Kuelekea Tamasha la fiesta Mr 2 akamatwa na Polisi.

Likwanda

JF-Expert Member
Jun 16, 2011
3,910
1,131
Habari kutoka TBC fm zinaeleza kuwa Mbunge wa Mbeya mjini Mh Joseph Mbilinyi a.k.a Mr 2 anashikiliwa na Polisi akihojiwa kwa kosa la kufanya mkutano huko Nzovwe bila ya kuwa na kibari cha Polisi. Msemaji wa CHADEMA mkoani Mbeya ameiambia TBC fm kuwa walienda Polisi kuwajulisha kuwa Mh Sugu atakuwa na mkutano wa kuongea na Watu wake na Sio mkutano wa Hadhara, hivyo wamelishanga jeshi la polisi kwa kumshikili Mbunge huyo. Menye update za habari hii naomba watujuze zaidi kama ni kukosa kibari au lile sakata la Tamasha la fiesta?
 
huo ni muendelezo wa kamata kamata kwa wabunge wa chadema!mpaka 2015 itakua hakuna mwana chadema licha ya wabunge ambaye hana kesi ya kubambikiziwa!
 
Juzi walivyokesha wana TANU mnazi mmoja sheria inaruhusu mkusanyiko wa watu baada ya saa 12 jioni?au ukivaa magamba ya kijani hakuna tatizo
 
Hizo ndo intelejensia za Magamba! kweli nchi hii bado inaishi kwenye zamam za Ujamaa
 
na UJAMAA na KUJITEGEMEA zinabaki kuwa nguzo na sera muhimu kwa taifa letu kuelekea MAENDELEO CHANYA
 
Nahisi kuna watu wanataka kumwonyesha Sugu kwamba pamoja na ubunge wake, wenyewe ndo wameshika mpini. Sugu nae naona ameamua kukomaa nao. Kwa kifupi, hii bado ni movie ya Maleria no more!
 
Back
Top Bottom