Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,489
- 40,018
2008-10-16 13:40:56
Na Mary Edward Dodoma
Mwedesha Mashitaka katika kesi ya Deus Mallya, Mrakibu wa Polisi, William Maganga, amefariki dunia gafla wakati akiwa katika harakati ya kuifanyia uchunguzi barua ya dhamana ya Mallya, iliyokuwa na kasoro kadhaa.
Akizungumzia tukio hilo, askari polisi mmoja ambaye hakutaka jina lake litajwe alisema Oktoba 7 mwaka huu, Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya,Thomas Simba, alimtaka mwendesha mashitaka huyo kuichunguza barua ya dhamana iliyoletwa makahamani hapo na Julius Michael kwa lengo la kumwekea dhamana Mallya.
Uchunguzi huo ulitokana na dosari kadhaa zilizojitokeza kwenye barua hiyo, ikiwemo kukosewa kwa jina la mtuhumiwa lililoandikwa Dinis Maliwa badala ya Deus Mallya na pia mhuri uliogongwa kwenye barua hiyo haukusomeka vizuri.
Kutokana na kasoro hizo, hakimu huyo alitilia shaka barua hiyo na kumtaka mwendesha mashitaka, Maganga kuichunguza kwa makini barua hiyo na kesi hiyo kusogezwa mbele hadi Oktoba 13 mwaka huu, ambapo mwendesha mashitaka huyo alitakiwa kutoa taarifa za uchunguzi wa barua hiyo.
Kwa mujibu wa askari huyo, marehemu Maganga alipatwa na kiharusi ghafla siku hiyo hiyo aliyoahidi kuichunguza barua hiyo na kufariki dunia Oktoba 13 siku ambayo alitakiwa kutoa mahakamani taarifa ya uchunguzi wa barua hiyo.
Kutokana na kifo hicho, kumeibuka maneno mengi toka kwa baadhi ya watu, wakikihusisha kifo hicho na imani za kishirikina.
Lakini mmoja wa wanafamilia ya Marehemu Maganga alipoulizwa kuhusiana na tetesi hizo, alikataa na kusema sababu ya kifo chake ni kiharusi.
Hata hivyo, akiongea kwa sharti la kutotajwa jina lake, alikiri kwamba kuna tabia ya baadhi ya watu kunapotokea kifo, kuwa na maoni yao, hususan watu wanaoamini ushirikina.
Hatma ya kesi hiyo ya Mallya aliyeshtakiwa kwa kosa la kuendesha gari kwa mwendo wa kasi na kusababisha kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Tarime kwa tiketi ya Chadema, Marehemu Chacha Wangwe, itajulikana Oktoba 27 mwaka huu.
Hatua hiyo imekuja baada ya Mwendesha Mashitaka, Mrakibu wa Polisi anayeendesha kesi hiyo kwa sasa, Porcup Urio, kumwomba hakimu anayesikiliza kesi hiyo, kuipangia tarehe nyingine kwa madai kuwa, kumekosekana maelezo ya mtu mmoja wa upande wa mashtaka, ambaye anadaiwa kuwepo safarini.
Kutokana na maelezo hayo, Hakimu Simba alimtaka mwendesha mashtaka kukamilisha taratibu zote ili kesi hiyo ianze kusikilizwa mara moja katika tarehe iliyotajwa, vinginevyo mahakama itachukua maamuzi mengine.
My Take:
Well, what can I say. Mauti ndiyo hayo tena. Na hii kesi sidhani kama itafika mahali, kwani the next ni barua kutoweka na yule jamaa aliyejaribu kumpa dhamana Mallya kutokuonekana. Je, Mallya naye atapatwa na ugonjwa wa ghafla na hivyo kesi nayo kuisha? I'll give you 80 percent hii kesi haiendi popote.