Kufa kufaana .... Mchungaji Dr. Rwakatare kumrithi Marehemu Mbatia? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kufa kufaana .... Mchungaji Dr. Rwakatare kumrithi Marehemu Mbatia?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Keil, Oct 28, 2007.

 1. K

  Keil JF-Expert Member

  #1
  Oct 28, 2007
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mchungaji Rwakatare kumrithi Mbatia

  na Mwandishi Wetu

  MCHUNGAJI kiongozi wa Kanisa la Assemblies of God Mikocheni B, Dar es Salaam, Dk. Gertrude Rwakatare, anatajwa kuwa ndiye anayetarajiwa kuirithi mikoba ya ubunge ya Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Salome Joseph Mbatia, aliyefariki dunia kwa ajali ya gari Jumatano iliyopita, Njombe, mkoani Iringa.

  Mbatia aliyefariki dunia akiwa katika kampeni za kusaka kura za ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC), alipata uwaziri kutokana na kuwa Mbunge wa Viti Maalumu kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

  Kwa mujibu wa dodoso za kisiasa, Dk. Rwakatare mwenye umri wa miaka 55, ambaye pia ni mmiliki wa shule za St. Mary's, anapewa nafasi hiyo kutokana na mtiririko katika orodha ya wagombea wa Viti Maalumu vya ubunge kupitia chama tawala, CCM ambao majina yao yalipelekwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

  Katika orodha hiyo iliyotokana na uchaguzi mkuu wa mwaka 2005, jina la Dk. Rwakatare (CCM) linatajwa kuwa lilishika nafasi ya 61 kati ya majina ya wagombea wa Viti Maalumu vya wanawake yaliyopelekwa NEC kwa ajili ya kuthibitishwa kupenya hadi bungeni.

  Kwa mujibu wa NEC, CCM inawakilishwa bungeni na wabunge 58 wa viti maalumu vya wanawake. Kati ya wabunge hao, 42 wanawakilisha mikoa ya Tanzania Bara, kila mkoa ukiwakilishwa na wabunge wawili na wabunge 10 waliochaguliwa na chama kutokana na kushika nafasi ya tatu nyuma ya wabunge hao 42 kutoka mikoani.

  Lakini jina la Dk. Rwakatare na wengine kuanzia namba 60 kwenda juu, lilikatwa kutokana na kuwapo viti maalumu 58 vya wanawake vya kuiwakilisha CCM bungeni. UWT ilitoa upendeleo kwa kulipa kila kundi kiti kimoja isipokuwa UVCCM iliyopewa viti viwili.

  UVCCM ilipewa nyongeza ya kiti kimoja baada ya Baraza Kuu la umoja huo kutaka kupewa kiti kimoja zaidi, likipinga kuwa na mwakilishi mmoja tu katika chombo hicho cha kutunga sheria.

  Katika mkutano huo, wajumbe wa Baraza Kuu la UVCCM, waliweka shinikizo kwamba endapo kiti hicho kisingeongezwa, basi hata ile nafasi moja ambayo walipewa wangeikataa.

  Katika mchakato wa kutafuta wawakilishi wa umoja huo, Lucy Mayenga, alishika nafasi ya kwanza, nafasi ya pili ilichukuliwa na Amina.

  Dk. Rwakatare hakupatikana kuzungumzia suala hilo, kwani kila alipotafutwa kupitia simu yake ya mkononi, ilikuwa haipatikani.

  Naye, Dk. Ishengoma alipotafutwa kuzungumzia angalau mtu aliyemfuatia, alidai yuko mbali na Dar es Salaam na kwamba hafahamu lolote.

  Hata hivyo, kulingana na orodha, baada ya Dk. Ishengoma, Mkuu wa Mkoa wa Pwani aliyeirithi mikoba ya hayati Amina Chifupa, anayefuatia ni Dk. Rwakatare.

  "Huyu yupo katika orodha ya waliopendekezwa na CCM, kama ilivyo kwa Dk. Ishengoma, si unakumbuka hata aliyemrithi Amina Chifupa hakutoka UVCCM? Wote hawa ni watu wa CCM, kwa hiyo inawezekana akarithi mtu kutoka katika orodha ya NEC, hasa anayemfuatia Dk. Ishengoma," kilieleza chanzo chetu cha habari.

  Dk. Ishengoma, baada ya kukabidhiwa mikoba ya Chifupa aliyefariki Juni 26, mwaka huu, aliapishwa Agosti 16, mwaka huu.

  Dk. Ishengoma, aliapishwa katika siku ya mwisho ya mkutano wa Bunge la Bajeti ya serikali ya mwaka wa fedha wa 2007/2008.

