Naungana na mchokoza mada na comments za RockSpider. Kila mafanikio yana kinara wake. Hatukatsi,CHADEMA kimejengwa kwa nguvu za wengi,wanachama na wafuasi.Kuna nafasi ya waasisi kama Mzee Mtei,Brown Ngwililupi, Medard Mtungi,aBob Makani na wengine. Walianzisha na kukisimika chama kwa sera na katiba ambazi ziliwagusa na kuwavutia wengi akiwamo hayati baba wa taifa. JKN aliwahi kukiri wazi juubya umakini wa CHADEMA.
Wapo waliokuwa pamoja na waasisi hawa ktk hatua za mwanzo lkn wakakata tamaa na kurudi CcM,kumbukumbu zangu zinamtambua aliyekuwa mbunge na waziri ktk awamu zote 4 za utawala wa nchi hii toka Mufindi,akitajwa kuwamo ktk CHADEMA lkn baadae akarudi kwa chama kizee. Huyu na wengine walirudisha harakati zetu nyuma,bila shaka alitishwa na maneno kuws uraia wake na uhalali wa ukwasi wake vilitiliwa shaka.
Walijitokeza warithi wa waasisi wa CHADEMA,kina Zitto,Mbowe,na Dr wa ukweli. Hawa wametenda kazi zao kwa umakini,bungeni,ktk majimbo yao na ktk jukwaa la mapambano ya hoja. Wamekuwa best models,na kuwavuta hili kundi kubwaaa la vijana machachari na makini,ndio sababu CHADEMA kimefikaktk kiwango cha kuaminiwa kushika dola.
Angalizo kuwa tusibweteshwe na hatua hii,tukadhani tumeshafika,bali tuongeze bidii. Kaxi bado haijaanza.
Mambo 2 yanapaswa kutufunza kuwa CcM wana roho ya paka shume jizi,usiridhike kuwa umeliua hadi uwe umetenganisha kichwa na kiwiliwili.
Kwanza ni ktk uchaguzi wa wawakilishi wetu kuunda mabaraza ya katiba ya wilaya. CcM walituzidi kete,wakawapitisha watu wao tu japo wengi ni semi literate na kuwaengua wana CHADEMA ambao wengi ni vijana na wasomi. Imetokea kata za Kibaoni na Ifakara,Kilombero na wilaya zingine.
Kilichotokea Kibondo ktk kuwachagua Meya na Naibu wake juzi.
Haya ni masomo tosha kwetu kuwa tuna kaxi ya kuwaelimisha mbumbumbu walio na fikra kuwa CcM bado ni baba yao. Tunapaswa kuwaandaa vijana hasa walioko sekondari na mitaani wajiunge na CHADEMA,waimaridhe BAVICHA huko waliko,na wajiandikishe kuwa wapiga kura,na siku ya uchaguzi wakakichague CHADEMA.
Huku Ifakara,juhudi hizi zinaonyesha matunda baada ya kunyakua kiti cha udiwani kata ya Ifskara. Kinachofuata ni udiwani kata ya Kibaoni tayari iuchukua kata zote na jimbo/majimbo mwaka 2015.
Mwenyekiti wetu wa mkoa,mama Susana Kiwanga,mjukuu wa TOVEGALE,anzisha vuguvugu la kukijenga chama,Kilombero,Ulanga na mkoa wote.
CHADEMA daima