Kuelekea Uchaguzi Mkuu Oktoba 2020

Subira the princess

JF-Expert Member
Mar 3, 2018
2,474
2,649
Wasalaam, tangu tumepata Uhuru tumetawaliwa na CCM, matatizo na umasikini tulionao umesababishwa na wakoloni weusi CCM. Hawa CCM wamegeuza hii nchi ya kifalme anatawala babu hadi mjuku, kazi yao kubwa wakoloni hawa kutuimbia watanzania ngonjera;


1. Mhe. Ally Hassan Mwinyi; ruksa
2. Mhe. Mkapa ngonjera yake ni; mtaji wa masikini ni nguvu zake mwenyewe
3. Mhe. Kikwete; maisha bora kwa kila mtanzania
4. Mhe. Magufuli; hapa kazi tu.

Pamoja na kauli mbiu hizo bado maisha ya Mtanzania wa kawaida yameendelea kuwa magumu na sababu ni hawa hawa ccm wakoloni weusi.

Rai yangu kwa watanzania bila kujali itikadi zetu za vyama wala ukanda, dini wala kabila tuungane kwa umoja wetu tukapige kura kuikataa ccm ili tupate Uhuru wa kweli tuweze kujitawala hii nchi ni tajiri na ni yetu zote wala sio Mali ya kikundi cha watu wanaojiita CCM. Tukumbuke ulofa tulionao tumepewa na CCM.

Ova..

Mungu ibariki Tanzania, watazame watesi kwa jicho lako ukawahukumu utulipie kisasi maana mateso yamezidi. Ameen
 
Siku nikisikia Mbowe siyo mwenyekiti tena nitaipigia kura Chadema.Chama cha familia kiongoze nchi????
 
Aiseee ukweli mtupu ,waliikunywa maji ya bendera ya kijani wanavyojitahidi kuidivert mada ,wanahangaika kweli ,jikiteni kwenye hoja.
 
Back
Top Bottom