Cicero
JF-Expert Member
- Jan 20, 2016
- 2,924
- 3,073
Mkataba wa uanzishwaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki umeainisha sifa za mtu kukidhi ili kuchaguliwa kuwa mbunge wa Afrika Mashariki. Mtu huyo;
1. Lazima awe raia wa nchi anayotaka kuiwakilisha
2. awe na sifa za kuchaguliwa kuwa mbunge wa bunge la nchi anayotaka kuiwakilisha
3. Asiwe waziri katika serikali ya nchi anayotaka kuiwakilisha
4. Sio afisa wa Jumuiya ya Afrika Mashariki
5. Ana historia ya kudhibitika ya kuunga mkono malengo na dhamira ya Jumuiya ya Afrika Mashariki
Pia mkataba unasema kila bunge la nchi mwanachama litawachagua wawakilishi hao (tisa) mradi wasiwe tayari ni wabunge wa nchi husika.
Ni kweli kwamba enzi zakuanzishwa kwa Jumuiya labda ilikuwa ni vigumu kwa wabunge wa Afrika Mashariki kuchaguliwa na wananchi moja kwa moja. Lakini sasa nyakati zimebadilika na litakuwa jambo jema endapo wananchi wataweza kuwachagua wawakilishi wao kwenye Bunge la Afrika Mashariki.
Uchaguzi mkuu ukifika watu wawe wanapiga kura ya kumchagua mbunge wa jamhuri Dodoma, mbunge wa Afrika Mashariki Arusha, mkuu wa mkoa wao (hii nimechombeza mwenyewe haihusiani na mada) na Rais wa Jamhuri.
Hii itasaidia sana watu kuifahamu Jumuiya yao kwa kuwa wawakilishi hao lazima watazunguka nchi nzima kupiga kampeni.
Natumaini uchaguzi wa mwaka huu utakuwa wa mwisho wa wabunge wa Afrika Mashariki kuchaguliwa na wabunge wa jamhuri na sio na wananchi wao moja kwa moja.
Nawasilisha hoja!