Kuelekea kumpata mgombea urais kwa tiketi ya UKAWA, usomi kuwa kigezo?

Waridi

JF-Expert Member
Mar 30, 2008
1,025
172
Wakuu,
Habari za uhakika ni kuwa leo katika mkutano wa waandishi wa habari, NCCR kimekuwa chama cha tatu kumtaja mgombea wake mtarajiwa.

Yaelekea ukawa utapambanisha wasomi.

CUF wanakuja na Profesa

NCCR wanakuja na Dokta

NLD nao wamemtaja Dokta

CHADEMA bado kimya, lakini yaelekea watamtaja Dokta.

Habari zaidi kwenye media leo na kesho.

Ni miaka takribani ishirini tangu Watanzania tulipoanza kuchagua viongozi wetu wa nchi tukiwa ndani ya mfumo wa vyama vingi. Katika miaka yote hiyo CCM imeweza kushinda chaguzi katokana na uchanga wa vyama vya siasa vilivyoshiriki uchaguzi miaka hiyo ya nyuma.

Pia uzoefu wa chama tawala katika siasa za Afrika umesaidia sana katika ushindi wao. Katika chaguzi za karibuni yaani kuanzia mwaka 2000, chama cha Upinzani cha CUF kilionekana kukubalika sana miongoni mwa Watanzania, CCM kwa kuona hatari iliyokuwa ikiwakabili huko mbele wakatafuta eneo la udhaifu lililoko ndani ya CUF kisha wakalitengenezea propaganda ili kuidhohofisha CUF, na kwa vile CUF hawakuwa wamejiandaa kukabiliana na propaganda za na namna ile kutoka CCM wakajikuta wanayumba na kudhohofika kisiasa.

Kuanzia mwaka 2010 CHADEMA wakaibuka kama chama chenye nguvu zaidi kisiasa kiasi kuitikisa CCM vilivyo katika mwaka huo wa uchaguzi. Lakini kama ilivyokuwa kwa CUF, CCM walifanikiwa kuona upenyo wa kuishambulia CHADEMA kwa propaganda zile zile walizozitumia dhidi ya CUF. Kwa mara nyingine tena Watanzania wakakawizwa kupata utawala walio utamani wa chama mbadala.

Muungano wa vyama vya siasa nchini ni jambo lililokuwa linangojewa kwa hamu kubwa na Watanzania wengi katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu 2015 katika wakati ambao wananchi wameichoka mno CCM,hasa huu muungano unaohusisha vyama viwili vyenye wafuasi wengi hapa nchini vya CHADEMA na CUF. Hii ni hatua moja kubwa sana kuelekea kuiondoa CCM madarakani,hatua inayofuata kwa UKAWA ili kuitoa CCM madarakani ni kumtafuta mgombea wa urais atakayekubalika kirahisi na pande zote mbili.

Kama atapatikana mgombea wa urais atakayeweza kukubalika na WanaCUF na WanaCHADEMA kwa urahisi basi kazi ya kuifurusha CCM madarakani itakuwa rahisi kama kuvunja biskuti kwa meno. Mgombea wa urais wa UKAWA licha ya kuwa na sifa stahiki za kuongoza ofisi kubwa kama ya urais lakini pia aweze kukubalika na Watanzania wa imani tofauti tofauti hasa miongoni mwa wafuasi wa imani kubwa mbili hapa Tanzania, za Wakristu na Waislamu.

Mgombea wa urais atakayeweza kuzileta imani hizi mbili pamoja dhidi ya adui mmoja ambaye ni CCM. UKAWA (CHADEMA, CUF,NCCR-Mageuzi na NLD) tunaamini busara yenu katika kutuletea mgombea sahihi wa urais atakayeweza kuing'oa CCM madarakani
 
Wakuu,
Habari za uhakika ni kuwa leo katika mkutano wa waandishi wa habari, NCCR kimekuwa chama cha tatu kumtaja mgombea wake mtarajiwa.
Yaelekea ukawa utapambanisha wasomi.
CUF wanakuja na Profesa
NCCR wanakuja na Dokta
NLD nao wamemtaja Dokta
CHADEMA bado kimya, lakini yaelekea watamtaja Dokta.
Habari zaidi kwenye media leo na kesho.
Kama UKAWA watautumia usomi kama kigezo, they will be doing a grave mistake!.
Kigezo kiwe, uwezo, kukubalika na kuchagulika!. Mfano, kwa usomi, Lipumba ndie msomi zaidi, lakini aligombea mara 4 kupitia CUF na mara zote alikataliwa!, kama hawafanya utafiti kwa nini Lipumba alikataliwa na kumfanya mgombea wa UKAWA kwa matumaini kura za Chedema na NCCR ndizo zitamuokoa, it will be a mistake!.

