Ulichoandika mwanzo mwisho hakina shaka hata chembe,kama wa tz hatuwezi chukua hatua tutaishia kulalamika miaka nenda rudi,pili kama hatuwezi kuchukua hatua tufanye kafara la kitaifa.angalia deni la taifa na hamna mtu anajali kweli inauma sana!
Mkuu sisi waTZ sijui tuna tatizo gani hasa yani hatuwezi kabisa kuamua kwa kauli moja hata kidogo. Nchi yenye resouce nyingi kiasi hiki lakini watawala waweka maslahi yao mbele sana sijui labda itafika siku hiyo.
Hutaki unaacha!
wakuu,
Nilikuwa na hizi information lakini nikawa natafuta uthibitisho kutoka kwa source zangu na nimehakikisha sasa namwaga hapa.
naomba tuanzie na Richmond je, mwajua kwanini maazimio yake hadi sasa hayatekelezeki? Tunafahamu kuwa mtekelezaji mzuri wa maazimio yale ya bunge ni mamlaka ya juu ambayo ni Rais lakini kwa sababu yeye mwenyewe ndiye source na mwenye ile business basi maazimio yale hadi leo ni ngumu kutekelezeka (recall huyu jamaa aliwahi kuwa waziri wa ile wizara kipindi cha mwinyi).
PILI:
Suala la Jairo je, maazimio ya bunge ameyatekeleza kwa kiasi gani? Kumbukeni pia bunge liliwahi kuitaka serikali kuvunja mkataba na TICTS lakini mpaka leo hakuna utekelezaji ni kwa sababu Rais hawajibiki ipasavyo kwa wananchi wake na sababu kubwa ni kuwa yeye mwenye huwa nyuma ya madudu mengine yanayofanywa na viongozi ndio maana alisema Jairo atapangiwa kazi nyingine na mpaka leo anadunda na usafiri wa serikali.
Hayo nilikuwa nataka kuweka base ya hoja yenyewe.
SASA KUELEKEA BARAZA JIPYA:
hizi information ni classified lakini sina jinsi naweka wazi japo mpangilio unaweza kuwa ovyo.
Hapa jamani tatizo sio hawa watendaji wakuu bali ni Mkulu mwenyewe kwa sababu kubwa ambayo ni kwamba yeye anafanya biashara kupitia migongo ya hawa watendaji wake wakuu. Suala la wizara ya miondombinu Nundu yuko right kwa sehemu kubwa lakini mkuu alimtumia Mfutakamba kwa ajili ya manufaa yake ndio maana mlisikia kibali cha kusafiri alikitoa ofisi ya juu na ni State house ndio maana Nundu alisema ule makataba ulikuwa na Interest ya 77% in turn lakini hakueleweka sasa hapa Nundu anaweza kutolewa kafara au naibu akapangiwa kazi nyingine.
Tukija kwa Maige utaona analalamika sana lakini wale wakurugenzi wanafanya madudu na hawachukuliwi hatua yoyote ni kwa sababu wako nyuma ya mgongo wake unafikiri kwanini Kamrani hachukuliwi hatua yoyote? Kiufupi huyu jamaa anfanya biashara na mkulu mwenyewe na an biashara zingine zaidi ya hizo pamoja na KUCHIMBA MADINI NDANI YA HIFADHI ZETU na KUUZA MAGARI YA WIZI KUTOKA NCHI ZA UGHAIBUNI lakini nobody says anything kwa sababu mawasiliano yake anafanya na mkulu ndio maana maofisa wa serikali wanaogopa kwenda kwake.
So, let me end up here today lakini hiyo ndiyo hali halisi kiufupi TUNA RAIS MFANYABIASHARA.
MY TAKE KWENYE BARAZA JIPYA:
Tusitegemee miujiza na wale watakaopigwa chini watapangiwa kazi zingine au hawatachukuliwa hatua zozote zile. Kuhusu watendaji wa wizara wanaweza kutolewa kwenye sehemu zao lakini hatua thabiti hazitachukuliwa kwa sababu kichosumbua nchi hii ni USHAHIDI.
