Kufariki na Kufariki Dunia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kufariki na Kufariki Dunia

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by Makoye Matale, Jun 19, 2011.

 1. Makoye Matale

  Makoye Matale JF-Expert Member

  #1
  Jun 19, 2011
  Joined: May 2, 2011
  Messages: 6,480
  Likes Received: 450
  Trophy Points: 180
  Wana JF nawasalimu sana katika Jina la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Baada ya salamu hizo leo nimekuja na kamada kadogo kabisa katika hili jukwaa la lugha.

  Watu wengi wamekuwa na maswali mengi, mtu anapokufa wasemeje; wengine wamekuwa wakisema 'amefariki', wengine wanasema 'amefariki dunia', kwa kuangalia makundi haya baadhi ya watu wameshindwa kufahamu hasa ni kundi lipi liko sahihi.

  Nimefuatilia na kugundua kuwa: Neno 'kufariki' chanzo chake siyo 'kufa' bali ni 'faraka' yaani kuachana na ...; mfano marafiki wawili waliopendana wakaamua kuvunja urafiki basi huitwa 'wamefarakana' yaani wameachana! Hivyo basi mtu anapoishi duniani anakuwa ameambatana na dunia, pale mtu huyo anapoachana na dunia basi anakuwa 'amefarakana' na hiyo dunia au ametengana na hiyo dunia hivyo ni sahihi kusema 'amefariki dunia' na siyo kuishia tu kwamba 'amefariki' ambapo huacha swali kwamba 'kafariki nini'?

  Kwa upande mwingine neno 'kufariki' linaweza kutumiwa kwa mtazamo huu: Mtu ambaye ameishi Dar es Salaam na sasa ameuhama Dar es Salaam anaenda mji mwingine; atakapokuwa ameuhama Dar es Salaam haitakuwa makosa kusema mtu huyo 'amefariki Dar es Salaam'.
   
 2. Nanren

  Nanren JF-Expert Member

  #2
  Jun 19, 2011
  Joined: May 11, 2009
  Messages: 1,739
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160


  Hiyo ina furahisha. Mtu anahama Tanzania, unasema amefariki Tanzania.

  Ila sasa tukirudi kwenye kufariki dunia, Je neno dunia maana yake nini?
  Ni pamoja na huu udongo kwenye ardhi tunamoishi?
  Kama ndivyo, mtu akizikwa humu humu duniani, basi hajafariki dunia. Kwa sababu bado yupo duniani.

   
 3. N

  Nyamanoro JF-Expert Member

  #3
  Jun 22, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 577
  Likes Received: 237
  Trophy Points: 60

  Ukizikwa ndugu yangu bado unakuwa umefariki dunia,kwani maisha duniani hutakuwa nayo tena, hakuna maisha chini ya ardhi ( kwa sisi wenye imani ya dini). Kwa hiyo kufariki ni kuondoka sehemu unayoishi kwenda sehemu nyingine,lakini kufariki dunia ni kukosa uhai.
   
 4. Nanren

  Nanren JF-Expert Member

  #4
  Jun 22, 2011
  Joined: May 11, 2009
  Messages: 1,739
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Asante bwana Nyamanoro.
  Hapo kwenye blue, ina maana kwa sisi tuanoamini mizimu, na kuamini kuwa ukizikwa bado unakuwepo hai kwa namna fulani, basi sisi HATUFARIKI DUNIA, hii ni kwa mujibu wa imani yangu..
   
 5. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #5
  Jun 22, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Hata kwa imani yako ukifa utakuwa umeifariki dunia...! Hiyo imani ya kusema kuwa mizimu huja duniani kutembelea jamaa si kweli, ila watu huwa wanakwenda aidha makaburini au kwenye mapango, au kwenye miti mikuwa ambapo wana amini kuwa hapo ndipo mizimu ipo, yaani ni sawa na kwenda kibanda cha simu na kuwasiliana na mtu aliye upande wa piili wa dunia.
   
 6. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #6
  Jun 22, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,336
  Likes Received: 22,188
  Trophy Points: 280
  Bukibuji amegariki kitanda......Means Bujibuji kakiacha kitanda chake na kuingia kwenye purukushani, Kiswahilii bwana iz vele entelestingi langweji
   
 7. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #7
  Jun 22, 2011
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,584
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Japo kusema "kufariki dunia" ndio sahihi, lakini matumizi ya muda mrefu na ya watu wengi ya "kufariki" yamekwishajihalalisha.

  Hivyo kihalisia Kufa = Kufariki dunia = kufariki.
   
