Kufa ni kufanya nini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kufa ni kufanya nini?

Discussion in 'Jamii Intelligence' started by Iron Lady, Aug 27, 2012.

 1. Iron Lady

  Iron Lady JF-Expert Member

  #1
  Aug 27, 2012
  Joined: Mar 4, 2008
  Messages: 4,077
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Naomba kuelimishwa juu ya hiki kitu kufa.

  Tukisema mtu kafa kinachokufa ni nini? Je, kutopumua ni kufa? Brain kutofanya kazi ni kufa? Mapigo ya moyo yakiacha kufanya kazi ndio kufa au roho kutoka ndio kufa?

  Napata shida mno nisaidieni maana naanza kuhisi watu wanaweza kuwa wanazikwa wazima.
   
 2. C

  Chesty JF-Expert Member

  #2
  Aug 28, 2012
  Joined: Aug 30, 2009
  Messages: 2,353
  Likes Received: 424
  Trophy Points: 180
  Mwanadamu is made up of three major parts, Body, Soul au nafsi ambayo inafanywa na vitu vitatu (Intellect, Free will na Emotions), halafu cha tatu ni spirit.

  Elewa kuanzia leo kuwa spirit ni kipande kinachotokana na pumzi ya Mungu (angalia uumbaji wa mwanadamu) na kimsingi ndio mtu mwenyewe. Kwa maneno mengine ni kuwa binadamu ni roho, ana nafsi na anaishi kwenye nyumba inaitwa mwili.

  Mtu sio mwili, na ndio maana tunasema mwili wa marehemu, maana yake ni kuwa mwenyewe hayupo mwenye huo mwili.
  Biblia inathibitisha kuwa roho ndio mtu mwenyewe, Ufunuo 20:15 inasema kama jina la mtu halijaonekana kwenye kitabu cha uzima atatupwa kwenye ziwa la moto.

  Siku ya hukumu hatutakuwa na miili yetu hii ya nyama, tutakuwa na miili ya rohoni. Ndio maana mtu akiitwa Fatuma ni roho yake ndio inaitwa Fatuma.

  Baada ya hapo sasa kifo simply ni roho ya mtu ambayo ndio mtu mwenyewe anaondoka kwenye nyumba yake na kuacha pagala ambalo ni mwili. Mara nyingi anaiacha nyumba yake inapokuwa na matatizo either inavuja (magonjwa, nk). Mtu anapokufa hawezi kusema amekufa, yeye anajiona ameondoka tu na yupo sehemu nyingine.

  Hii term ya kufa tunaijua sisi wanadamu lakini yule aliyekufa anajiona amechukuliwa na malaika au mashetani kulingana na jinsi alivyokuwa anaishi hapa duniani. Na ndio hapo eternity inapoanza...

  Hili ni somo pana kidogo, mara nyingi Yesu alikuwa hatumii term kufa alikuwa anasema amelala na inabidi aamshwe, kwa Mungu kufa ni eternal separation kati ya Mungu na mwanadamu kwa kutupwa kwenye ziwa na moto au jehanum.

  Sasa kwa fact hiyo ndio maana Yesu alipofika kwenye kaburi la Lazaro aliita LAZARO NJOO!!! alifanya hivyo kwa sababu anajua kuwa Lazaro sio ule mwili, ila yupo somewhere na anaweza kuisikia sauti ya Yesu na kurudi kwenye nyumba (mwili) yake, na ndivyo ilivyokuwa.
   
 3. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #3
  Aug 28, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  KUFA NI KUFA...

  POSSIBILITY YA WATU KUZIKWA wazima ipo saana
  hasa huku kwetu Africa
   
 4. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #4
  Aug 28, 2012
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Kufa ni process. Ni kama kuzimika kwa kibatari ambacho mafuta yake yamekwisha. Mwanga unaanza kupungua kidogo-kidogo na mwishowe mwanga unazimika. Vivyo hivyo kufa kunaanza hatua kwa hatua: kukosa pumzi, mapigo ya moyo yanasimama, ubongo unaacha kufanya kazi, nk mwishowe inakuwa si kiumbe hai tena bali kifu kwani yale yote yanayompa mtu uhai yanakuwa hayafanyi kazi tena au yamesambatika.
   
 5. Iron Lady

  Iron Lady JF-Expert Member

  #5
  Aug 28, 2012
  Joined: Mar 4, 2008
  Messages: 4,077
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  kama kufa ni pale roho ya mtu inapoondoka kwa maana ya mtu huyo ndio anaondoka na kuuacha mwili, sasa yule anayekuja kusema huyu mtu sasa kafa nakuwa anangalia nini vitakavyomuashiria huyu mtu sasa kafa? je kutopumua(pumzi)pekee isipokuwapo mtu kafa? na anastahili kuzikwa?
   
