Mu-sir
JF-Expert Member
- Oct 12, 2010
- 3,621
- 1,629
- Thread starter
- #21
UFISADI NDANI YA TAIFA LETU: ENYI MA-TOMASO MSIOAMINI HATA ZA 'JIKONI KWAO HAWA JAMAA' - NANI KASEMA ETI SIKU HIZI SAMAKI HUANZA KUOZA KUANZIA MKIANI HAPA???
Ni nani asiyejua kwamba walalahoi wa nchi hii mali zetu zinahamishiwa uarabuni kwa kutumia kila wizara kama wakala wa UFISADI?
Wapi uliwahi kusikia eti waziri anamgomea rais kujiuzulu kwake licha ya KUBEMBELEZWA SAAAANA KUOKOA JAHAZI kimtindo jambo analoonelea kwamba binafsi hajanufaika nayo kama si kutuambia umma wa Tanzania kiaina kwamba 'MIE NILIIBA KWA MAELEKEZO NA FAIDA YAKE YEYE huyu bana halafu leo hii nisulubiwe mimi; HAKA SIJIUZULU KITU NG'O'!!
WaTanzania, kuna tatizo tena zito ajabu pale pale Magogoni kwenyewe hivyo hata waje Waziri Zitto Kabwe au Tundu Lissu chini ya kivuli cha mbuyu huu huu bado UFISADI utaendelea kupaa kwa kasi ile ile!!!
Machimbo ya Uranium hifadhini nani mwingine tena akafanye na kule Bukombe kama si wenye meno ndani ya nchi?? Taifa hili litaendelea kutafunwa na wenye meno huku wenye moyo wakiendelea kuduwazwa na kufanywa kuonekana tu mahayawani kila kukicha.
INAUMA SANA!!!!!!!!!!
Mkuu hao jamaa hata mimi nashangaa kwa nini wasimlipue mkulu wao na nadhani kinachosababisha ni kale ka ugonjwa ketu ka USHAHIDI WA KUJITOSHELEZA!! hivi mnafikili yeye ni mjinga aache ushahidi kijinga? Hata Zitto awe waziri mkuu bado madudu yatakuwepo tu na Zitto ataonekana mchafu because of thi Bull.
Mimi nadhani Lowassa ndiye angemlipua lakini akatikisa kiberiti akidhani mkuu atambeba kumbe ndo akatupwa nafikiri huko aliko anajuuuuta kumfahamu mkulu.