Kuendelea Chuo au kwenda Chuo cha Polisi?

Kuendelea Chuo au kwenda Chuo cha Polisi?

Simply! Miaka kadhaa nyuma na mimi nilikuwa mwanafunzi wa mwaka wa kwanza,nikisoma bachelor of science in education chemistry and biology,na boom nilipata,nilipata fursa hiyo ya ajira polisi niliacha chuo,nikaenda CCP,baada ya kuingia kwenye mfumo wa ajira nikaanza kusoma OPEN UNIVERSITY OF TANZANIA,namaliza mwaka huu nikisoma Bsc ICT.Niliosoma nao A-level wengine mpaka sasa hawana mishe licha ya kumaliza degree za science,sasa huyo aliyesoma masomo ya sanaa,anashupaza shingo,aende CCP faster,asijulize mara mbili
Mkuu, imekuchukua miaka mingapi kuhitimu degree yako Open University?
 
Habari Wanabodi,

Nina binti yangu yuko mwaka wa kwanza chuo akiwa na 80% ya mkopo HESLB ila amekuwa shortlisted usaili wa Jeshi la Polisi.

Hivyo naomba mawazo yenu aendelee na Chuo au aende CCP ikitokea amepita usaili?

Natanguliza shukran.
Akienda chuo uhakika WA kupata ajira anao?

Akienda CCP uhakika WA kupata kazi upo?



Kumbuka kina wasomi wengi wapo mitaani hawana ajira na walienda chuo wakamaliza wanauza mandazi hakuna ajira.

Kazi kwako.

Nafikili nimekurahisishia.
 
Basi umepata binti wa kujivunia... hizo akili itakuwa karithi kwa mama yake...

Mwache aende CCP... ipo siku utakuja kujua maamuzi aliyo yafanya yalikuwa sahihi...

Akitoka CCP mwambie akasome open university, hata wewe kama mzazi una weza kumudu gharama zake

Atamaliza ktk kipindi cha miaka mitatu digrii na baada ya hapo ana peleka vyeti ambavyo kwa mtumishi wa umma kupanda daraja ni baada ya miaka mitatu hadi mitano kama sijakosea...

Na moja kwa moja atakuwa ktk qulification ya kupata ukapteini/nyota moja. Kitakacho bakia ni historia

Na anaweza kuendelea kusoma mpaka kufikia miaka yake mitato akawa amepata na masters

Na una fahamu digree ni nyingi hivyo akiongeza thamani yake basi kila kitu ni mtelemko kuelekea mbele

Atakuja wasaidia ndugu zake wengine ktk taasisi na nje ya taasisi

Wanasema kuwa na ndugu au rafiki baadhi ya maeneo
1. Afya/hostali/daktari
2. Polisi/askari
3. Nk....
Kaka samahani turekebishe hapo kidogo Jeshi la polisi kwa rank ya nyota moja huwa ni mkaguzi msaidizi na siyo kapteni kwa mifumo ya majeshi ya hapa kwetu kapteni ni afisa wa askari jeshi la wananchi mwenye nyota tatu.
 
Back
Top Bottom