 6. Mess

  Mess JF-Expert Member

  #6
  Aug 28, 2012
  Joined: Mar 2, 2009
  Messages: 667
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kufa ni brain kuacha kufanya kazi
   
 7. Iron Lady

  Iron Lady JF-Expert Member

  #7
  Aug 28, 2012
  Joined: Mar 4, 2008
  Messages: 4,077
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  maana daktari mmoja alikuwa akieleza swala zima la kufa nikaogopa kidogo maana alisema asilimia 60 ya watu wanaowapima watu na kukamilisha kuwa wamekufa huwa wanakosea kwani mtu anaweza zimia hata kwa siku 3 na bado akawa hajafa akaenda kufia kaburini kwa kukosa hewa na joto na vitu vingine.
   
 8. Iron Lady

  Iron Lady JF-Expert Member

  #8
  Aug 28, 2012
  Joined: Mar 4, 2008
  Messages: 4,077
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  wale wanaokuwa ICU wankuwa katika hali gani "Unconscious"? na ukiwa katika hali hii unakuwaje? je unapumua ila huwezi kujisogeza au hata brain haifanyi au nini?
   
 9. Iron Lady

  Iron Lady JF-Expert Member

  #9
  Aug 28, 2012
  Joined: Mar 4, 2008
  Messages: 4,077
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  je brain haiwezi kuacha kufanya kazi kwa muda halafu ikarudi ktk hali yake ya kawaida?
   
 10. Iron Lady

  Iron Lady JF-Expert Member

  #10
  Aug 28, 2012
  Joined: Mar 4, 2008
  Messages: 4,077
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  ningependa sasa kujua hivyo viashiria ambavyo madokta wanatumia kusema huyu sasa kafa.
   
 11. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #11
  Aug 28, 2012
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  In fact kwakuwa kufa ni process, kuna ugumu wa ku-establish muda halisi wa mtu kufa. madaktari wanadai mtu anakuwa amekufa pale ubongo wake unapokoma kufanya kazi (brain death). Lakini nyanja nyingine za elimu kwa mfano watu wa dini wanadai ni pale roho inapotengana na mwili. Lakini swali linabaki: ni wakati gani mwili unakuwa umetengana na na roho? Hapo panahitaji alama za kuonekana na kuonesha kwamba mwili na roho vimetengana. Kwa hiyo wataangalia kama mwili umepoa (umekuwa wa baridi), moyo haupigi tena, nk. Lakini yote haya siyo uthibitisho usio na shaka kwamba mtu amekufa, ndo maana kuna wakati watu wanazikwa wakiwa hai.
   
 12. N

  Nonda JF-Expert Member

  #12
  Aug 28, 2012
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,960
  Trophy Points: 280
  Unaikumbuka hii?

  The Bolton midfielder was "in effect dead" for 78 minutes after suffering a cardiac arrest during his club's FA Cup tie with Tottenham.

  BBC Sport - Fabrice Muamba: Doctors re-live race to save Bolton midfielder

  Halafu jamaa kafufuka tena, mwone hapa BBC News - Fabrice Muamba: Medics are my 'heroes'
   
 13. Mess

  Mess JF-Expert Member

  #13
  Aug 28, 2012
  Joined: Mar 2, 2009
  Messages: 667
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Inaweza, ila ikiacha kwa muda fulani kitaalam haiwezi tena fanya kazi
   
 14. Watu8

  Watu8 JF-Expert Member

  #14
  Aug 28, 2012
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 47,350
  Likes Received: 2,688
  Trophy Points: 280
  Pindi moyo unaposima akusafirisha damu mwilini, mtu husemekana amekufa.
  Ndio kwa njia rahisi watu hupima pulse "mapigo ya moyo" katika mshipa wa shingoni au wakati mwengine karibu na kiganja cha mkono.
   
 15. C

  Chesty JF-Expert Member

  #15
  Aug 28, 2012
  Joined: Aug 30, 2009
  Messages: 2,353
  Likes Received: 424
  Trophy Points: 180
  Madaktari huwa wanaangalia vitu kadhaa kuthibitisha kuwa mtu amekufa:

  1. Mapigo ya moyo
  2. Eye movements
  3. Mishipa ya damu
  4. Joto la mtu, n.k

  Kwa sababu definition ya wanadamu ya kufa ndio hiyo basi ni kweli kuwa mtu anaweza kuwa booked for mortuary pindi hivyo vitu vinapobehave namna hivyo.

