Uchaguzi 2020 Kuelekea Uchaguzi Mkuu

Hassan Rwitita

Senior Member
Sep 4, 2018
148
66
Hivi ccm na mwenyekiti wao pamoja na kuteua mkuu wa majeshi, wakuu wa mikoa, ma IGP na viongozi wote majeshi ya ulinzi na idara zake zoote, bado wanawaswasi na uchaguzi.

Ameteua Tume ya Uchaguzi na kaweka wanachama wake wote na kila afisa wapo lakini bado hawajiamini ni kwa Nini hawajiamini wakati mpaka askali polisi wanatembea na kadi ya CCM kwa nini wote wanahangaika na upinzani ambao wanasema haujafanya kitu hapa Tanzania.

Ila mwenyekiti wao ndio amefanya mengi kiasi kwamba hakutakiwa hata kufanya kampeni kwa mujibu wa watu wake wanomsifu Kama Yesu, bado vijana wa CCM viongozi wa CCM kuanzia shina mpaka juu kabisa wanawabugudhi wapinzani ni kwa Nini iwe hivyo ikiwa wanasema anakusanya Kodi, amejenga reli, amejenga madaraja Dar, na ameleta heshima maofisini, amemaliza rushwa kabisa amejenga shule anasomesha watoto bure amewakamata mafisadi jamani nasifa zote hizo lakini ameibuka na kutunga sheria ngumu sana, yaani kiasi kwamba yeye ndio amekuwa mpinzani wa maendeleo ambayo ilitakiwa awache watu waseme ili apate kunyosha alipokosea!

Katunga sheria za vyombo vya habari katunga sheria za mitandao, na sheria nyingi tu zinazohusu wanaomkosoa. Sasa lumumba Nani kawadanganya kuwa Tanzania inastahili kutawaliwa na CCM tu.

CCM na vibaraka wote mbona mnajitutumua lakini mnajawa na hofu dhidi ya chama Cha upinzani ambacho mnasema hakina Sera Wala ushawishi. Hebu jitokezeni Basi tujue tatizo liko wapi linalofanya muwe na hofu dhidi ya CHADEMA ambayo mnasema imekufa mnafikia kutumia polisi kuwabugudhi mnatumia mfadhiri wa viama vya siasa kuwasmea mmeenda mbali mpaka mnasema hata wimbo wa taifa wameuongezea ubeti mwingine haha!!

Vijana wa Lumumba na mwenyekiti wenu na majeshi yote mtungi na vikundi vyake nyie ndio mmekuwa wapinzani sio watawala Tena mnaishi kwa hofu kuliko hata wapinzani si kawaida kwa miaka ya hivi karibuni mumeongeza hofu kuliko awamu zote za utawala wa CCM mnanusa nini kilichoko mbeleni.

Sijui kuandikwa vizuri mtanisaidia kusahihisha nilipokosea
 
JPM kwa kweli ana kazi maana tayari Tundu Lissu kamwandalia form ya pingamizi na sasa anakusanyiwa ushahidi... ccm wajiandae kupangua hoja..Yaani mishale kila sehemu...wanasheria kazi ya ulaji kwenye uchaguzi huu - washindwe tu kujaza mapesa mifukoni mwao...asiye na mwana...
 
JPM kwa kweli ana kazi maana tayari Tundu Lissu kamwandalia form ya pingamizi na sasa anakusanyiwa ushahidi... ccm wajiandae kupangua hoja ... yaani mishale kila sehemu...wanasheria kazi ya ulaji kwenye uchaguzi huu - washindwe tu kujaza mapesa mifukoni mwao...asiye na mwana...
Yaani huku kuna wapambe Uchwara wa kutosha ambao nahisi akili zao kuna watu wamewapa wawashikie,,,, hivi kuna mtu wa kumshinda Mh. Magufuli kweli mwaka huu au mnaota ndoto mchana kweupe nyie?????!!!!!!! Poleni sana maana mna mategemeo hewa
 
Muovu hukimbia hata asipokimbizwa...nimesahau kitabu gani kwenye Bible
 
HOFU ya UCHAGUZI inaua. Eti "Bwana" yule anawaaminisha wananchi wasiwe na HOFU ya corona wakati yeye mwenyewe HOFU ya UCHAGUZI inampelekesha. Ama kweli tumbo ni mwanaharamu.
 
Siku zote mwenye kutenda mema na ya haki huwa hawezi muogopa yeyote kwa sababu anakuwa na baraka na ulinzi wa Mungu, kinyume chake ndicho watawala wetu kinachowatafsiri kwa muonekano wao. Hivyo hofu kuu ni kufunika huo moto wa mapumba unaofukuta kwa chini huku wakijitahidi sana kutuaminisha sisi darasa la saba kuwa mambo ni shwari sana na hakuna shida yoyote.

Kama wangekuwa watenda mema na ya haki wangejipima kwa kuacha uchaguzi huru na wa haki, usimamiwe na tume huru na vyombo vya nje visivyo na uegemezi wa pande yoyote, wasibighudhi wapinzani, waache kila mmoja kwa nafasi na uwezo wake afanye siasa zake kama demokrasia wanayoihubiri inavyowataka wafanye, waache tukamilishe mchakato wa katiba mpya na mwisho kabisa wasitumie vyombo vya dola na usalama kuingilia siasa za nchi.

Hapo sasa ndio watajua kati ya wajumbe wa posho na wajumbe wa kweli nani mjumbe haswaaa!
 
Yaani huku kuna wapambe Uchwara wa kutosha ambao nahisi akili zao kuna watu wamewapa wawashikie,,,, hivi kuna mtu wa kumshinda Mh. Magufuli kweli mwaka huu au mnaota ndoto mchana kweupe nyie?????!!!!!!! Poleni sana maana mna mategemeo hewa

Maisha na kuishi ni kuwa na matumaini hata pale inapooneka hakuna matumaini... inabidi uwe nayo,vinginevyo bila matumaini hata Masha yenyewe hayatakuwepo... Hata mfu, anatumaini kuendelea kuishi kwa kadri ya imani Yake...
 
Back
Top Bottom