Elections 2015 Kuelekea Uchaguzi Mkuu 2015: Ajenda ya UFISADI ni Kama IMEFIA kwa Magufuli na kuzikwa Kwa Lowassa

meningitis

JF-Expert Member
Nov 17, 2010
8,349
4,674
Mwaka 2010 hoja ya udini na ufisadi zilitawala katika kampeni na kupelekea kosakosa ya Chadema kuingia magogoni.

Tunapoelekea oktoba 2015 tunaona hoja ya UFISADI ikiibuka tena kama dhambi ya kuiadhibu ccm.

Fikiria kuhusu watuhumiwa wa Escrow, wale waliosafishwa vs walioachwa bila kusafishwa vs walioachwa bila kutuhumiwa.

Taarifa ya CAG imekuja wakati mbaya sana, hata kama upotevu wa matrillion 2014 ni sawa na upotevu wa mabilioni mwaka 2010.hoja itabaki kuwa ni upotevu mkubwa.

Mgombea kutoka pande yoyote ni lazima awe tayari kujibu hoja dhidi ya ufisadi na kutoa ahadi dhidi ya mafisadi.

Nani ni nani? Tusubiri tuone!

-----------
July 27
Ndugu wanajamii Nawaza kwa Sauti,

Imagine CCM wangemteua Lowasa kuwa mgombea nafasi ya Urais kwa tiketi ya chama chao, ni ipi ingekuwa ajenda namba 1 ya upinzani kwa wananchi dhidi ya CCM baada ya Katiba mpya?

KUCHAGULIWA KWA MAGUFULI na CCM ni kama KUUA hoja hii ya ufisadi kwa upinzani kwani rekodi yake ya utendaji kazi iko wazi na Ufisadi wake wa nyumba za Serikali ni wa kutafuta kwa tochi na aueleweki vizuri kwa wapiga kura wa kawaida..

KUKARIBISHWA KWA LOWASSA UKAWA ni mazishi ya Ajenda hii kwani nguvu kubwa itaelekezwa katika kutangaza sera za ukawa na KUMSAFISHA Lowasa na "Washkaji" zake atakaoamia nao UKAWA. kuna msemo kuwa "USIMCHOKOZE CHIZI WAKATI UPO KTK NYUMBA YA VIOO" kuishutumu CCM kwa ufisadi ni sawa na kumchokoza chizi.

MCHANGA WA MWISHO KTK KABURI LA AJENDA hii ni kauli za viongozi wa ukawa wakiongea na wanahabari kuwa mtu awezi kuitwa fisadi mpaka athibitishwe na MAHAKAMA! lol. kwa maneno haya Zee la Makengeza, Rosta, Tiba,na wote wa ESCROW, MEREMETA, EPA nk ni watu safi mpaka mahakama itakapothibitisha vinginevyo. Mafisadi labda ni Mramba na Yona.

Kwa kuwa wanasiasa ni opportunists usishangae kuona baadhi ya viongozi na wagombea ubunge/udiwani wakitoka CDM, NCCR, NLD, CUF kuelekea ACT kutake advantage ya Ajenda hii kutetea nafasi zao.

Vyovyote itakavyokuwa UFISADI si tu kete ya kisiasa bali ni janga la kitafa.

Mwisho wa kuwaza kwa sauti.
 
well said mkuu...
Hasa CCM ambao ni chama tawala hoja ya kwanza 1:Ufisadi, hoja ya Pili 2: Rushwa ....kisha zinaanza hoja za maendeleo ya Jamii....Patamu hapo ...kama mgombea wako mtalajiwa hana majibu hayo HANA NAFASI.
 
Ni kweli UDINI ndio ulioibeba CDM hata lema ARUSHA alipigiwa kampen huko KANISANI, kakobe Aliahirisha hadi misa akawa anahimiza waumini kumchagua mkiristu ule waraka ulioletwa na maaskofu ndo ulikuwa muongozo kwa mapandre
 
Mgombea yoyote awe wa ccm au upinzani ni lazima ajue kuwa ajenda kuu ya uchaguzi mwaka huu ni ufisadi.
Nakubaliana na wewe kwa asilimia 100%, tena isiwe tuu ni ufisadi bali pia rais wa nchi yetu lazima awe ni mtu mwenye long expiriaence ya uzoefu wa muda mrefu kwenye ajenda hiyo, nikimaanisha ili kuweza kumkamata mwizi, sometimes one has to 'set a thief to catch a thief!', hivyo mgombea pekee wa CCM mwenye sifa hiyo ni one and only Edward Ngoyai Lowassa, ndiye pekee mwenye uwezo wa kupambana na ufisadi kwa sababu sio tuu anaujua, bali yeye mwenyewe anatuhumiwa kuwa fisadi, hivyo ndiye pekee mwenye uwezo wa kupambana na ufisadi!.