  Kwa hiyo basi shetani anatumia mbinu hii kuchukua watu. Anafanyaje, mtu ni roho na shetani ni roho, so anaweza kuingia kwenye nyumba yake (mwili) na kumkaba mtu wa ndani ambaye ni roho. Kitakachotokea ni kuwa mwili wa yule mtu utaacha kabisa kuperform activity zake.

  Akipelekwa hospital daktari atathibitisha kuwa amekufa na hivyo kupelekwa mortuary. Sehemu nyingine wana taratibu za kumzika mtu siku hiyo hiyo. Nini kinatokea baada ya hapo, aweza kuja kufukuliwa usiku na kuamshwa na wachawi akapuliziwa dawa akaanza kufanya kazi kwenye duka la mtu, kiwandani kwa mtu, nk.

  Watu wanaishi hapa mjini kwa namna hizo. Haya maarisha yamekuwa rampant sana among the Bible believing christians na wengi wamekuwa wakirudishwa kwa kumuomba Mungu.
   
 16. T

  Tiger JF-Expert Member

  #16
  Aug 28, 2012
  Joined: Nov 30, 2007
  Messages: 1,750
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Ninavyofahamu, mwanadamu ni muunganiko wa body, mind & soul.
  Hivi vitu vitatu vinapotengana, tunasema mtu "kafa".
   
 17. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #17
  Aug 28, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,355
  Trophy Points: 280
  Joto pia linaweza lisiwe kipimo, watu wanazimia/kupata coma katika subzero temperature huwa wanaweza wasipimike kwa hayo hapo juu.Mapigo ya moyo yanaweza kuwa almost nill,comma macho huwa yanakuwa static.Kama atakuwa exposed vizuri anaweza asiungue ngozi.Na kwa vile mahitaji ya chakula ni kidogo kwa mztu aliye ktk coma,moyo hauhitaji kupump damu sana,joto la mwili litakuwa chini sana kiasi ch akusimamisha activities nyingi sana na mwili unaweza usifikie kuharibu protein muhimu.


  Kuhusu brain kufa.Kuna baadhi ya mambo ya miwli yanakuwa controlled na spinal cord ,na upande fulani wa ubongo.Kwa hiyo partial death inaweza isiwe kigezo cha kuhakikisha kuwa mtu kafa.

  Test za kifo ni debatable kwa jinsi madaktari bingwa wanavyogundua mamabo tofauti.Wanvyoweza fanya upasuaji wa ubongo, moyo, ini, macho, wanavyoweza pima signals na ku decode, wanakuja kundua kuwa wanaweza badili vyote hapo juu na mtu akawa hajafa.Kwetu sisi mtu akiingia katik mazingira hayo kuna uwezekano akafa akiwa katika coma kwa mazingira anayowekwa au hata zoezi la kuzika,au hata akafia ardhini,au akafa kwa kuchomwa kama hiyo ndio mila.
   
 18. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #18
  Aug 29, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,679
  Trophy Points: 280
  Kufa,kazi ipo hapa,ninavyojua mimi,kufa maana yake ni kitu kushindwa kufanya kazi.Tunaposema mtu kafa tunamaanisha mwili umeshindwa kuendelea kuwepo.Kinachokufa ni mwili sio WEWE,ndo maana utasikia MWILI WA JUMA.Hii inamaana yule sio Juma ila mwili wake.Ili ieleweke au iamuliwe mwili umekufa ni mpaka maeneo muhimu ya mwili yawe hayafanyi kazi,moyo na ubongo ndivyo vinavyofanya mwili uishi.Kwa mfano moyo,moyo ndio unaoisafirisha damu kwenye mwili,na damu moja ya kazi yake ni kusafirisha chakula na oxygen.Damu ikisimama au ikishindwa kufika eneo moja la mwili,eneo hilo litaoza kwa sababu limekosa oxygen,mfano,ukichukua kamba ukafunga kiasi cha damu kutokupenya kwenye kidole,utapata matokeo hayo.Hivyo kufa ni mwili kushindwa kujiendesha au kufanya kazi!
   
 19. Ambitious

  Ambitious JF-Expert Member

  #19
  Aug 29, 2012
  Joined: Dec 26, 2011
  Messages: 2,125
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Scary stuffs..
   
 20. Iron Lady

  Iron Lady JF-Expert Member

  #20
  Aug 29, 2012
  Joined: Mar 4, 2008
  Messages: 4,077
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  mh sasa hii inazidi kuwa mbaya sana,
   
Loading...