Mgombea wa UKAWA lazima ateuliwe kwa kuzingatia political dynamics na electability ya mgombea husika!, mfano baada ya 'yakhe' kukaa pale miaka 10!, kuna watu ukiwaletea 'yakhe' mwingine!, no matter how good he/she is, watampiga chini right away!.

Dr. Slaa was good ile 2010, is he still good for 2015?, anachagulika?, CCM ikimsimamisha yule 'jamaa yangu', Dr. Slaa ana chances za kufurukuta?!, vigezo kama hivyo vikizingatiwa UKAWA watamtafuta sio tuu mgombea bora, bali mgombea muafaka!.

Ningemshauri Lipumba aanze kuufikiria na ubunge, urais alishindwa, akashindwa, akashindwa tena na tena!, akisimamisha 2015, utashindwa tuu!.

UKAWA lazima ichague the winning team, na sio the losers ikitegemea kushinda!.

Pasco
 
Haya maneno ya ukweli Pasco,lakini huoni kama inatakiwa asimamishwe mgombea ambaye anakubalika na watu wengi zaid na kwa analysis ya harakaharaka namuon ni Dr.Slaa,kwa sababu huyu atahitaji kuungwa mkono tu na vyama vingine hasa CUF kwa sababu ya yale mambo ya udini,ila wakileta mtu mwingine ambaye hatokei Chadema itawagharimu sana Ukawa.
 
Last edited by a moderator:
Wakuu,
Habari za uhakika ni kuwa leo katika mkutano wa waandishi wa habari, NCCR kimekuwa chama cha tatu kumtaja mgombea wake mtarajiwa.
Yaelekea ukawa utapambanisha wasomi.
CUF wanakuja na Profesa
NCCR wanakuja na Dokta
NLD nao wamemtaja Dokta
CHADEMA bado kimya, lakini yaelekea watamtaja Dokta.
Habari zaidi kwenye media leo na kesho.

Kwa Chadema, hawana Dr aliyesomea, labda yule wa Canon laws ambazo hazina tofauti na udaktari tiba mbadala.
 
Kupatikana kwa mgombea mmoja wa urais tiketi ya UKAWA, ndio the biggest test ya UKAWA!. CUF wao wana wagombea wao wa kudumu, huu uchaguzi wa 2015, utakuwa ni mwaka wa 20!, watu bwale wale!, ili wakubali kubadilisha much sacrifices lazima zifanyikie sio tuu kwa ajili ya kushinguzi, bali kupata win win situation kwamba sio kila chama kitapata nini, bali vyama vikubali ku loose ili kwa togetherness they'll win!. Akisimama Dr, wale ma fundamentalists wa CUF watajiona Chadema ndio imeshinda!. Kwa maoni yangu, very honest opinion, kwa viongozi hawa wa vyama vinavyounda UKAWA, bado havina mgombea urais wa kuwaingiza ikulu 2015!.

..nimemsikiliza Ismail Jussa anasema Ukawa wanaweza kutafuta mtu wa nje atakayewaunganisha wote!!

..Jussa anasema wananchi wana imani kubwa sana na Ukawa kiasi kwamba mtu yeyote yule atakayekwenda kinyume na umoja huo atakuwa amejimaliza kisiasa.

..kwa upande wangu nadhani huu muungano unajibu mapungufu ya CDM na CUF, kwasababu vyama hivi viko upande mmoja wa muungano wa Tanzania. Walivyounganisha nguvu ndiyo watapata a balanced ticket ktk nafasi ya Raisi na Makamu wa Raisi.

cc Kafman
 
Mkuu Joka Kuu, nakubaliana na wewe, hapa serious head hunting, lobbying na advocacy inatakiwa sana kumpata the right candidate na akakubali!, the best option ni CCM wamtose yule 'jamaa yangu' na UKAWA wamchukue, CCM itapigwa chini kama kumsukuma mlevi vile!, UKAWA wataingia ikulu kama kuingia choo cha mlango wa gunia!.
Ila pia lazima tuambiane, ikiwa CCM itamsimamisha 'yule jamaa', then, whoever atakayesimamishwa, ni kujifurahisha tuu!.