Mtu yoyote asiye lijua tatizo kamwe hawezi kupambana nalo!, ili mtu uweze kupambana na tatizo, ni kwanza yeye mwenyewe ulijue tatizo, chanzo chake, na jinsi ufisadi unavyotekelezwa, hivyo kuwa na uwezo wa kupambana kwa kuzijua mbinu zote!.

Mfano hai ni ufisadi wa iliyokuwa City Water, Lowassa akiwa ni waziri wa Maji, baada tuu ya kuujua ufisadi wao, aliwatimulia mbali, wakafungasha virago vyao na kukimbilia mahakama ya usuluhishi kule London, nako tukawatwangwa, sasa imebaki tuu historia ya utendaji uliotukuka wa Edward Lowassa!.

Hivyo Lowassa ndio mtu pekee anayeujua sio tuu anayeujua ufisadi wa Tanzania nje ndani!, bali pia ndio mwenye uwezo wa kukabiliana nao na kuukomesha!. Mfano mzuri ni kwenye ufisadi wa Richmond!, Lowassa alishuhudia jinsi ufisadi huo unavyolitafuna taifa hili na uko kwenye level gani!, kwa ushujaa wa ajabu, akaamua kujitoa mhanga, yeye mwenyewe, kwa nafsi yake, kuibeba dhambi ya ufisadi huo uliotaka kuliangamiza taifa ili yeye ndiye ateketee lakini taifa liokoke!.

Ni kweli aliibeba hiyo dhambi na akafa nayo, kama yule aliyekuja kuzibeba dhambi za ulimwengu huu, ambapo kwa kupigwa kwake, sisi tuliponywa!, alikubali kudhalilishwa, kuteswa hadi kifo msalabani, lakini siku ya tatu, alifufuka na kwenda kwenye uzima wa milele huku amekaa kulia kwenye kiti cha enzi!.

Vivyo hivyo ufisadi wa Richmond, bado uko vile vile, Lowassa aliubeba msalaba ule ili taifa liokoke!, tofauti na yule aliyebeba dhambi za Ulimwengu, dhambi ya Richmond haikuisha kwa kujiuzulu kwa Lowassa, bali baada ya Lowassa kukaa pembeni, wenye Richmond yao, ambayo waliibadili jina kuwa Dowans, wakaishitaki Tanzania kule London, wakashinda!, Tanzania ikajidai haitalipa tozo ya Dowans, ila tozo ile imelipwa 'kisiri siri', Dowans ikajibadili tena jina kuitwa Simbion!, ufisadi ule unaendelea hadi kesho, mitambo ni ile ile!, capacity charge ni ile ile!, ila jina sasa ni Simbion!, na wanaendelea kupiga hela kama kawa!.

Mtanzania gani mwingine mwenye guts za ku deal na ufisadi wa level hii?!. Ni Lowassa Pekee!, hivyo uchaguzi wa mwaka huu ndio ile siku ya tatu...

Pasco
 
Pasco, na timu inayomzunguka ina uzoefu wa kutosha kabisa katika agenda hii. Mh Chenge, Karamagi na Rostam to mention a few. Yes Edward ndio mgombea sahihi nakubaliana na Pasco
 
Last edited by a moderator:
Philosopher without philosophy. . . . . . . . .
Ila pia kuwasoma kina Socrates na Plato na kuwaelewa kunahitaji level fulani ya uelewa!. Hata Masiya, sio wote walimwelewa ndio maana kuna wengine wa kuwafafanulia ili wale wazito wa kuelewa filosofia na wao pia waelewe!, ndio maana hata kwenye hili bandiko langu la filosofia ya ufisadi, msomajia asiye mwana filosofia, atatoka kapa na kuishia kuita
"Philosopher without philosophy!".
Pasco
 
Pasco, na timu inayomzunguka ina uzoefu wa kutosha kabisa katika agenda hii. Mh Chenge, Karamagi na Rostam to mention a few. Yes Edward ndio mgombea sahihi nakubaliana na Pasco
Ni kweli hii timu imesheheni!, umemsahau Mama Tiba, na kati ya watia nia hao 30 wa CCM, watia nia 15 ni wa kwake!.

Pasco
 
Mgombea yeyote awe wa CCM au upinzani ni lazima ajue kuwa ajenda kuu ya uchaguzi mwaka huu ni ufisadi.

