Kuepusha Taaruki Rais awe anahutubia taifa kila mwisho wa mwezi

realoctopus

JF-Expert Member
May 11, 2014
3,232
1,981
Wapendwa wana JF,nawasalimu sana.

Nimekuja kiushauri,kwa kiongozi wetu mpendwa.

Namshauri atenge muda wake,angalau mara moja kwa mwezi,ili aweze kuongea nataifa.

Katika kuongea na taifa lake,itakuwa rahisi sana kwake kujifunza mambo mapya wananchi wake wanapitia.

Pia,itamsaidia kupunguza malalamiko kutoka kwa wananchi kwamba mambo hayaendi sawa,kumbe kwa kuongea nao wataweza kujua ni kwa nini unaamua kuchukua njia A badala ya B katika kuendesha taifa.

Katika kuongea nao,wataweza kujua ni kwa nini flani katika utawala wako huwezi kumuondoa licha ya makelele sababu anamuhimu kuliko mwengine.

TENGA MUDA ONGEA NA WANAO,NI USHAURI TUU.
 
Hivi unavyoshauri hivyo ulimsindikiza kuchukua fomu..!?
Mtu alishasema lakini bado mnamng'ang'ania
na licha ya hivyo mpaka yule mwingine akathubutu kutuita MALOFA nitaikumbuka hii hadi nakufa ila siku moja atalipa tu.
 
Kuna jambo rais ashauriwi vizuri,Na kama anashauriwa basi ni mbishi ndio maana kila kukicha anaandamwa bila yeye kujua tatizo linaanzia kwake.
Unapoongoza nchi yapo mambo mengi yanatokea,Na yapo yale yanayogusa au kustua jamii kubwa.Mara nyingi mambo hayo yanahitaji yatolewe ufafanuzi wa kiuongozi.
Rais ameogopa kama si kudharau mtindo mzuri wa kuongea na wananchi kila mwisho wa mwezi.
Hiyo ndio ilikuwa nafasi/uwanja pekee wa rais kujibu kero,tuhuma na mambo yote yenye utata kwa nchi.
Kwanza faida yake angejibu mambo baada ya tafakuri kutokana na uzito wa jambo na si kukurupuka anapokuwa kwenywe zinduzi za miradi.
Angeandaa majibu yenye shebe na utafiti wa kina wa kitaalamu,Majibu ambayo yasingeleta taharuki na kumfanya yeye anayeanzisha taharuki kuja kukasirika pale watu wanapozidi kuhoji au kutokuridhishwa na majawabu yake kama baba.
Ushauri:Ikulu mshaurini rais arudishe utaratibu wa kuongea na watoto kila mwisho wa mwezi.Kwanini anaogopa?
 
Ili kusiwe na taharuki pamoja na mkanganyiko miongoni mwetu ni heri asihutubie kabisa mpaka atafute mtu awe muongeaji kwa niaba maana swahiba hata kwenye msiba analeta mada tofauti usishangae akapewa nafasi ya kuongea harusini akaanza kumshambulia Nape kua anasababisha kuchelewa kwa Tz ya viwanda.
 
Hahahhahha mwezi una unatani na mkulu uo mwezi mzma ajapata coverage afu vijana kama Nape waendelee kutamba thubutu
 
Kuna jambo rais ashauriwi vizuri,Na kama anashauriwa basi ni mbishi ndio maana kila kukicha anaandamwa bila yeye kujua tatizo linaanzia kwake.
Unapoongoza nchi yapo mambo mengi yanatokea,Na yapo yale yanayogusa au kustua jamii kubwa.Mara nyingi mambo hayo yanahitaji yatolewe ufafanuzi wa kiuongozi.
Rais ameogopa kama si kudharau mtindo mzuri wa kuongea na wananchi kila mwisho wa mwezi.
Hiyo ndio ilikuwa nafasi/uwanja pekee wa rais kujibu kero,tuhuma na mambo yote yenye utata kwa nchi.
Kwanza faida yake angejibu mambo baada ya tafakuri kutokana na uzito wa jambo na si kukurupuka anapokuwa kwenywe zinduzi za miradi.
Angeandaa majibu yenye shebe na utafiti wa kina wa kitaalamu,Majibu ambayo yasingeleta taharuki na kumfanya yeye anayeanzisha taharuki kuja kukasirika pale watu wanapozidi kuhoji au kutokuridhishwa na majawabu yake kama baba.
Ushauri:Ikulu mshaurini rais arudishe utaratibu wa kuongea na watoto kila mwisho wa mwezi.Kwanini anaogopa?
Ni ishauri mzuri, ila umempa raisi anayejiamini na asiyepangiwa cha kufanya.
 
mkuu, kabla ya kutekeleza hilo inafaa Rais afundishwe/ajifunze lugha ya kidiplomasia. na kwa vile alishawahi kusema yeye sio mwanasiasa ndio maana mara zote hotuba zake hazikosi maneno yenye ukakasi.
tatizo amesema yeye hapangiwi.
 
Asee
Bora akae kimya kabisaaa
Maana kila akihutubia lazima toe boko
Hamna kitu hapo
 
Labda awe anahutubia siku hakuna mechi za majuu.Ya nini kuharibiwa wkend ?
 
Muda wa kuzungumza sidhani kama ni issue sana mana hekima na busara visipotangulia hata akizungumza mara moja kwa miaka mitano haitasaidia kitu.
 
Back
Top Bottom