Kuelekea kumpata mgombea urais kwa tiketi ya UKAWA, usomi kuwa kigezo?

Hutaamini macho yako huyu jamaa yako atakapotupwa nje na wala hutamwona akichukuliwa na UKAWA. Hivi kama wenyewe hawamtaki ni kigezo gani ukawa watakitumia kumchukua na watatumia dodoki gani kumsafisha ili akubalike.kama ukawa watafanya unayoyasema wewe huo ndo utakuwa mwisho wao na ccm watakuwa wameua upinzani kwa ulaini na ukawa hawatakuja kurejea tena kwenye siasa za nchi hii!

Watanzania siyo wajinga na ukawa wanajua hawawezi kujaribu ujinga huu utawagaharimu maisha yao yote. Kama ni technique ccm inataka kuitumia kuua upinzani kwa ulaini basi ukawa waingie huu mkenge mark my word watu hawatawaamini tena wapinzani na hawatakaa wapige kura tena na ccm watakuwa wanarudi madarakani bila upinzani wowote.

Huyo jamaa yako safari yake ni ngumu njia imejaa mbigiri na yuko pekupeku! Kuleni hela zake lakini mjue mnaweza kusababisha mambo ya komba huko mbele!
Mkuu Ngonini, nimeipenda objectivity yako kumhusu huyu jaaa yangu na hatma ya upinzani Tanzania. Lets seat and watch, time will tell!.

Pasco
 
Ni miaka takribani ishirini tangu Watanzania tulipoanza kuchagua viongozi wetu wa nchi tukiwa ndani ya mfumo wa vyama vingi. Katika miaka yote hiyo CCM imeweza kushinda chaguzi katokana na uchanga wa vyama vya siasa vilivyoshiriki uchaguzi miaka hiyo ya nyuma.

Pia uzoefu wa chama tawala katika siasa za Afrika umesaidia sana katika ushindi wao. Katika chaguzi za karibuni yaani kuanzia mwaka 2000, chama cha Upinzani cha CUF kilionekana kukubalika sana miongoni mwa Watanzania, CCM kwa kuona hatari iliyokuwa ikiwakabili huko mbele wakatafuta eneo la udhaifu lililoko ndani ya CUF kisha wakalitengenezea propaganda ili kuidhohofisha CUF, na kwa vile CUF hawakuwa wamejiandaa kukabiliana na propaganda za na namna ile kutoka CCM wakajikuta wanayumba na kudhohofika kisiasa.

Kuanzia mwaka 2010 CHADEMA wakaibuka kama chama chenye nguvu zaidi kisiasa kiasi kuitikisa CCM vilivyo katika mwaka huo wa uchaguzi. Lakini kama ilivyokuwa kwa CUF, CCM walifanikiwa kuona upenyo wa kuishambulia CHADEMA kwa propaganda zile zile walizozitumia dhidi ya CUF. Kwa mara nyingine tena Watanzania wakakawizwa kupata utawala walio utamani wa chama mbadala.

Muungano wa vyama vya siasa nchini ni jambo lililokuwa linangojewa kwa hamu kubwa na Watanzania wengi katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu 2015 katika wakati ambao wananchi wameichoka mno CCM,hasa huu muungano unaohusisha vyama viwili vyenye wafuasi wengi hapa nchini vya CHADEMA na CUF. Hii ni hatua moja kubwa sana kuelekea kuiondoa CCM madarakani,hatua inayofuata kwa UKAWA ili kuitoa CCM madarakani ni kumtafuta mgombea wa urais atakayekubalika kirahisi na pande zote mbili.

Kama atapatikana mgombea wa urais atakayeweza kukubalika na WanaCUF na WanaCHADEMA kwa urahisi basi kazi ya kuifurusha CCM madarakani itakuwa rahisi kama kuvunja biskuti kwa meno. Mgombea wa urais wa UKAWA licha ya kuwa na sifa stahiki za kuongoza ofisi kubwa kama ya urais lakini pia aweze kukubalika na Watanzania wa imani tofauti tofauti hasa miongoni mwa wafuasi wa imani kubwa mbili hapa Tanzania, za Wakristu na Waislamu.

