Kuelekea Uchaguzi Mkuu: Chama cha ACT-Wazalendo chapokea 21 waliokuwa Wabunge wa CUF

CCM wanakamilisha Jambo lao Kubwa sana hapo kupitia CCM B a.k.a ACT Wazalendo ili Kupanga Mkakati wa Kukiua na Kukizika kabisa CHADEMA.
Ikifa chadema kwa kiasi gani umaskini wako utaisha mijitu mingine nyie ni hasara kwa Taifa
 
CCM wanakamilisha Jambo lao Kubwa sana hapo kupitia CCM B a.k.a ACT Wazalendo ili Kupanga Mkakati wa Kukiua na Kukizika kabisa CHADEMA.
Mbona ni kama kila mtu anajiona yeye ndo mpinzani kuliko mwingine?

Hii Sura inayojengeka ndio mbaya kuliko kuwahi kutokea
 
Ikifa chadema kwa kiasi gani umaskini wako utaisha mijitu mingine nyie ni hasara kwa Taifa

Bora yake Mimi ni Hasara kwa Taifa, ila Wewe Mwenzetu ni Takataka Kubwa, Mbaya na Kero kabisa kwa Wananchi wa Taifa letu hili la Tanzania.
 
Kwa ustaarab wa kawaida ACT walipaswa kushukuru hatua za Serikal kupambana na corona hadi nao len wamevua barakoa
 
Kwa haya majina ya wanaohamia na viongozi waliopo nachelea kusema ACT itakumbwa na propaganda ya udini. Kama CUF walivyokumbwa nayo.

Mbaya zaidi ni hauwezi kuchomoka.
 
Kumbe hii ndiyo imechukua nafasi ya CUF Zanzibar......maana naona bwege pekee kwa bara
 
Hongereni sana ACT Wazalendo ,Hongereni Sana Zitto,Maalim na Duni kwa kuweka maslahi ya taifa mbele ,Mtatiro aliipenda Sana CUF ila SHEKELI na NJAA zimempenda zaidi akaunga mkono JUHUDI.

Katika wanasiasa walionifedhehesha waliounga mkono JUHUDI ni Mtatiro maana jamaa alikuwa na misimamo dhabiti isiyoyumba lakini baada ya Kushikwa na NJAA ikabidi arudishe mpira kwa kipa na kuunga mkono JUHUDI kwasasa anakula SHUSHU tu.
 
Juzi tu Zitto alikuwa analilia lockdown kupunguza misongamano ili kujikinga na Corona, leo hii awekusanya watu kiasi hicho. Kweli mwanasiasa si wa kumsikiliza

Ahh, Hiyo furaha aliyokuwa nayo Zitto ni ya kufa mtu. CORONA ataikumbuka wapi!!!!!! Ukweli kijana kashinda bahati nasibu upende usipende. Maana ana maarifa ya vyama vikuu viwili ; CHADEMA NA CUF. Kakusanya wa wanachama wa vyama viwili hivyo ni sahihi kabisa kusema ACT- Wazalende ni muunganiko wa wazalendo wa nchi TZ tokaCHADEMA na CUF. Wakienda katika uchaguzi huku wakiringa kwa kujua siri, mbinu, udhaifu na nguvu ya vyama hivyo viwili.

Hata ukiwa wewe huwezi kukumbuka CORONA wala korokoroni. Jamani mwacheni kijana ajione anafaa kuwa kiongozi mkuu TZ. Jua liake, mvua inyeshe ACT- W haiwezi kukosa wabunge 15 TZ. Ni furaha ilioje toka mbunge mmoja mpaka 15 -- Chereko chereko
 
Wabunge 21 wa Viti Maalum au Majimbo?!

Hawa jamaa kwa upande wa Visiwani wako vizuri, ila huku Bara wanatakiwa kufanya jambo na "wenzao"..

Hao jamaa walimtapeli Lipumba.

Waliowengi ni majimbo, viti maalum ni wachache hapo. Ila mbunge ni mbunge tu akikukimbia toka chamani unapiga mayowe.
 
Chadema walimfukuza Zito walifukuza kichwa chenye hazina ya mipango.
Zito kamshawishi Maalim kujiunga ACT.
Zito muda si mrefu anamleta Lissu ACT.
Inamaana ACT ndo anaipiku Cdm.bunge lijalo watakuwa na wabunge wengi kutoka Zanzibar pia kura za Zanzibar na za bara zitawapa nguvu ya kutoa KUB wa bunge lijalo.
 
Back
Top Bottom