 8. Nanren

  Nanren JF-Expert Member

  #8
  Jun 22, 2011
  Joined: May 11, 2009
  Messages: 1,739
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Mkuu ekspata, mbona unatoa tafsiri tofauti ya imani yangu?
  Mimi naamini mtu ukifa roho yako bado ipo hai, na unaendelea kuwepo hapa duniani. Si lazima iwe pale ulipozikwa, hata nyumbani ulipokuwa unaishi, unaendelea kuwepo tu. Ila unakuwa free zaidi kwenye movement.
   
 9. N

  Nyamanoro JF-Expert Member

  #9
  Jun 22, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 577
  Likes Received: 237
  Trophy Points: 60

  Kumbe nyie mnaoamini mizimu dunia yenu iko chini ya ardhi?
   
 10. Nanren

  Nanren JF-Expert Member

  #10
  Jun 22, 2011
  Joined: May 11, 2009
  Messages: 1,739
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Dunia ni nini na ardhi ni nini? unaweza kutenganisha ardhi kutoka kwenye dunia? Kwa mtazamo wangu ni hapana. Kwa hiyo hata nikizikwa ardhini, ninakuwa bado nipo duniani.
   
 11. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #11
  Jun 22, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Mkuu, unakuwa kwenye dunia nyingine kabisa, si hii tena.
   
 12. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #12
  Jun 27, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Upo sahihi mkuu ila hapo kwenye red hawezi kuwa amefariki Dar es Salaam hadi ithibitike kuwa mtu huyo hatarudi Dar es Salaam kamwe. Kwa maelezo zaidi ni kuwa "Kufariki eneo fulani" ni kuhama eneo hilo na kwenda eneo lingine pasipo kurudi kamwe eneo la awali.
   
 13. Makoye Matale

  Makoye Matale JF-Expert Member

  #13
  Jun 28, 2011
  Joined: May 2, 2011
  Messages: 6,480
  Likes Received: 450
  Trophy Points: 180
  Hii ni 'common mistake'.
   
 14. Averos

  Averos JF-Expert Member

  #14
  Jun 28, 2011
  Joined: Aug 6, 2010
  Messages: 648
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 45
  Kazi ipo!
   
 15. fxb

  fxb Senior Member

  #15
  Jun 30, 2011
  Joined: Jun 22, 2011
  Messages: 124
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Nadhani kufariki kunatokea hapa DUNIANI kwa hivyo nionavyo mimi kusema kufariki yatosha.
  Mfano nitakaokupigia ni Kukoga na kukuga maji (Kwa kawaida binadamu wote ninaowafahamu huwa wanatumia maji katika kutimiza adhma yao ya kujiswafisha mwili mzima....kukoga ni sahihi).
  Kuna mtaalamu wa totologi aweza akatoa mwnga zaidi
   
 16. Manumbu

  Manumbu JF-Expert Member

  #16
  Jul 1, 2011
  Joined: Oct 28, 2009
  Messages: 1,751
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  nafahamu sote sisi tulihama toka matumboni mwa mama zetu, na hatutorudi tena huko. kwa tafsiri hii manake, badala ya kutumia kuzaliwa tunaweza sema mtoto amefariki toka tumboni kwa mama yake na sote tukaelewa kuwa amezaliwa?
   
 17. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #17
  Jul 4, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Hiyo ni sawa tu. Unaweza ukatumia tungo hasi kuelezea hali chanya. Mfano mtu mmoja akisema: "Mkeshaji hana roho mbaya" na mwingine akasema "Mkeshaji ana roho nzuri", hawa wote watakuwa wamezungumza kitu kimoja kwa kutumia maneno tofauti; mmoja ametumia sentensi hasi na mwingine ametumia sentensi chanya.
  Mfano mwingine ni ule wa haki na wajibu. Haki ya mtu mmoja huwa ni wajibu wa mtu mwingine, na wajibu wa mtu huyu huwa ni haki ya mtu mwingine. Ni kitu kimoja chenye maana moja kwa pande mbili tofauti.

  Unapofariki eneo moja ni kuwa unazaliwa eneo jingine. Mtu anayefariki tumboni mwa mama yake ni kuwa anazaliwa duniani (endapo tu atoka akiwa hai), vinginevyo atakuwa amefariki tumboni mwa mama yake na atakuwa amefariki dunia vilevile.
   
 18. Manumbu

  Manumbu JF-Expert Member

  #18
  Jul 6, 2011
  Joined: Oct 28, 2009
  Messages: 1,751
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Mkuu kwa hiyo ni sawa nikisema mwanangu amefariki toka tumboni kwa mama yake salama? hapo ntaeleweka kuwa mwanangu kazaliwa akiwa hai na afya njema? nadhani sikubaliani sana na maana hiyo, hata kama ni maana hasi. sidhani kama hata ntaeleweka. nadhani ntaonekana chizi au namchulia mwanangu kifo
   
Loading...