Kuendelea Chuo au kwenda Chuo cha Polisi?

Habari Wanabodi,

Nina binti yangu yuko mwaka wa kwanza chuo akiwa na 80% ya mkopo HESLB ila amekuwa shortlisted usaili wa Jeshi la Polisi.

Hivyo naomba mawazo yenu aendelee na Chuo au aende CCP ikitokea amepita usaili?

Natanguliza shukran.
Mwambie aahirishe masomo, aende CCP kwanza halafu akitoka huko anakuja kumalizia miaka ya chuo aliyobakiza. Ni bonge la bahati iwapo tu ataruhusiwa kuahirssha masomo
Asiporuhusiwa kuahirisha; mwache aendelee na masomo yake amalize kwanza. CCP anaweza kuomba tena baada ya masomo yake
 
Habari Wanabodi,

Nina binti yangu yuko mwaka wa kwanza chuo akiwa na 80% ya mkopo HESLB ila amekuwa shortlisted usaili wa Jeshi la Polisi.

Hivyo naomba mawazo yenu aendelee na Chuo au aende CCP ikitokea amepita usaili?

Natanguliza shukran.
Sasa amekuwa tu shortlisted hajaenda hata usaili we umeshaanza kufikiria habari ya aache chuo au la. Jibu mbona liko wazi afanye usaili asubiri matokeo wakati anaendelea kusoma. Akipata nafasi ameajiriwa kwa mtazamo wangu na kwa ugumu wa ajira wakati tulio nao aahirishe chuo kwa kufuata utaratibu aende mafunzo ya jeshi. Chuo kipo tu polisi wangapi wako masomono sahivi. Ni hayo tu.
 
Habari Wanabodi,

Nina binti yangu yuko mwaka wa kwanza chuo akiwa na 80% ya mkopo HESLB ila amekuwa shortlisted usaili wa Jeshi la Polisi.

Hivyo naomba mawazo yenu aendelee na Chuo au aende CCP ikitokea amepita usaili?

Natanguliza shukran.
Simply! Miaka kadhaa nyuma na mimi nilikuwa mwanafunzi wa mwaka wa kwanza,nikisoma bachelor of science in education chemistry and biology,na boom nilipata,nilipata fursa hiyo ya ajira polisi niliacha chuo,nikaenda CCP,baada ya kuingia kwenye mfumo wa ajira nikaanza kusoma OPEN UNIVERSITY OF TANZANIA,namaliza mwaka huu nikisoma Bsc ICT.Niliosoma nao A-level wengine mpaka sasa hawana mishe licha ya kumaliza degree za science,sasa huyo aliyesoma masomo ya sanaa,anashupaza shingo,aende CCP faster,asijulize mara mbili
 
Polisi sijui wanaishije laki tano kwa mwezi duuh
Unalipwa according to your education,haiwezekani na elimu yako ya form four yenye D mbili ulipwe milioni,hakuna taasisi yoyote ile serikalini utalipwa huo mshahara,ukiwa na elimu kubwa utalipwa pakubwa pia,hata huko polisi unapodai maslahi madogo,ni kwa wale wenye elimu za kuunga unga,ila wenye elimu zao kuanzia degree wanalamba parefu sana! Hata walimu pia mshahara wa mwalimu mwenye certificate ni tofauti sana na mwalimu mwenye degree.Hata kama wote wanafundisha shule ya msingi.weka kichwani hiyo
 
Polisi sijui wanaishije laki tano kwa mwezi duuh
I have a friend, a classmate, he is a police officer, ni graduate tulisoma wote LLB Mzumbe.

He earns more than 1.7M per month.

I have seen his salary slip, he has a basic salary of 965K plus about 4 different allowances which are tax-free. His take-home is 1.4M per month, he says apart from the salary they are also being paid a fixed ration allowance 300K each month and another allowance nimeisahau jina. So these guys don't earn that fedha kiduchu uliyoisema, hiyo ni uongo
 
Chuo lakini hakikisha anasomea kitu ambacho kitamsadia kwenye kazi. Hata Polisi anaweza kwenda baada ya chuo hiyo pesa atakulipa maana anapanda cheo haraka na elimu.

Ushauri wangu ni kitu gani anasoma nashauri asome vitu kama software engineering, design, Accounting, Finance au engineering. Akisomea social studies kama sociology na Human resources ni kama kupoteza pesa kama yuko kwenye hizo abadilishe
Usikilize hata huu sio ushauri
 
I have a friend, a classmate, he is a police officer, ni graduate tulisoma wote LLB Mzumbe.

He earns more than 1.7M per month.

I have seen his salary slip, he has a basic salary of 965K plus about 4 different allowances which are tax-free. His take-home is 1.4M per month, he says apart from the salary they are also being paid a fixed ration allowance 300K each month and another allowance nimeisahau jina. So these guys don't earn that fedha kiduchu uliyoisema, hiyo ni uongo
Hiyo uliyoisahau ni posho ya vinywaji wanapewa laki 3 kila baada ya miezi 3
 
Mm mbona nna mshahara huo kwa mwezi na nna nyumba tatu sa ivi na gari mbili tena nyumba moja iko kigambon mbili ziko tabora huku na mm n polisi so ishu sio mshahara bablai utakufa maskin
Hilo nalo mkalitazame
IMG_20230203_072632.jpg
 
Back
Top Bottom