Trust me hiyo agenda ni pana sana na hakuna atakayebaki kuanzia CCM hadi huko UKAWA.
Unaweza ukawa unajidanganya kuwa wapo wasafi ila nakuhakikishia sio CCM wala UKAWA, kote pameoza ukitumia kigezo hiki cha Ufisadi.
Tafakari mara mbili mbili.
Ukihadithiwa madubwasha wanayofanya viongozi unaowadhani ni wasafi utaomba masikio yako yasingekuwa yanasikia.
Luku vere
 
Ila pia kuwasoma kina Socrates na Plato na kuwaelewa kunahitaji level fulani ya uelewa!. Hata Masiya, sio wote walimwelewa ndio maana kuna wengine wa kuwafafanulia ili wale wazito wa kuelewa filosofia na wao pia waelewe!, ndio maana hata kwenye hili bandiko langu la filosofia ya ufisadi, msomajia asiye mwana filosofia, atatoka kapa na kuishia kuita "Philosopher without philosophy!".
Pasco

Napenda ujasiri wako tu . . . . ., .kusimamia unachoamini regardless of the ontology and epistemology behind your derivation so to say you real never bother on effects but passion and satisfaction

Sometimes you need to "set a thief to catch a thief" hii ni premise au conclusion au ni linking thread kati ya unachopenda na uhalisia???!!!

Philosopher without philosophy. . . . . . .
 
Ninakubaliana nawe 100%. Nilitundika makala yangu hapa jana kama sledi inayojitegemea lakini ikapotezewa. WanaJF wanapenda sana sledi zinazotaja majina ya watu na sio zinazotoa hoja. Nilikuwa nimeibatiza "Hii ni hoja, si kihoja: uchaguzi huu ni kati ya UFISADI vs. UZALENDO." Hoja niliyokuwa natoa ni kama hii lakini niliiweka katika muundo wa makala, tena fupi (kitu ambacho wabongo ni mtihani huo):

Wahenga walinena “Lila na fila havitangamani”.
Vivyo hivyo ufisadi na uzalendo havitangamani.
Tanzania, ama ukipenda iite Tanganyika na Zanzibar, kama taifa tumekabiliwa na maadui wakuu kadhaa tokea tupate uhuru. Katika miongo kama miwili, mitatu ya mwanzoni tuliweza kubaini maadui wakuu wapatao wanne ambao ni UMASKINI, UJINGA, MARADHI na RUSHWA. Sio tu kwamba maadui hawa wameendelea kututesa hadi leo, miaka zaidi ya 50 tokea tupate uhuru, bali pia wamejiimarisha na kuimarishwa na sisi wenyewe. Ni mzunguko pia, mzunguko usio na mwisho – kila adui anazaa na kuimarisha mwingine. Umaskini huzaa ujinga na maradhi, ujinga huzaa ama huimarisha umaskini, maradhi na rushwa, nk. Watu wengine vitu kama hivi huviona kama laana. Haishangazi kusikia msemo maarufu mitaani kwamba “aliyeturoga aliishakufa na tunguli zake.” Yaani tumekwama.

Mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi na hata kitamaduni kuanzia miaka ya tisini pamoja na kuleta mambo mazuri yenye manufaa kwa jamii, yalifungua milango na tukaanza kuona ujio wa adui mama wa wote – UFISADI. Pamoja na ukweli kwamba ni adui mdogo kiumri akilinganishwa na watangulizi wake, lakini ni mama wa maadui wote kwa sababu kuibuka kwake kumesababisha vita dhidi ya watangulizi kuwa ngumu na badala yake wameimarika zaidi. Kwa maneno mengine, UFISADI umesababisha maadui wakongwe (UMASKINI, UJINGA, MARADHI, na RUSHWA) kuwa imara na endelevu. Ukilalamika baadhi ya wananchi watakwambia hilo mbona kawaida!

Ni suala la mjadala kuhusu ni lini adui UFISADI aliibukia katika jamii yetu! Ni halali kusema kuwa fikira za kifisadi na hata ufisadi wenyewe umekuwepo miaka yote kutokana na hulka ya binadamu ikiwa ni pamoja na uchoyo, uroho, ubinafsi na hali kama hizo. Hata enzi za awamu ya kwanza ufisadi ulikuwepo japokuwa kwa kiwango cha chini na ukifanywa kwa siri. Wakati mwingine ulichukua sura ya ‘ubadhirifu’. Hayati Moringe Sokoine (pumzika kwa amani), kwa mfano, yeye aliuona kama uhujumu uchumi na hakusita kuchukua hatua kali. Enzi hizo ilikuwa ni kawaida kusikia maafisa serikalini ‘wakistaafishwa kwa manufaa ya umma’ pindi palipojitokeza dalili za kufisidi. Uzalendo ulitamalaki.