Mgombea wa urais atakayeweza kuzileta imani hizi mbili pamoja dhidi ya adui mmoja ambaye ni CCM. UKAWA (CHADEMA, CUF,NCCR-Mageuzi na NLD) tunaamini busara yenu katika kutuletea mgombea sahihi wa urais atakayeweza kuing'oa CCM madarakani
 
Mkuu Joka Kuu, nakubaliana na wewe, hapa serious head hunting, lobbying na advocacy inatakiwa sana kumpata the right candidate na akakubali!, the best option ni CCM wamtose yule 'jamaa yangu' na UKAWA wamchukue, CCM itapigwa chini kama kumsukuma mlevi vile!, UKAWA wataingia ikulu kama kuingia choo cha mlango wa gunia!.
Ila pia lazima tuambiane, ikiwa CCM itamsimamisha 'yule jamaa', then, whoever atakayesimamishwa, ni kujifurahisha tuu!.

Pasco

Team yule jamaa,hakuna jingine hapo.
 
Kupatikana kwa mgombea mmoja wa urais tiketi ya UKAWA, ndio the biggest test ya UKAWA!. CUF wao wana wagombea wao wa kudumu, huu uchaguzi wa 2015, utakuwa ni mwaka wa 20!, watu bwale wale!, ili wakubali kubadilisha much sacrifices lazima zifanyikie sio tuu kwa ajili ya kushinguzi, bali kupata win win situation kwamba sio kila chama kitapata nini, bali vyama vikubali ku loose ili kwa togetherness they'll win!. Akisimama Dr, wale ma fundamentalists wa CUF watajiona Chadema ndio imeshinda!. Kwa maoni yangu, very honest opinion, kwa viongozi hawa wa vyama vinavyounda UKAWA, bado havina mgombea urais wa kuwaingiza ikulu 2015!.

Pasco

Nakubaliana na mawazo yako. CUF bila shaka wataachiwa Zanzibar waiwakilishe UKAWA na si siri CUF Zanzibar ina nguvu na pia hakuna ubishi Tanganyika CHADEMA kina nguvu kwa hiyo kiachiwe kiwakilishe UKAWA bara. Kama CUF itang'ang'ania na Tanganyika iachiwe Kutakuwa hakuna maana ya muungano huo ambao ni chama kimoja tu kinasimamisha wagombea pabde zotekana kwamba hakuna vyama vingine. Mtihani mkuu uko kwa CUF kuhusu hili kwani huku mitaani wanadai kuwa asiposimishwa Profesa hawakubali watajitenga, hili si la kudharau tumeona mfano katika Serikali za mitaa.Busara itumike hasa kwa kuangalia vigezo kama matokeo ya serikali za mitaa.
 
Hutaamini macho yako huyu jamaa yako atakapotupwa nje na wala hutamwona akichukuliwa na UKAWA. Hivi kama wenyewe hawamtaki ni kigezo gani ukawa watakitumia kumchukua na watatumia dodoki gani kumsafisha ili akubalike.kama ukawa watafanya unayoyasema wewe huo ndo utakuwa mwisho wao na ccm watakuwa wameua upinzani kwa ulaini na ukawa hawatakuja kurejea tena kwenye siasa za nchi hii!

Watanzania siyo wajinga na ukawa wanajua hawawezi kujaribu ujinga huu utawagaharimu maisha yao yote. Kama ni technique ccm inataka kuitumia kuua upinzani kwa ulaini basi ukawa waingie huu mkenge mark my word watu hawatawaamini tena wapinzani na hawatakaa wapige kura tena na ccm watakuwa wanarudi madarakani bila upinzani wowote.

Huyo jamaa yako safari yake ni ngumu njia imejaa mbigiri na yuko pekupeku! Kuleni hela zake lakini mjue mnaweza kusababisha mambo ya komba huko mbele!
Halafu kila anayemwona kama kikwazo anataka kutoa uhai wake, sijui akiupata ukuu wa nchi ataua raia wangapi! Wacha wajanja kina Pasco watafune pesa yake.
 
Pasco upo sahihi lakini pia nataka nisisitize kuwa MGOMBEA WA KITI CHA URAIS, KAMA UKAWA TUNATAFUTA USHINDI, NI LAZIMA ATOKE CHAMA CHENYE WAFUASI WENGI. KWA SASA CHAMA AMBACHO KINA WAFUASI WENGI KWA KUTUMIA UTHIBITISHO WA MATOKEO YA UCHAGUZI 2010 NA SERIKALI ZA MITAA, NI CHADEMA.

