anti-fisadi
JF-Expert Member
- Nov 20, 2010
- 368
- 31
MMM katika hili tupo pamoja,tungeomba NEC waweke wazi palipo na lawama na vilevile Ukawa waweke wazi matokeo walio na utata nayo ili iamulike mapema na kwa amani #tanzaniakwanza
....utakuwa ni utani. Kwanini upinzani walikubali kuingia kwenye kinyang'anyiro cha kugombea? Kuna umuhimu wa kuheshimu vyombo halali vilivyoundwa kwa mujibu wa katiba
Siku hizi vipenzi na mashujaa wa chadema ni lowassa kingunge na sumaye, ama kweli siku zinaenda kasi sana!
Ila Kingunge huyu huyu si ndio Aliipinga sana rasimu ya katiba? Liwe funzo kwa wanasiasa kwa sababu siku yoyote unachokipinga kinaweza kukugeuka straighty.
hahahahahahaUnaweza kujipeleka Milembe ukifikiri umepoteza network hakyamama .....pesa mwanaharamu aisee ...
No prob, furaha yako itakamilika tuu!, kwa kazi nzuri iliyoifanyia UKAWA, do you still have a nerve and the moral authority kuishauri UKAWA what to do?!.Tume ina aminiwa kuendelea kutangaza matokeo
watu waamini matokeo yanayoendelea
M. M. Mwanakijiji
Neno la Hekima: Kama kweli Mbowe na Team Lowassa wanaamini kuwa matokeo ya Urais yamehujumiwa wanahitaji kwa haraka kufanya hivi: Kwa matokeo ya majimbo 113 ambayo yametangazwa hadi hivi sasa watoe nakala za mawakala wao kwenye majimbo hayo ili wananchi waweze kulinganisha kama yanaendana na yale ya Tume hasa kwa vile Jaji Lubuva Tumatatu alisema kuwa wao wanatangaza matokeo yale yale yaliyosainiwa majimboni.
Wakifanya hivi wataweza kuonesha kama Tume inaweza kuaminiwa kuendelea kutangaza matokeo au la. Ushauri huu pia unaweza kuwafaa CCM nao wafanye hivyo hivyo ili tuone hili. Lakini pia natoa ushauri kama huu kwa TUme ya Taifa ya Uchaguzi Kuagiza Wasimamizi wa Uchaguzi kwenye Majimbo yote ambayo tayari yametangazwa rasmi na yale yatakayotangazwa rasmi kuweka hadharani nakala zao za majimbo na hivyo tutaweza kulinganisha matokeo ya vyama, wasimamizi wa uchaguzi na tume ili tuepushe mambo ya kuitana Ikulu tena kwa mazungumzo zaidi.
Ili vyama visijisikie kuwa kwenye mtego, Tume iruhusu vyama hivyo kuweka hadharani nakala za matokeo yao kwa majimbo yale ambayo yameshatangazwa na mengine baada ya kutangazwa ili kukata mzizi wa fitina.
Hii ndio njia pekee ya kufanya watu waamini matokeo yanayoendelea au la. M. M. Mwanakijiji
Unaonaje na Zenji wakiufanyia kazi huu ushauri?
Na unadhani wataufanyia [kote bara na visiwani]?
Real? seriously? Dr Mihogo si hajabu naye akikana hakuwahi kuwa katika dubwasha hili. hongera kwa unafki wako.Well.. guess what; its a free country na Utanzania wako haunizidi wa kwangu. Huwezi kufanya lolote la hilo. Ila kuhusu UKAWA.. sikuwahi kuwa karibu na hilo dubwasha.