Lakini ikumbukwe kwamba uzalendo ni utamaduni na hauji kwa bahati nasibu kama mvua, bali hutengenezwa, hujengwa. Awamu ya kwanza chini ya Hayati Mwalimu Julius Nyerere (pumzika kwa amani) ulilitambua ili na ulijaribu kubuni msingi wa kujenga uzalendo. Maadili ya Uongozi, yaliyokuwa kama sehemu ya Azimio la Arusha, lengo lake lilikuwa ni kudhibiti hulka ya binadamu ya uchoyo, uroho, na ubinafsi ambavyo vikiachiwa huzaa ufisadi. Kwa kudhibiti ufisadi, maadili ya uongozi yalikuwa ni msingi wa kujenga uzalendo. Viongozi wakiwa wazalendo na kuonesha uzalendo, ni rahisi sana kwa wanaoongozwa au kutawaliwa kujenga moyo wa uzalendo. Watawala wakiwa mafisadi, hata wale wanaotawaliwa hufikiri kifisadifisadi hata kama hawako katika nafasi za kufisidi.

Azimio la Zanzibar (lililofuta Azimio la Arusha) lilifungua milango ya UFISADI kutoka faraghani na kuja hadharani. Kufuta maadili ya uongozi ilikuwa ni sawa na fungulia mbwa. Wananchi wakaaminishwa ufisadi ni jambo la kawaida, ni sehemu ya utandawazi, na ‘haki’ kwa wale wachache wanaopata access kwa raslimali za taifa. UFISADI ukazaa kundi dogo la ‘matajiri’ ambao wengi wao hawawezi kukuonesha vyanzo vya utajiri wao na kundi kubwa la hohehahe ambao wengi wao ni mlo mmoja kwa siku. Na katikati ya makundi haya mawili kuna makuwadi wa mafisadi ambao kazi yao ni kuwapigia debe mafisadi kila ifikapo wakati wa uchaguzi. Kazi ya makuwadi (hawa ni vijana na wazee, wanawake kwa wanaume, wasomi na wasokuwa wasomi) ni kuwarubuni mahoehahe kuwa neema inakuja iwapo watamchangua fisadi fulani kuwa rais au mbunge au diwani wao.

Mifano michache isiyokuwa na shaka inasadifu hapa kuonesha kutamalaki kwa ufisadi hususan baada ya kuzikwa kwa Azimio la Arusha na kuzaliwa Azimio la Zanzibar. Kashfa ya EPA iliyotekelezwa miaka ya mwishoni mwa awamu ya tatu chini ya Rais Benjamin Mkapa na kuanikwa hadharani na wazalendo wapinzani katika miaka ya mwanzo ya awamu ya nne chini ya Rais Jakaya Kikwete. Ilikuwa ni wakati huu ambapo neno ‘ufisadi’ lilipata mashiko kwa maana ya ‘wizi wa raslimali za taifa unaoratibiwa na mfumo usio rasmi ndani ya serikali.”

Rais Jakaya Kikwete alikuwa na fursa ya kipekee ya kukemea na kutokomeza utamaduni huu kwa vile ulikuwa bado haujashika mizizi. Ndio ulikuwa unachipua. Na kama angefanya hivyo, leo hii tungekuwa tunasimulia masimulizi mengine! Haishangazi kwa nini alipata ushindi wa kishindo mwaka 2005 – wananchi walishaanza kuonja madhara ya ufisadi na walimwona kama mzalendo na asiyekuwa na tamaa ya utajiri wa wizi (ufisadi). Lakini ama kwa makusudi au kwa kutofahamu (sehemu ya udhaifu wake), Rais Kikwete hakuifanya kazi ya kutokomeza ufisadi kama mojawapo ya ajenda zake za kukumbukwa katika historia ya taifa hili. Hata hivyo sina uhakika kama alikuwa na ajenda yo yote mahususi!! Yawezekana ilikuwa ni kwa makusudi kwa sababu ndio mfumo uliomwezesha kuingia madarakani (kumbuka kusudi kubwa la ufisadi wa EPA ilikuwa ni kuwezesha ushindi wa CCM japokuwa wajanja walijiwekea mifukoni mwao). Kama binadamu ye yote yule alijikuta ana kigugumizi ama mtihani mgumu kukaripia ufisadi.