Pasco
 
Wakuu,
Habari za uhakika ni kuwa leo katika mkutano wa waandishi wa habari, NCCR kimekuwa chama cha tatu kumtaja mgombea wake mtarajiwa.
Yaelekea ukawa utapambanisha wasomi.
CUF wanakuja na Profesa
NCCR wanakuja na Dokta
NLD nao wamemtaja Dokta
CHADEMA bado kimya, lakini yaelekea watamtaja Dokta.
Habari zaidi kwenye media leo na kesho.
Anaweza kuwa na doctorates hata 5 lakini politically akawa na uzito wa unyoya. Tunahitaji, pamoja na usomi, political heavy weight kupeperusha bango la UKAWA. Huyo Dr Kahangwa wa nccr agombee udiwani, anaweza kuwa mwenyekiti mzuri wa halmashauri.
 
Tatizo ni kwamba, ccm nao wapo makini. Wanajua kuwa, wakimtupa tu tayari anadondokea kwenye kapu la UKAWA na hapo ndo kuipoteza Ikulu moja kwa moja.
Sasa, laiti mambo yangegeuka mapema tu, jamaa akaamua kujitosa UKAWA, mkaona jinsi maccm yangelichanganyikiwa.
Mwaka huu, lazima mtu azimie kwa mbio hizi, kijiti kinaelea hewani, hata ccm hawajiamini ka zama zile. Watu wamefunguka, ndo maana kumtaja mgombea labda itakuwa siku 1 kabla ya kampeini
 
Mkuu Joka Kuu, nakubaliana na wewe, hapa serious head hunting, lobbying na advocacy inatakiwa sana kumpata the right candidate na akakubali!, the best option ni CCM wamtose yule 'jamaa yangu' na UKAWA wamchukue, CCM itapigwa chini kama kumsukuma mlevi vile!, UKAWA wataingia ikulu kama kuingia choo cha mlango wa gunia!.
Ila pia lazima tuambiane, ikiwa CCM itamsimamisha 'yule jamaa', then, whoever atakayesimamishwa, ni kujifurahisha tuu!.

Pasco
Hapana, ccm watakuwa wameingizwa Ikulu kwa mlango wa uani.
 
Kwa Chadema, hawana Dr aliyesomea, labda yule wa Canon laws ambazo hazina tofauti na udaktari tiba mbadala.

Yaan ww ni mbumbumbu kwel unawezaj kusem dr.slaa hajasoma?achen kutumika kama toilet paper wadau,usijivike akili ya maiti! tafakar chukua hatua
 
Haya maneno ya ukweli Pasco,lakini huoni kama inatakiwa asimamishwe mgombea ambaye anakubalika na watu wengi zaid na kwa analysis ya harakaharaka namuon ni Dr.Slaa,kwa sababu huyu atahitaji kuungwa mkono tu na vyama vingine hasa CUF kwa sababu ya yale mambo ya udini,ila wakileta mtu mwingine ambaye hatokei Chadema itawagharimu sana Ukawa.

Hapa naunga hojaa kabisa Mmi sioni haja ya UKawa kutafuta mtu toka cuf,nld,au nccr hapa jibu tosha Rais apendekezwwe kutoka CDM
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Joka Kuu, nakubaliana na wewe, hapa serious head hunting, lobbying na advocacy inatakiwa sana kumpata the right candidate na akakubali!, the best option ni CCM wamtose yule 'jamaa yangu' na UKAWA wamchukue, CCM itapigwa chini kama kumsukuma mlevi vile!, UKAWA wataingia ikulu kama kuingia choo cha mlango wa gunia!.
Ila pia lazima tuambiane, ikiwa CCM itamsimamisha 'yule jamaa', then, whoever atakayesimamishwa, ni kujifurahisha tuu!.

Pasco
Hutaamini macho yako huyu jamaa yako atakapotupwa nje na wala hutamwona akichukuliwa na UKAWA. Hivi kama wenyewe hawamtaki ni kigezo gani ukawa watakitumia kumchukua na watatumia dodoki gani kumsafisha ili akubalike.kama ukawa watafanya unayoyasema wewe huo ndo utakuwa mwisho wao na ccm watakuwa wameua upinzani kwa ulaini na ukawa hawatakuja kurejea tena kwenye siasa za nchi hii!

Watanzania siyo wajinga na ukawa wanajua hawawezi kujaribu ujinga huu utawagaharimu maisha yao yote. Kama ni technique ccm inataka kuitumia kuua upinzani kwa ulaini basi ukawa waingie huu mkenge mark my word watu hawatawaamini tena wapinzani na hawatakaa wapige kura tena na ccm watakuwa wanarudi madarakani bila upinzani wowote.

Huyo jamaa yako safari yake ni ngumu njia imejaa mbigiri na yuko pekupeku! Kuleni hela zake lakini mjue mnaweza kusababisha mambo ya komba huko mbele!
 
Back
Top Bottom