CHADEMA INATAKIWA ITOE MGOMBEA WA KITI CHA URAIS, CUF INATAKIWA ITOE MGOMBEA WA KITI CHA UBUNGE AMBAYE ATAKUWA WAZIRI MKUU. NCCR NA NLD WATOE WAGOMBEA WA UBUNGE WATAKAOPEWA UWAZIRI KATIKA WIZARA MOJAWAPO MUHIMU.

Hakuna ndoto wala muujiza utakaoweza kuwafanya UKAWA washinde ambao utakuwa tofauti na kuruhusu chama chenye wapenzi wengi kumtoa mgombea wa kiti cha urais. CHADEMA imejitahidi sana kuwa na uongozi mpaka ngazi ya chini kabisa katika maeneo mengi. Mpaka sasa, ukiacha CCM ndiyo, CHADEMA ndiyo chama pekee cha siasa chenye mtandao mpana wa uongozi na chenye wafuasi wengi wenye mtawanyiko mpana kuliko kingine chochote.

Na kwa CHADEMA, sioni kama kuna mtu mwingine yeyote mwenye kuungwa mkono na watu wengi, na anayefahamika kwa wapiga kura wengi kumzidi DR. WILBROAD SLAA.

Kama UKAWA watautumia usomi kama kigezo, they will be doing a grave mistake!.
Kigezo kiwe, uwezo, kukubalika na kuchagulika!. Mfano, kwa usomi, Lipumba ndie msomi zaidi, lakini aligombea mara 4 kupitia CUF na mara zote alikataliwa!, kama hawafanya utafiti kwa nini Lipumba alikataliwa na kumfanya mgombea wa UKAWA kwa matumaini kura za Chedema na NCCR ndizo zitamuokoa, it will be a mistake!.

Mgombea wa UKAWA lazima ateuliwe kwa kuzingatia political dynamics na electability ya mgombea husika!, mfano baada ya 'yakhe' kukaa pale miaka 10!, kuna watu ukiwaletea 'yakhe' mwingine!, no matter how good he/she is, watampiga chini right away!.

Dr. Slaa was good ile 2010, is he still good for 2015?, anachagulika?, CCM ikimsimamisha yule 'jamaa yangu', Dr. Slaa ana chances za kufurukuta?!, vigezo kama hivyo vikizingatiwa UKAWA watamtafuta sio tuu mgombea bora, bali mgombea muafaka!.

Ningemshauri Lipumba aanze kuufikiria na ubunge, urais alishindwa, akashindwa, akashindwa tena na tena!, akisimamisha 2015, utashindwa tuu!.

UKAWA lazima ichague the winning team, na sio the losers ikitegemea kushinda!.

Pasco
 
Nijuacho Lipumba anaenda kuisambaratisha CCM jimbo la Temeke.Ndiyo Mbunge mtarajiwa wa Temeke
wanajifanya hawajui hawa - baache kama balivyo!! kete yao ya mwisho eti ni kugawanyika kwa UKAWA wakati wa michakato ya kuwapata wawakilishi wa Udiwani, Ubunge na Urais.
 
Kupatikana kwa mgombea mmoja wa urais tiketi ya UKAWA, ndio the biggest test ya UKAWA!. CUF wao wana wagombea wao wa kudumu, huu uchaguzi wa 2015, utakuwa ni mwaka wa 20!, watu bwale wale!, ili wakubali kubadilisha much sacrifices lazima zifanyikie sio tuu kwa ajili ya kushinguzi, bali kupata win win situation kwamba sio kila chama kitapata nini, bali vyama vikubali ku loose ili kwa togetherness they'll win!. Akisimama Dr, wale ma fundamentalists wa CUF watajiona Chadema ndio imeshinda!. Kwa maoni yangu, very honest opinion, kwa viongozi hawa wa vyama vinavyounda UKAWA, bado havina mgombea urais wa kuwaingiza ikulu 2015!.

