The mountain lion
JF-Expert Member
- Oct 6, 2014
- 1,153
- 412
Mkuu ukiambia you ignorant, usilalamike kuwa unatukanwa, ignorant maana yake ni mjinga, na mjinga ni kutojua, ukishaufuta ujinga, unakuwa sio mjinga tena maana sasa umejua!, kwa vile ulichoandika hapa ulidhani unajua, kumbe hujui, huo ni ujinga!, kazi yangu ni kukuelimisha tuu ili ujue!.
Laiti ungelijua Lowassa kabeba zigo la nani, na kavumilia kiasi gani, utakubaliana na mimi, kama nampa pekee ya kumshukuru ni kumpatia urais kama asante yake, bora hata huo urais apewe, tusonge mbele, kuliko akinyimwa na akaamua kusema, huo ndio utakuwa mwisho wa kitu kinachoitwa CCM.
- Richmond kweli ni kampuni hewa!, lakini mitambo ya Richmond sio mitambo hewa, ni mitambo ya ukweli!. Gharama za milioni 152 kwa siku, sio za gharama za kulipia jina la Richmond, ni gharama za kuilipia hiyo mitambo kwa siku!, na hapo bado gharama za kulipia umeme unaofuliwa na mitambo ile, na umeme huo huo sio umeme hewa ni umeme kweli!. Ungekuwa na akili, ungeuliza hizo fedha milioni 152 kwa siku zinalipwa kwa nani?!.
- Lowassa hakusaini chochote kwenye dili ile, bali alikuwa akipeleka maelekezo ya mwenye mitambo yake!.
- Kamati ya Mwakyembe aliposhauri mkataba uvunjwe tuu na hakuna kitakachotokea, mkataba ukavunjwa, Tanzania tukapigwa faini ya bilioni 90, bungeni wakaahidiwa hatulipi. Kwa taarifa yako, tozo ile tumeilipa kisiri siri!, umeme umepandishwa kufidia na Watanzania tunakamuliwa hadi kesho!. Ungekuwa na akili ungeuliza kama serikali iliahidi hailipi, imekuwaje tena tumelipa?, kwa nini tulipe kisiri siri/, na hizo fedha zimelipwa kwa nani?!. Na baada ya kulipishwa waliojitia kimbelembeli kuwa eti hatulipi, wako wapi, wamefanywa nini?!, Tanzania inhekuwa Chini, saa hizi hao jamaa ingekuwa ni historia tuu!.
- Zitto akashauri ama tuitaifishe mitambo au tuinunue!, maji yalipopungua, serikali yetu ikaamua kuiwasha mitambo ya IPTL yenye kutumia gharama mara 100 ya Dowans, huki ikituchafulia sasa hizi ni akili au matope!.
- Sasa kwa taarifa yako, ule mkataba wa kinyonyaji wa Richmond, bado upo, na ile capacity charge ya shilingi milioni 152 bado inalipwa daily!. Mitambo ya Dowans ndio hii, mitambo ya Simbion na mkataba ndio ule ule!, walio ilaani Richmond ndio walio ishangilia Simbion!. Nilifikiri ungetaka kujua ilikuwa tunaendelea kulipa, na anayelipwa hizi fedha ni nani?!.
Laiti mngelijua Simbion ndio ile ile Richmond na capacity charge ile ile, mkataba ule ule, watu humu msingesema, mngejinyamazia tuu kama Lowassa!. Hutuoni watu humu tumejinyamazia usidhani ni wajinga!, tuna maana yetu!.
Pasco
Huyo Lowasa wako mwenyewe aliahidi ataongelea sakata la Richmond pale Arusha lakini hakuluongelea na anakimbia kuliongelea. Unafikiri ni kitu gani anaficha kuhusu Richmond? Kama alibeba msalaba ambao sio wake kwa nini asituambie wapiga kura huo msalaba ulikuwa wa nani kwa nini afiche?
Ni wakina nani a najaribu kuwalinda.
Hebu jibu hapo Pasco.