  Source: Tanzania Daima
   
 2. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #2
  Oct 28, 2007
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,222
  Likes Received: 2,086
  Trophy Points: 280
  Ina maana Mama Rwakatare kaacha kazi ya kuwaombea watu kanisani kajiunga na siasa? Anaweza kuwatumikia mabwana wawili kwa wakati mmoja kweli? Anaweza kweli kuitumikia sisiemu iliyochafuka kwa rushwa, upendeleo, kujuana na ukabila na wakati huo huo kumtumikia Mungu kwa moyo wake wote? Anawaweka kundi lipi kondoo wake ambao sio wana sisiemu?
   
 3. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #3
  Oct 28, 2007
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Kufikia hatua ya kuwa na mashule kama St.Mary's na Kanisa kubwa la namna ile lazima uwe na connection na CCM maana wadanganyika wanaamini without CCM hakuna cha halali. Muda wote nimekuwa najiuliza nguvu na hata utajiri wa huyu Mama lakini leo kujua kwamba yuko katika Siasa pia basi nimechoka . Haya makanisa yana maana yake maana leo hii Pengo kama ataamua kugombea Ubunge kwa CCM sijui hatma ya waumini wa Katoliki itakuwaje. Mungu ni mwema sasa tutaanza kuhoji nguvu za giza za huyu Mama na mkono wake mzito ndani ya CCM kama ni sawa na mahubiri yake .
   
 4. Mtaalam

  Mtaalam JF-Expert Member

  #4
  Oct 28, 2007
  Joined: Oct 1, 2007
  Messages: 1,278
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 145
  sasa naanza pata hata hofu juu ya huduma ya mama yule... na pia naanza pata hofu juu ya kifo kile...na ol in ol nazidi ongeza hofu na kupoteza imani na chama chetu tawala cha chukua chako mapemaaaaaa aka chama cha mafisadi..c.c.m!!kidumu chama cha mafa**
   
 5. Mushobozi

  Mushobozi JF-Expert Member

  #5
  Oct 28, 2007
  Joined: Aug 20, 2007
  Messages: 543
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  lakini si nilisikia yuko kwenye orodha ya watu wanaotumia misaada ya watoto yatima kujinufaisha mwenyewe?
   
 6. Nyangumi

  Nyangumi JF-Expert Member

  #6
  Oct 28, 2007
  Joined: Jan 4, 2007
  Messages: 508
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyu mama nasikia ana connection katika yale majina ya Mh.Marehemu AC.
  Ntaambiwa majungu.Te te hehehehe.
   
 7. F

  FDR Jr JF-Expert Member

  #7
  Oct 29, 2007
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 249
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  JF ni mahali patakatifu? Nadhani tuwe wakweli tu juu ya yale yanayojiri hapa kwetu,kwa kufanya hivyo tutakuwa tunawatendea haki watakaoirithi nchi yetu.

  Dkt Mwamasika alishawahi kuwa politician,Supa alikuwa kasisi,Mch.Jesse Jackson alishawahi kuwa mwanasiasa akifanana sana na Barack Obama lakini sasa yeye ni mwanaharakati.Tunao Masheikh wengi na wanazuoni ambao ni wanasiasa,why Getrude Pang'alile Rwakatare??? Anayo haki ya kuchagua na kuchaguliwa,ni haki yake ya kikatiba akiwa ni raia wa nchi hii.

  Vyovyote itakavyokuwa,itakavyosema ni lazima tukubali kuwa kila binadamu ana historia ya heri na shari maishani mwake,hilo ni wazi na dhahiri.

  Mwisho ningependa tu ndg zangu tufahamu kuwa 2005 huyu mama aliamua kuingia kilingeni kwa dhati na ni miongoni mwa viongozi wa dini waliojitokeza hadharani kumuunga mkono Jakaya,ikumbukwe kuwa Jakaya ndiye aliyekifungua kile kituo cha malezi ya watoto yatima pale Tabata Bima mwezi kati ya May-July 2005,huyu mama aliamini kuwa kupitia akina mama wa mkoa wa morogoro angelipata ushindi kwa njia za uaminifu tu,alifanya kampeni ya kiungwana sana lakini akaja kuzidiwa na shemeji yake Makamba (Dkt Ishengoma)na tajiri ya Kichaga (Mama Nkya)kwa nguvu ya fedha.Wakina mama wa morogoro waliuza utu wao kwa wageni kwa sababu ya fedha na wakamnyima mwenzao kwa sababu tu aliwaomba kura kwa uungwana,nihitimishe kwa kusema kama ataipata nafasi hiyo ni wajibu kwake kumlilia mungu wake kwa ajili ya mkoa wa morogoro lakini zaidi kuhakikisha 2010 uhalifu wa kura haupewi nafasi.Mungu awabariki sana
   