Lakini mitihani ya aina hiyo ndio huwa vipimo vya uongozi – bora au dhaifu. Alipaswa kujiweka juu ya zaidi ya mwananchi wa kawaida kimaono na kimkakati kwa kutumia mamlaka aliyokuwa nayo ya uenyekiti wa Chama tawala, kiserikali/kidola na kikatiba kukemea kwa nguvu zote na hatimaye kutokomeza ufisadi kabla ya kustawi – Waingereza wakisema once and for all! Hilo hakulifikia na huo ndio udhaifu katika utawala wake. Na matokeo yake kashfa za kifisadi ziliendelea chini ya utawala wake. Bila kupoteza muda inasadifu kutaja mifano miwili ya ufisadi wa Richmond na Escrow.

Watanzania walio wengi wanachukia UFISADI kwa sababu wanapata madhara yake moja kwa moja ikiwa ni pamoja na huduma hafifu za elimu, utabibu, maji na umeme na miundombinu. Haishangazi rasimu ya Katiba Mpya (almaarufu Rasimu ya Mzee Warioba) iliyokuwa imeyatendea haki maoni ya wananchi, ilikuwa na vifungu maalumu vilivyokuwa vinapendekeza kurejeshwa kwa maadili ya uongozi. Kwa makusudi Rais Kikwete na wenzake napo wakashindwa kuonesha nia ya kuchukia ufisadi. Wakaishambulia rasimu ya mzee Warioba na kutengeneza waliyoona inafaa kwa kutupilia mbali maoni ya wananchi ikiwa ni pamoja na maadili ya uongozi. Ninaweza kusema kuwa Mheshimiwa Kikwete hapa hakushindwa mtihani, bali alishindwa quiz. Kwa hali ya kawaida ungefikiria kuwa Rais Kikwete angeiona kama fursa ya pili na ya mwisho kujiunga na upande wa wanyonge ili historia imkumbuke hivyo. Hadi leo hii hatuna uhakika na hatima ya Katiba iliyopendekezwa na CCM, yaani Katiba ya Kikwete!!

Lakini tuna uhakika kwamba uchaguzi mkuu utafanyika Oktoba 25, 2015 kwa mujibu wa Katiba ya sasa ya mwaka 1977. Katika uchaguzi huu wananachi watakuwa wanachagua ama UFISADI endelevu au safari mpya ya kurejesha UZALENDO. Mafisadi na makuwadi wao ni kikundi kidogo sana lakini chenye nguvu kubwa ya fedha. Uwezekano ni mkubwa kuweza kuwarubuni wananchi ambao ni mahohehahe kutokana na ufisadi huo huo. Tayari hilo ni dhahiri katika mchakato wa kutafuta wadhamini kwa watangazania wa chama tawala. Walalahoi wanakiita kipindi cha mavuno. Wanachama wapya wa CCM wanaibuka kila siku. Kila mtia nia ana tani za kadi za uanachama. Mkakati ni ‘tunakuwezesha kwa kuchukua kadi ya chama ili utuwezeshe.’ Hatujui hata kama makao makuu ya chama wana udhibiti wo wote wa kadi za uanachama. Haitashangaza watu kujiandikisha mara tatu au nne katika daftari la wapiga kura la BVR za kichina. Hii ndiyo nguvu ya pesa.

Wazalendo ni wengi sana bila kujali ni wanachama au wasahabiki wa chama kipi. Hata ndani ya CCM wapo wazalendo wengi – wanachama, mashabiki, na viongozi. Wale hohehahe wananunuliwa. Wale walio nacho nao hawataki kujionesha waziwazi kulaani ufisadi kwa sababu hawana uhakika iwapo dola itaangukia mikononi mwa mafisadi au wazalendo. Ikitokea dola ikaangukia mikononi mwa mafisadi basi wanaweza kukumbukwa na kutupiwa makombo. Hata hivyo, Umma wa wapenda uzalendo ukihamasishwa na kuelimishwa vilivyo unaweza kujiletea ushindi – mabadiliko yatakayonufaisha kizazi hiki na vijavyo.

Eneza ujumbe kuanzia katika familia hadi taifa: UFISADI NI ADUI MKUU WA MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA. KULA MAFISADI, KURA WAZALENDO (wa aina zote – UKAWA, CCM, ACT, nk)

Mpiga Zeze
Nansio, Ukerewe.
 
Nakubaliana na wewe kwa asilimia 100%, tena isiwe tuu ni ufisadi bali pia rais wa nchi yetu lazima awe ni mtu mwenye long expiriaence ya uzoefu wa muda mrefu kwenye ajenda hiyo, nikimaanisha ili kuweza kumkamata mwizi, sometimes one has to 'set a thief to catch a thief!', hivyo mgombea pekee wa CCM mwenye sifa hiyo ni one and only Edward Ngoyai Lowassa, ndiye pekee mwenye uwezo wa kupambana na ufisadi kwa sababu sio tuu anaujua, bali yeye mwenyewe anatuhumiwa kuwa fisadi, hivyo ndiye pekee mwenye uwezo wa kupambana na ufisadi!.