Kumbukeni kuwa washauri wake wameshamshauri sana achukue hatua za kufumua pale palipo na amshaka kuanzia watendaji wabovu hadi mawaziri wao ila tatizo ni je, atamweka nani wa kufanya vile anavyotaka yeye akiwatoa hao waliopo? Ndio maana kumekuwa na kusitasita kutoa maamuzi magumu tunayoota mchana kwamba yatatokea lakini whatever happens itakuwa kiinimacho na mtasikia mengine in few years.
Najua mtauliza source ni my insider wa Ikulu na namwamini.
PIA KUMBUKENI.
kila wizara ambayo waziri na naibu wake wana misunderstanding jueni kuwa mmoja yuko anatekeleza matakwa ya mkulu wa kaya na mwingine anafuata taratibu kitu ambacho kitawa cost hawa wanaofuata taratibu kuliko wale wanaom-save mkulu.
acha njaa itupige kwanza tutie adabu ndipo tutajituma wenyewe kuingia barabarani,wakati dr slaa anatuambia kuwa tusipo mchagua tutakumbuka maneno yakd ndio sasa,na wakati wa kutia kwa ile kauli yake ya kua nchi haitatawalika,unakuja wacha njaa itupige tukifulia tutatia adabu.kitakacho tutia hasira ni pale mtu anasoma na mtoto wa kigogo mnamaliza wote yeye anapata kazi wewe una kaa kijiweni mwika kumi wakati kwanza unamzidi GPA.sasa tukiwa wengi ndio utaona kuwa hata risas,mabomu na askar havitatosha
mkuu angalia ukifunuliwa mengi unaweza kujuta kwa nini uko patmo.
Ni upepo tu, utapita.
mkuu mu-sir ulichoandika ndicho nilichofikiria miaka yote,mfano wizi wa mabilioni ya bagamoyo ni ridhiwan aliyepiga akishirikiana na watendaji na ridhiwan=jk,..
mkuu angalia ukifunuliwa mengi unaweza kujuta kwa nini uko patmo.
sote tukiwa na mawazo kama yako mkuu mbona tutaisha. Au na wewe unanufaika kwa namna yoyote ile na huu utawala wa Vasco da Gama?
Hapana Wakuu, na mniwie radhi mmenifahamu hivyo. Mimi ni miongoni mwa mamilioni ya Watanzania wanaoteseka kutokana na utawala huu. Hapa nilikusudia kukariri tu hiyo kejeli yake, "Ni upepo tu utapita - JK 22/04/2012", licha ya mashaka yote tuliyonayo, licha ya wezi kubainishwa wazi wazi, Raisi wa Mambo ya Nje a.k.a Vasco da Gama wetu anazurura Brazili, kufika hapa hiyo ndiyo iliyokuwa kauli yake ya kwanza, akaweka mizigo, akabadilisha nguo, huyoooooo mazikoni Malawi.sawa yawezekana ukawa unanufaika na mirija/diri za JK,lakin ndugu yangu ukila ukashiba jitahidi na majirani washibe kwan kikinuka ndio utajua nini tunamaanisha ktk hii thread
Hiki ni kisiwa cha upweke nitatafakari na kuchukua hatua bila kuwa influenced. Nimesoma mengi hapo ila mimi kwa moyo wangu na nafsi yangu naamini kwamba Nundu amezungukwa na genge la mafisadi na ameingia tu kwenye anga zao na wanataka kumshughulikia.
Hapana Wakuu, na mniwie radhi mmenifahamu hivyo. Mimi ni miongoni mwa mamilioni ya Watanzania wanaoteseka kutokana na utawala huu. Hapa nilikusudia kukariri tu hiyo kejeli yake, "Ni upepo tu utapita - JK 22/04/2012", licha ya mashaka yote tuliyonayo, licha ya wezi kubainishwa wazi wazi, Raisi wa Mambo ya Nje a.k.a Vasco da Gama wetu anazurura Brazili, kufika hapa hiyo ndiyo iliyokuwa kauli yake ya kwanza, akaweka mizigo, akabadilisha nguo, huyoooooo mazikoni Malawi.