Pasco

Hivi unataka kusema hakuna hata mmoja kati ya watu wa Ukawa wanaoweza kugombea na kushinda? Nami nakuunga mkono kabisa Ukawa wana mtihani mkubwa sana katika kumpata Candidate wao na nadhani Cuf kwa sababu wagombea wao walishashiriki kwa takribani miaka 20 ni bora wakajitoa tu wakashindana NLD,CHADEMA na NCCR Mageuzi ili hao wapigiwe kura ndani ya Ukawa ila suala hili linahitaji uvumilivu na busara za hali ya juu sana kulivuka hili daraja walilo nalo.
 
..nimemsikiliza Ismail Jussa anasema Ukawa wanaweza kutafuta mtu wa nje atakayewaunganisha wote!!

..Jussa anasema wananchi wana imani kubwa sana na Ukawa kiasi kwamba mtu yeyote yule atakayekwenda kinyume na umoja huo atakuwa amejimaliza kisiasa.

..kwa upande wangu nadhani huu muungano unajibu mapungufu ya CDM na CUF, kwasababu vyama hivi viko upande mmoja wa muungano wa Tanzania. Walivyounganisha nguvu ndiyo watapata a balanced ticket ktk nafasi ya Raisi na Makamu wa Raisi.

cc Kafman

Sorry kwa kuchelewa Mkuu,
Hilo litakuwa wazo zuri sana la kuweka mtu tofauti na hao wanaotajwa lakini inabidi apitie kwenye Chama kinachokubalika zaidi ili iwe rahisi kukubalika pia inatakiwa wapate ambaye ana potentiality na anayekubalika sana. Na hao wengine tofauti na chama atakachopitia wasije wakaona kama wamepoteza sana akili ya uvyama inabidi waiondoe hapo ndipo watakapofanikiwa na hii idea ni nzuri sana katika kuusaka ushindi.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Joka Kuu, nakubaliana na wewe, hapa serious head hunting, lobbying na advocacy inatakiwa sana kumpata the right candidate na akakubali!, the best option ni CCM wamtose yule 'jamaa yangu' na UKAWA wamchukue, CCM itapigwa chini kama kumsukuma mlevi vile!, UKAWA wataingia ikulu kama kuingia choo cha mlango wa gunia!.
Ila pia lazima tuambiane, ikiwa CCM itamsimamisha 'yule jamaa', then, whoever atakayesimamishwa, ni kujifurahisha tuu!.

Pasco

Lakini ndugu yangu huyo jamaa Ukawa wanajua ni kete nzuri lakini hawawezi kuitumia kwa sababu walizozieleza za kwamba kete ilochafuka saana,hata mi naunga mkono,kwani hata huko Ccm hakuna mtu msafi na mzuri zaidi ya huyu mtu au hata kutoka nje ya vyama na akasimama watu wakamuunga mkono na ushindi ukapatikana Pasco?
 
Hutaamini macho yako huyu jamaa yako atakapotupwa nje na wala hutamwona akichukuliwa na UKAWA. Hivi kama wenyewe hawamtaki ni kigezo gani ukawa watakitumia kumchukua na watatumia dodoki gani kumsafisha ili akubalike.kama ukawa watafanya unayoyasema wewe huo ndo utakuwa mwisho wao na ccm watakuwa wameua upinzani kwa ulaini na ukawa hawatakuja kurejea tena kwenye siasa za nchi hii!

Watanzania siyo wajinga na ukawa wanajua hawawezi kujaribu ujinga huu utawagaharimu maisha yao yote. Kama ni technique ccm inataka kuitumia kuua upinzani kwa ulaini basi ukawa waingie huu mkenge mark my word watu hawatawaamini tena wapinzani na hawatakaa wapige kura tena na ccm watakuwa wanarudi madarakani bila upinzani wowote.

Huyo jamaa yako safari yake ni ngumu njia imejaa mbigiri na yuko pekupeku! Kuleni hela zake lakini mjue mnaweza kusababisha mambo ya komba huko mbele!

Hata mi nakuwa nawaambia huyo hasafishiki! japo kwa wasomi na walioko mijini wanaweza kubadilika na kama kuna ukweli wakauelewa lakini walioko vijijini hawajui na hawawezi kuelewa hilo,unajua Pasco mtu akichafuka kujisafisha inahitaji muda na gharama za kutosha!
 