Mtu yoyote asiye lijua tatizo kamwe hawezi kupambana nalo!, ili mtu uweze kupambana na tatizo, ni kwanza yeye mwenyewe ulijue tatizo, chanzo chake, na jinsi ufisadi unavyotekelezwa, hivyo kuwa na uwezo wa kupambana kwa kuzijua mbinu zote!.

Mfano hai ni ufisadi wa iliyokuwa City Water, Lowassa akiwa ni waziri wa Maji, baada tuu ya kuujua ufisadi wao, aliwatimulia mbali, wakafungasha virago vyao na kukimbilia mahakama ya usuluhishi kule London, nako tukawatwangwa, sasa imebaki tuu historia ya utendaji uliotukuka wa Edward Lowassa!.

Hivyo Lowassa ndio mtu pekee anayeujua sio tuu anayeujua ufisadi wa Tanzania nje ndani!, bali pia ndio mwenye uwezo wa kukabiliana nao na kuukomesha!. Mfano mzuri ni kwenye ufisadi wa Richmond!, Lowassa alishuhudia jinsi ufisadi huo unavyolitafuna taifa hili na uko kwenye level gani!, kwa ushujaa wa ajabu, akaamua kujitoa mhanga, yeye mwenyewe, kwa nafsi yake, kuibeba dhambi ya ufisadi huo uliotaka kuliangamiza taifa ili yeye ndiye ateketee lakini taifa liokoke!.

Ni kweli aliibeba hiyo dhambi na akafa nayo, kama yule aliyekuja kuzibeba dhambi za ulimwengu huu, ambapo kwa kupigwa kwake, sisi tuliponywa!, alikubali kudhalilishwa, kuteswa hadi kifo msalabani, lakini siku ya tatu, alifufuka na kwenda kwenye uzima wa milele huku amekaa kulia kwenye kiti cha enzi!.

Vivyo hivyo ufisadi wa Richmond, bado uko vile vile, Lowassa aliubeba msalaba ule ili taifa liokoke!, tofauti na yule aliyebeba dhambi za Ulimwengu, dhambi ya Richmond haikuisha kwa kujiuzulu kwa Lowassa, bali baada ya Lowassa kukaa pembeni, wenye Richmond yao, ambayo waliibadili jina kuwa Dowans, wakaishitaki Tanzania kule London, wakashinda!, Tanzania ikajidai haitalipa tozo ya Dowans, ila tozo ile imelipwa 'kisiri siri', Dowans ikajibadili tena jina kuitwa Simbion!, ufisadi ule unaendelea hadi kesho, mitambo ni ile ile!, capacity charge ni ile ile!, ila jina sasa ni Simbion!, na wanaendelea kupiga hela kama kawa!.

Mtanzania gani mwingine mwenye guts za ku deal na ufisadi wa level hii?!. Ni Lowassa Pekee!, hivyo uchaguzi wa mwaka huu ndio ile siku ya tatu...

Pasco

Hivi Pasco unahitaji kufa kwa kujifungua ili utambue vifo vya wajawazito ni tatizo?
 
Last edited by a moderator:
Trust me hiyo agenda ni pana sana na hakuna atakayebaki kuanzia CCM hadi huko UKAWA.
Unaweza ukawa unajidanganya kuwa wapo wasafi ila nakuhakikishia sio CCM wala UKAWA, kote pameoza ukitumia kigezo hiki cha Ufisadi.
Tafakari mara mbili mbili.
Ukihadithiwa madubwasha wanayofanya viongozi unaowadhani ni wasafi utaomba masikio yako yasingekuwa yanasikia.
Luku vere
Ni heri asibaki hata mmoja!
 
Nakubaliana na wewe kwa asilimia 100%, tena isiwe tuu ni ufisadi bali pia rais wa nchi yetu lazima awe ni mtu mwenye long expiriaence ya uzoefu wa muda mrefu kwenye ajenda hiyo, nikimaanisha ili kuweza kumkamata mwizi, sometimes one has to 'set a thief to catch a thief!', hivyo mgombea pekee wa CCM mwenye sifa hiyo ni one and only Edward Ngoyai Lowassa, ndiye pekee mwenye uwezo wa kupambana na ufisadi kwa sababu sio tuu anaujua, bali yeye mwenyewe anatuhumiwa kuwa fisadi, hivyo ndiye pekee mwenye uwezo wa kupambana na ufisadi!.