 8. Gembe

  Gembe JF-Expert Member

  #8
  Oct 29, 2007
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 2,505
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  nilikuwa najiuliza ni kwanini huyu mama lipewa nafasi ya kundi la vijana ambacyo iliachwa wazi na amin chifupa,kumbe ni connection ya Makamba,kulundikiwa cheo kwa huyu mama,
  kwanini hawa wasomi wasirudi vyuoni kufundisha na siasa?
  ushemeji+usanii+mtandao=Ufisadi
   
 9. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #9
  Oct 29, 2007
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,855
  Likes Received: 2,431
  Trophy Points: 280
  kama ningekuwa mshauri wa mama rwakatare ningemshauri aachane na mambo ya ubunge kwani lazima achague kati ya utumishi na ubunge..ajifunze kwa mwemzake kakobe alipojiingiza kwenye siasa alipoteza imani kwa waumini wake wengi hadi ikabidi awaombe radhi na kuachana na siasa...

  akumbuke kati ya wafuasi wake wengine hawatamuelewa akiwa biased kama mbunge wa ccm...japo wengi wanaweza kumkubali...labda kama nchi yetu ingekuwa inakubali wagombea binafsi....
   
 10. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #10
  Oct 29, 2007
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,222
  Likes Received: 2,086
  Trophy Points: 280

  Ikumbukwe kuwa hatupingi suala la Mama Rwakatare kwenda kwenye siasa. Ila tunaongelea suala la 'Full-fledged politics' za sisiemu na uchafu unaoendana nazo.
  1. Kwamba Mama huyu yuko tayari kutumia pesa (regardless kama ni pesa chafu ama vinginevyo) kupata madaraka kama ilivyo jadi ya chama chake, na wakati huo huo kumtumikia Mungu? Kwa sababu sisiemu ya sasa, bila pesa haiendi, hapendwi mtu.
  2. Yuko tayari kutumikia siasa za fitina (ambazo ni jadi ya chama chake)za kupakana matope na wakati huo huo kuwahubiria habari njema waumini wa kanisa lake?
  3. Ako tayari kukaa vikao vya usiku wa manane na kupanga mikakati ya 'ushindi wa kishindo', wakati anajua kuwa mbinu hizo ni haramu na kinyume cha maadili?
  4. Mwenyekiti wa chama chake anasema hajui kwa nini Tanzania ni masikini hadi leo, yeye mama anayetaka kuingia huku anajua chanzo cha umasikini wetu?
  Tujifunze kutochanganya siasa na dini, tumkumbuke Kakobe enzi za Mrema.

  Tuendelee kulumbana kwa faida ya taifa.
   
 11. bokassa

  bokassa JF-Expert Member

  #11
  Oct 29, 2007
  Joined: May 19, 2007
  Messages: 403
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hivi mtikila ni nani vileee!!!!!!
   
 12. M

  Masatu JF-Expert Member

  #12
  Oct 29, 2007
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Mama Rwakatare ni haki yake anayopewa na katiba ya nchi kushiriki siasa katika chama anachokipenda. Huyu mama yupo makini sana na ndio maana amekuwa tishio kwa maslahi ya wachache ambao kwao mchungaji mzuri ni yule anaeshinda mahakamani na kufurumusha matusi kwa viongozi wa chama tawala.

  Suala la kuchanganya dini na siasa halipo hapo tusilazimishe hoja akiwa Bungeni hatoi mahubiri ya bwana same as akiwa kanisani hatonadi sera za chama.
   
 13. M

  Mwafrika wa Kike JF-Expert Member

  #13
  Oct 29, 2007
  Joined: Jul 5, 2007
  Messages: 5,194
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  go rwakatare,

  jiunge na kundi la wafisadi! kwani wewe malaika ukae pembeni wakati wengine wakitajirika kwa kuuza nchi?

  Rwakatare, kula nchi mama, I am all for you. Be careful though usisafiri kwenda mikoani kutetea ufisadi huko kwani utakumbana na hasira ya MUNGU wa kweli!
   
 14. M

  Masatu JF-Expert Member

  #14
  Oct 29, 2007
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Kazi kweli kweli...
   
 15. M

  Mwafrika wa Kike JF-Expert Member

  #15
  Oct 29, 2007
  Joined: Jul 5, 2007
  Messages: 5,194
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  sio kazi tu,

  bali moto pia!
   
 16. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #16
  Oct 29, 2007
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,222
  Likes Received: 2,086
  Trophy Points: 280

  Kazi ipo!
  Hahahahhh
   
 17. bokassa

  bokassa JF-Expert Member

  #17
  Oct 29, 2007
  Joined: May 19, 2007
  Messages: 403
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Natamani kuona boriti za mwafrika wa kike!! usije niambia huna hata kijibanzi!!!!!
   
Loading...