Last edited by a moderator:
Kwa Chadema, hawana Dr aliyesomea, labda yule wa Canon laws ambazo hazina tofauti na udaktari tiba mbadala.
Dr ni Dr tu awe wa tiba mbadala, physical education, kucheza ngoma, kuigiza, kuchora n.k jaribu wewe kusomea ndo utajua kama ni rahisi au ngumu
 
Kupatikana kwa mgombea mmoja wa urais tiketi ya UKAWA, ndio the biggest test ya UKAWA!. CUF wao wana wagombea wao wa kudumu, huu uchaguzi wa 2015, utakuwa ni mwaka wa 20!, watu bwale wale!, ili wakubali kubadilisha much sacrifices lazima zifanyikie sio tuu kwa ajili ya kushinguzi, bali kupata win win situation kwamba sio kila chama kitapata nini, bali vyama vikubali ku loose ili kwa togetherness they'll win!. Akisimama Dr, wale ma fundamentalists wa CUF watajiona Chadema ndio imeshinda!. Kwa maoni yangu, very honest opinion, kwa viongozi hawa wa vyama vinavyounda UKAWA, bado havina mgombea urais wa kuwaingiza ikulu 2015!.

Pasco

nikuulize Pasco,hivi vyama vinategemea ruzuku ambayo inapatikana kwa nafasi za ubunge wa majimboni na wale wa viti maalumu.Hesabu za kupata nafasi za wabunge wa viti maalumu inatokana na asilimia za kura za urais kwa kila chama,je kwa upande huo endapo CUF hakitakuwa na mgombea kitapataje asilimia za kupata wabunge wa viti maalumu na pia ruzuku ya kuendeshea chama ?
 
lakini ndugu yangu huyo jamaa ukawa wanajua ni kete nzuri lakini hawawezi kuitumia kwa sababu walizozieleza za kwamba kete ilochafuka saana,hata mi naunga mkono,kwani hata huko ccm hakuna mtu msafi na mzuri zaidi ya huyu mtu au hata kutoka nje ya vyama na akasimama watu wakamuunga mkono na ushindi ukapatikana pasco?

dr john pombe magufuli
 
nikuulize Pasco,hivi vyama vinategemea ruzuku ambayo inapatikana kwa nafasi za ubunge wa majimboni na wale wa viti maalumu.Hesabu za kupata nafasi za wabunge wa viti maalumu inatokana na asilimia za kura za urais kwa kila chama,je kwa upande huo endapo CUF hakitakuwa na mgombea kitapataje asilimia za kupata wabunge wa viti maalumu na pia ruzuku ya kuendeshea chama ?
Mkuu BigMan, asante kwa hili, hii ni hoja ya msingi sana!. Wengi wa members wa jf ni wanachama, wafuasi na washabiki wa vyama, ambao msingi mkubwa wa majadiliano yao ni mapenzi yao kwa vyama vyao na watu wao!.

Hili unalolizungumzia, nimelizungumza sana humu!, tangu ile 2010 Dr. Aliopogomea matokeo ya urais, niliuliza humu anagoma nini wakati ni yeye mwenyewe aridhia kuingia dimbani kwenye mashindano huku akielewa uwanja sio sawa!.

Yaani mnagombea kisu, mwenzako kashika mpini, wewe unaelekezewa kwenye makali na unakubali kushika!, ukikatwa unalalamika!.

Niliwaambia Chadema, badala ya kupigania misingi ya uchaguzi huru na wa haki, wao kazi yao kuingia kwenye chaguzi kwa kuherehere, kisha kuja kususa!. Walipaswa kupigania misingi ya haki na ushirikiano wa vyama ambapo idadi ya viti maalum itokane na idadi ya wabunge.

Mchakato wa katiba ulipoanza Chadema wali play a big role kuupitisha huo nchakato, tango mwanzo tukawaeleza matokeo!, shauri ya chai, juice na vitafunwa vya ikulu, wakayasahao yote, sasa mchakato umekamilika ndio wanajidai kusasa, wana susa nini?.

Walipoasisi UKAWA nilieleza humu jinsi UKAWA ulivyo a 'marriage of convenience' conveniences zikiisha ni kila mtu na lwake!.

Sasa its high time, wapinzani wasikubali kuingia kwenye uchaguzi bila rules of the game kurekebishwa kutengeneza level playing field kwa ushindani wa haki!. Hili la ushirikiano wa vyama likiwa ni top agenda!.

Pasco
 
Back
Top Bottom