Mtu yoyote asiye lijua tatizo kamwe hawezi kupambana nalo!, ili mtu uweze kupambana na tatizo, ni kwanza yeye mwenyewe ulijue tatizo, chanzo chake, na jinsi ufisadi unavyotekelezwa, hivyo kuwa na uwezo wa kupambana kwa kuzijua mbinu zote!.

Mfano hai ni ufisadi wa iliyokuwa City Water, Lowassa akiwa ni waziri wa Maji, baada tuu ya kuujua ufisadi wao, aliwatimulia mbali, wakafungasha virago vyao na kukimbilia mahakama ya usuluhishi kule London, nako tukawatwangwa, sasa imebaki tuu historia ya utendaji uliotukuka wa Edward Lowassa!.

Hivyo Lowassa ndio mtu pekee anayeujua sio tuu anayeujua ufisadi wa Tanzania nje ndani!, bali pia ndio mwenye uwezo wa kukabiliana nao na kuukomesha!. Mfano mzuri ni kwenye ufisadi wa Richmond!, Lowassa alishuhudia jinsi ufisadi huo unavyolitafuna taifa hili na uko kwenye level gani!, kwa ushujaa wa ajabu, akaamua kujitoa mhanga, yeye mwenyewe, kwa nafsi yake, kuibeba dhambi ya ufisadi huo uliotaka kuliangamiza taifa ili yeye ndiye ateketee lakini taifa liokoke!.

Ni kweli aliibeba hiyo dhambi na akafa nayo, kama yule aliyekuja kuzibeba dhambi za ulimwengu huu, ambapo kwa kupigwa kwake, sisi tuliponywa!, alikubali kudhalilishwa, kuteswa hadi kifo msalabani, lakini siku ya tatu, alifufuka na kwenda kwenye uzima wa milele huku amekaa kulia kwenye kiti cha enzi!.

Vivyo hivyo ufisadi wa Richmond, bado uko vile vile, Lowassa aliubeba msalaba ule ili taifa liokoke!, tofauti na yule aliyebeba dhambi za Ulimwengu, dhambi ya Richmond haikuisha kwa kujiuzulu kwa Lowassa, bali baada ya Lowassa kukaa pembeni, wenye Richmond yao, ambayo waliibadili jina kuwa Dowans, wakaishitaki Tanzania kule London, wakashinda!, Tanzania ikajidai haitalipa tozo ya Dowans, ila tozo ile imelipwa 'kisiri siri', Dowans ikajibadili tena jina kuitwa Simbion!, ufisadi ule unaendelea hadi kesho, mitambo ni ile ile!, capacity charge ni ile ile!, ila jina sasa ni Simbion!, na wanaendelea kupiga hela kama kawa!.

Mtanzania gani mwingine mwenye guts za ku deal na ufisadi wa level hii?!. Ni Lowassa Pekee!, hivyo uchaguzi wa mwaka huu ndio ile siku ya tatu...

Pasco

Taifa liokoke kwa kipi? Uamuzi wa busara ulikuwa kukataa ku-sign ule mkataba kwa sababu alijua una walakini na Richmond ilikuwa kampuni hewa lakini kwa umbumbumbu wake alisign. Hana cha kujitetea hapa asingesign Taifa lisingeingia hasara na huo ndo ulikuwa Uamuzi sahihi.
Tumelipa Tsh. 152mil kwa siku kwa Kampuni hewa, Tukalipa zaidi ya 90bn kama faini kwa DOWANS yote ni kwa sababu ya LOWASA. Halafu unakuja kumtetea mtu ambaye maamuzi yake mabovu ambayo yeye anajinadi ni magumu yameligharimu Taifa pesa mingi sana.
 
Naam.

Wakati ajenda ya mwaka huu ni UFISADI (wizi) na wakati akina Pasco wakiamini mtu wao ataweza kuwakamata mafisadi (wezi) wenzie kwasababu ana uzoefu wa kuiba bado sijaona popote jamaa yao huyo ambapo amesimama na kusema prime ajenda yake itakuwa ni UFISADI, sijaona. Na hawa ndugu zetu wanasahau kwamba tabia ni sawa na ngozi ya mtu, wanasahau kwamba kitabia na mienendo bina adamu haridhiki mpaka kufa kwake, wao hili hawalioni.

Mifano ipo mingi sana katika hili, akina Sesseko Mobutu, Dangote, Bill Gates n.k ni matajiri wa kutupwa na bado mpaka leo hawajaridhiki, bado wanatamani zaidi kwa njia zote harali na haramu.

Na ajabu ya Pasco, anakubali Lowassa ni fisadi ila wanaamini Lowassa akiwa raisi eti ataivua tabia yake hiyo na badala yake ataanza kuwakamata mafisadi wenziwe, hii ni hatari ya karne, eti shetani awe adui na shetani mwenzie, eti shetani atatenda mema! haya bwana, ila madhara ya hoja kama hii yataanza kuonekana ukweli tena ulio mchungu kwa watanzania wenzangu.

