Kuelewa kunavyokuza kueleweka kwa Kenani Kihongosi

kevylameck

Member
Nov 3, 2013
18
19
25A1C802-6663-4586-B04C-3AD632DB484B.jpeg

Katibu Mkuu wa UVCCM, Kenani Kihongosi.

Na Kevin Lameck

Tuna masikio mawili na mdomo mmoja, kwa sababu tunapaswa kusikiliza zaidi na kuzungumza kidogo.

Huu ni msemo maarufu sana kwa waswahili na ambao unahusishwa na mwanahistoria Plutarch na mwanafalsafa Zeno wa Citium.

Ujumbe wa Papa Francisko katika siku ya kumbukumbu ya Mtakatifu Francis wa Sales kwa mwaka huu ulilenga kwa usahihi kuhusu 'kusikiliza'.

Papa Fransisco anasema shauku isiyo na mipaka ya kusikilizwa imeongezeka kote duniani kuanzia kwenye siasa, kwa familia nk.

Kusikiliza kunatajwa kuwa stadi muhimu ambayo kila mmoja anapaswa kuwa nayo. Kusikiliza ni mchanganyiko mzuri wa kusikia kile mtu mwingine anasema na kujihusisha na mawazo yake.

Bahati mbaya tumezoea zaidi ujuzi wa kusoma, kuandika na kuzungumza; kusikiliza kunatajwa kuwa muhimu zaidi hasa wakati huu wa changamoto za kijamii.

Jumatatu ya August 16,2021 Katibu Mkuu wa UVCCM Kenani Kihongosi kwa mara ya kwanza alitambulisha utaratibu wake mahususi wa kutenga siku maalumu za kuwasikiliza vijana wenzake na wale anaowaongoza.

Utaratibu wake huo ni tofauti na ule wa viongozi wa serikali kutenga siku za kusikiliza kero za wananchi. Kenani hakusudii kusikiliza kero pekee.

Mara zote anahitaji maoni na mitazamo ya anaowaongoza kuhusu uongozi wake, mambo gani ya kushughulikiwa na tafakuri kuhusu UVCCM ya siku za usoni.

Utaratibu huu umeendelea mara zote kwa kusikiliza mtu mmoja mmoja na kwa wingi unaokubaliwa na muda anaoutenga kufanya hivyo katika maeneo tofauti.

Kwa sisi tuliobahatika kushiriki mazoezi haya na ziara ya mwezi wa tano mwaka huu, ziara ya Vijana ngorongoro Green Tour tunaweza pia kushuhudia hili kwa nyakati tofauti tofauti. Alisikiliza wengi na kupata maoni yao binafsi kuhusu Siasa, uongozi na uwezeshaji wa kiuchumi.

Leo tena kwenye ofisi ndogo za UVCCM ,Upanga-Dar es salaam amerejea mpango wake. Ndg. Kenani anatufundisha kwa vitendo umuhimu wa kusikiliza.

Kusikiliza ni muhimu kwasababu ya uwezo wake wa kudumisha mahusiano pamoja na kuimarisha uwezo wa kukubali maoni ya wengine na hata kusikia yale mengine tusiyoyapenda.

Kadiri unavyosikiliza zaidi ndivyo unavyogundua kuwa sio tu unakuwa mtatuzi na msuluhishi bora wa changamoto na matatizo bali pia unakuwa mtu bora zaidi.

Kusikiliza ni ujuzi muhimu zaidi kwa Kiongozi. Ni msingi wa ujuzi na sifa muhimu zinazomtambulisha kiongozi bora na wa tofauti kwenye jamii.

Sio siri kwamba kuwa na hekima na ujuzi hakupatikani kwa kuwa mzungumzaji ama mzingatiaji wa hisia binafsi. Hekima na busara hupatikana kwa kusikiliza.

Andy Stanley Mmarekani, Mwanzilishi na mchungaji wa North Point Ministries anasema viongozi wasiosikiliza hatimaye watazungukwa na watu ambao hawana la kusema ama kushauri.

Kusikiliza kunakusababishia na kukuza ufahamu na ukuaji binafsi.

Usiposikiliza huwezi kustawi ama kustawisha ofisi ama biashara unayoifanya. Makampuni yaliyofanikiwa yamekumbatia vilivyo 'kusikiliza".

Viongozi wasiosikiliza ni viongozi wanaokataa kuzijua changamoto halisi zinazowaathiri watu wao. Ni viongozi wenye kujiona kuwa sahihi kuliko kupata majibu sahihi.

Viongozi hawa wanashindwa kutambua kuwa thamani ya kweli inajengwa pale tu wanaposikilizana kwa nia ya kuongeza maana katika mazungumzo, wanapokuwa huru kutoa maoni yao bila kuhukumiwa wanapojisikia kusikilizwa na kuheshimiwa kwa maoni yao.

Mshauri wa tabia na msaikolojia Stephen Covey anasema "katika tabia za watu wanaofaa sana ni pamoja na kutafuta kuelewa kisha kueleweka."

Covey anamaanisha kuwa hii ndiyo kanuni muhimu zaidi katika uongozi na kwamba kupitia hilo viongozi wanaweza kuleta mageuzi makubwa chanya kwenye jamii.

Jessane Collins mhariri wa jarida la Mental Floss yeye anasema mara nyingi uongozi unahusisha kusikiliza. Anasema "huwezi kuunda timu inayostawi ikiwa huwezi kujibu kile kinachoisumbua jamii."

"Kama kiongozi unahitaji kuwa na sauti yenye nguvu na unahitaji kujua ni wakati gani wa kusikiliza", anasema Amy Jen Su, mmiliki mwenza wa kampuni ya mafunzo ya uongozi nchini Marekani, Mhadhiri anayeheshimika sana mjini Baltimore na mwandishi wa kitabu maarufu cha "The leader you want to be."

Kusikiliza labda ndiyo siri inayotunzwa vyema na safari ya uongozi na maono ya Ndg. Kenani Kihongosi. Ni mtindo na aina bora ya heshima ambayo mtu yeyote anayezungumza naye anaweza kupata. Ni tabia ya kujifunza na kuitekeleza kuanzia ndani ya familia zetu.
 
Kwenye mpira hii huwa tunaita pasi ya tangulia tuonane. Yaani unapiga mpira kwa mbele halafu unamzunguka adui yako unauchukua tena. Yaani unajipasia.

Ina maana kumbe UVCCM haiyajui matatizo ya vijana wa Tanzania mpaka wanatenga muda wa kusikiliza?
 
Huyo msanii anafanya ulaghai na kufanya siasa zionekane kituko kwa wasomi. Mwambieni aeleze pesa za Rushwa alizopekea kwa mkono gani
 
Back
Top Bottom