzuri ni sawa na kuforce Maji yapande mlima Kupeleka peleka tu mji haraka haraka tu ilimradi tu ionekane umefanya wewe still it doesnt explain any essence
 
Mmh!Tetemeko?Lini na ilikuwaje?Linaathiri maghorofa ya ukubwa gani?Yaliyopo kwa nini hayawahi kuathirika?
Asee bwana mdogo hama kwa wazazi,waache wao wakaishi walikohamishiwa na serikali
Mafuriko ya jangwani tu serikali wameshindwa kutafuta engineering solution [emoji23][emoji1] waneenda dodoma kwenye matetemeko. Hizo gharama za kukarabati nyufa za majengo endapo kuna matetemeko sijui zipo au ndio siasa tu
 
Wewe ni mmoja wa wasomi ambao ni kama kirusi ambao mmekuwa chanzo cha kutotoa maamuzi.Kila kitu urasimu,michakato,upembuzi yakinifu,na ujinga mwingine kama huo ambao kwa kuuendekeza,nchi hii imechelewa dana kupiga hatua.
Mtu kama Lowasa aliamua mradi wa maji ziwa Victoria kwenda shy na kahama kwa sababu ya uthubutu.Kama anavyofanya Rais Magufuli na sio kusubiri ushauri kama wako kutokana na elimu ya madesa
 
Pumba tupu hujui kujenga hoja watu walifocus usalama zaidi afu watu wa Dar ni tabu tupu ukiwa Dar ni full foleni full stress makazi duni joto Kali shida tupu
 
Kama hupendi kwa sasa hayo ndiyo maamuzi. Period.
 
Ni fikra jangwa sana na ubinafsi kuona dodoma hapafai kuwa mji mkuu kiserikali. Mimi simfuasi wa vyama lakini kuweka mji eneo lile kwanza litafanya mji ukue ambapo litagusa sekta zote kiuchumi, afya na mengineyo. Litapunguza kwa hali ya juu ile hali ya kudumaa kimaendeleo kwa mji ule, wasomi uwezo wao unatia shaka sana maana kimaono kweli unaona kwasababu DSM tayari ni jiji basi hapohapo ndio mji mkuu wa kiserikali uwepo. Fikra z kimskini ni pale mtu unapotoa maoni kuwa nchi fulanifulani wameweza kuendeleza miji yao ya kiserikali iliyo kwenye jiografia tata kwasababu wanahela za kutosha...kwahiyo katika akili ya usomi mtu huyu anaona aisi watanzania hatutaweza kuendelea kiuchumi kufanya hayo yaliyofanywa ughaibuni...ni mawazo kujiona duni na kujiona hakuna namna. Kunahaja ya kubadilika kifikra...
 
ni mara yangu ya kwanza kukaa ddm angalau kwa wiki mbili sasa, ukweli bado safari ni ndefu sana sana kuifikisha ddm kwenye hadhi ya jiji, ddm bado mno
Ulichokiona wewe hata mimi numekiona tena kwa jicho kali sana MIJI YA KALE ILIKUA MAARUFU KWA BIASHARA MPAKA IKAJENGEKA NA KUWA MIJI MIKUBWA HOJA YA KUJENGA KAMA SERIKALI YETU INAVYOFANYA NI KAMARI MBAYA SANA TUSIJE KUWA NA MAGOFU BAADAE
 
Mkuu umeongea point sana kwakweli TUACHE KUKURUPUKA KISIASA TUWEKE MIPANGO YA MUDA MREFU TENA TUKIWA NA SABABU ZA KIUCHUMI

Huu ni mji wa dubai uwekezaji wake na muda waliotumia si sawa na serikali kuingia madarakani na kuanza kuwekeza katika kipindi cha miaka mitatu tu dodoma imekua jiji na unataka kushindana kimapato na majiji mengi ni kudanganya tu wakuu ina hitaji muda na fedha za kutosha kuwekeza na sio siasa za majukwaani
 
Sio lazima tufanane au tufanye kama wanavyofanya wao! Acha tufanye yetu na ndo tumeshahamia Dom hakuna kurudi nyuma
 
Dodoma ndo ishakuwa makao makuu ndugu hakuna namna
 
Hoja zako ni za kifala sana, yaani nilijua unashusha madini kumbe uharo tuu. Nenda kaone jiji linavyokua tena ni la kisasa. Nchi hii mikoa mingapi haina ukame? Hata hiyo yenye mvua imejaa milima tuu ovyo ovyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…