Pasco, siasa maana yake ni pale tunapokubaliana kuuweka ukweli pembeni na kuanza kuongea uongo kwa kuusafisha kwa sabauni, hiyo ndo siasa.
 
Taifa liokoke kwa kipi? Uamuzi wa busara ulikuwa kukataa ku-sign ule mkataba kwa sababu alijua una walakini na Richmond ilikuwa kampuni hewa lakini kwa umbumbumbu wake alisign. Hana cha kujitetea hapa asingesign Taifa lisingeingia hasara na huo ndo ulikuwa Uamuzi sahihi.
Tumelipa Tsh. 152mil kwa siku kwa Kampuni hewa, Tukalipa zaidi ya 90bn kama faini kwa DOWANS yote ni kwa sababu ya LOWASA. Halafu unakuja kumtetea mtu ambaye maamuzi yake mabovu ambayo yeye anajinadi ni magumu yameligharimu Taifa pesa mingi sana.
Mkuu ukiambia you ignorant, usilalamike kuwa unatukanwa, ignorant maana yake ni mjinga, na mjinga ni kutojua, ukishaufuta ujinga, unakuwa sio mjinga tena maana sasa umejua!, kwa vile ulichoandika hapa ulidhani unajua, kumbe hujui, huo ni ujinga!, kazi yangu ni kukuelimisha tuu ili ujue!.

  1. Richmond kweli ni kampuni hewa!, lakini mitambo ya Richmond sio mitambo hewa, ni mitambo ya ukweli!. Gharama za milioni 152 kwa siku, sio za gharama za kulipia jina la Richmond, ni gharama za kuilipia hiyo mitambo kwa siku!, na hapo bado gharama za kulipia umeme unaofuliwa na mitambo ile, na umeme huo huo sio umeme hewa ni umeme kweli!. Ungekuwa na akili, ungeuliza hizo fedha milioni 152 kwa siku zinalipwa kwa nani?!.
  2. Lowassa hakusaini chochote kwenye dili ile, bali alikuwa akipeleka maelekezo ya mwenye mitambo yake!.
  3. Kamati ya Mwakyembe aliposhauri mkataba uvunjwe tuu na hakuna kitakachotokea, mkataba ukavunjwa, Tanzania tukapigwa faini ya bilioni 90, bungeni wakaahidiwa hatulipi. Kwa taarifa yako, tozo ile tumeilipa kisiri siri!, umeme umepandishwa kufidia na Watanzania tunakamuliwa hadi kesho!. Ungekuwa na akili ungeuliza kama serikali iliahidi hailipi, imekuwaje tena tumelipa?, kwa nini tulipe kisiri siri/, na hizo fedha zimelipwa kwa nani?!. Na baada ya kulipishwa waliojitia kimbelembeli kuwa eti hatulipi, wako wapi, wamefanywa nini?!, Tanzania inhekuwa Chini, saa hizi hao jamaa ingekuwa ni historia tuu!.
  4. Zitto akashauri ama tuitaifishe mitambo au tuinunue!, maji yalipopungua, serikali yetu ikaamua kuiwasha mitambo ya IPTL yenye kutumia gharama mara 100 ya Dowans, huki ikituchafulia sasa hizi ni akili au matope!.
  5. Sasa kwa taarifa yako, ule mkataba wa kinyonyaji wa Richmond, bado upo, na ile capacity charge ya shilingi milioni 152 bado inalipwa daily!. Mitambo ya Dowans ndio hii, mitambo ya Simbion na mkataba ndio ule ule!, walio ilaani Richmond ndio walio ishangilia Simbion!. Nilifikiri ungetaka kujua ilikuwa tunaendelea kulipa, na anayelipwa hizi fedha ni nani?!.
Laiti ungelijua Lowassa kabeba zigo la nani, na kavumilia kiasi gani, utakubaliana na mimi, kama nampa pekee ya kumshukuru ni kumpatia urais kama asante yake, bora hata huo urais apewe, tusonge mbele, kuliko akinyimwa na akaamua kusema, huo ndio utakuwa mwisho wa kitu kinachoitwa CCM.

Laiti mngelijua Simbion ndio ile ile Richmond na capacity charge ile ile, mkataba ule ule, watu humu msingesema, mngejinyamazia tuu kama Lowassa!. Hutuoni watu humu tumejinyamazia usidhani ni wajinga!, tuna maana yetu!.

Pasco
 
Back
Top Bottom